Friday, February 17, 2017

#KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU!

Hivi ulishawahi kukutana na mlevi aliyezoea pombe?

ukimkaribia tu hata kama hajanywa pombe utasikia harufu ya Pombe, yaani huhitaji kuuliza utajua tu ni mlevi!

Kwa sababu kile kilevi kimemwingia ndani yake haswaaa!
Je wale wenzetu, wanaopenda kula vitunguu swaumu sana,,
yaani ukimsogelea tu, utasikia harufu ya vitunguu saumu na vile viungo vyao vingine!Akiongea ndio usiseme!!

Kwa sababu vile viungo viko ndani yake.

#Kwenye Yohana 15, Yesu anatuambia TUKAE NDANI YAKE NAE NDANI YETU!

Yeye akikaa ndani yetu ni zaidi ya hiyo mifano nliyoitoa hapo juu!!
Yaani maana yake utakua unanukia yeye, ukizungumza tutasikia yeye, iko ndani yako!

Vipi kuhusu,sisi tukikaa ndani yake inakuwaje?
Uliwahi kuwa ndani ya nyumba alafu akapita mtu kwa nje, unadhani yule mtu atakuona?
Hapana, ni mpaka aingie ndani au wewe utoke nje!
yaani ile nyumba inakua imekuficha kwa sababu uko ndani yake!

Sasa, Yesu anasema KAENI NDANI YANGU,

Yaani ukikaa ndani yake, ni wazi kuwa ili uonekane lazima au wewe utoke nje au aliyeko nje aingie ndani kupitia yeye(mlango) ndio muonane!

#SASA CHANGANYA HIZI MBILI,
KAENI NDANI YANGU, NAMI NDANI YENU!!
Yaani unakua ndani Yesu, Nje Yesu!

Kote kote Yesu!

Alafu anasema Ukishafanya hivyo, OMBA LOLOTE KWA JINA LANGU, Nawe Utapata!

#Hebu pata picha katika hicho kiwango kuna uwezekano wa kukosa utakacho?,, wakati YEYE YUKO NDANI YAKO, NA WEWE UKO NDANI YAKE!

#Amua Leo Kuwa Ndani Yake, nae Ndani Yako!
#YesuNdaniYangu!!

Tuesday, February 7, 2017

# Darasa La Hekima #KWA WAZAZI WOTE na WAZAZI WATARAJIWA WOTE.

Mzazi mpende mwanao leo,
Mwonyeshe upendo leo,
Mfundishe kumpenda Mungu leo,
Mwambie unampenda leo,

Huwezi kujua Mungu amekupa kuwa nae kwa muda gani!
Yaweza kuwa muda mfupi sana au miaka mingi sana!

Ila fanya leo.


Ukiondoka hawezi kukumbuka mali ulizoacha.. Ila ataukumbuka upendo wako..
hekima zako..
busara zako..

Usijidai uko busy sana na kazi, ukasahau familia yako..
Watoto wanakuona usiku kwa usiku au baada ya siku kadhaa..

Jua kuwa wanahitaji upendo wako..

Kama kuna kitu cha thamani unaweza kuwapa wanao leo ni MUDA wako.

Ongea nao
Sali nao
Cheza nao
Cheka nao

Ni rahisi kukumbuka tabasamu lako kuliko hata zawadi uliyowaletea!

Ni rahisi kukumbuka sala yako kuliko maneno uliyosema ulipokua unawagombeza..

Ni rahisi kukumbuka kuwa uliwaambia unawapenda kuliko matusi uliyowahi kuwatukana..

#Fanya leo
#Onyesha Upendo Leo

Wednesday, February 1, 2017

#DarasaLaHekima #TendaMemaWakatiWote

Hatufanyi mema kwa sababu tunalipa wema,
au kwa sababu tunatafuta kuja kufanyiwa mema,

#Tunafanya mema kwa sababu ni asili yetu!

#Tunafanya mema kwa sababu tumeumbiwa hayo kuyafanya!

#Tunafanya mema kwa sababu aliye ndani yetu ni mtenda mema!

#Tunafanya mema kwa sababu ni wajibu wetu!

#Tunafanya mema kwa sababu ni utamaduni wa ufalme wetu kutenda mema!

Monday, January 30, 2017

#DarasaLaHekima #NoaUpangaWako


Upanga ni upanga uwe mKali au mButu.

Lakini tofauti kati yake itaonekana wakati wa matumizi.

Upanga ulionoelewa ni mkali na unapotumika huleta maangamizi makubwa kwa wakati mmoja.

Upanga butu, hutumika pia ila madhara yake ni madogo, na huenda mtumiaji akatumia nguvu kubwa sana wakati wa kuutumia!

Maombi ni kama upanga,

Maombi yenye maarifa sahihi ya Neno la Mungu, ni kama upanga ulionolewa!

Maombi yasiyo na maarifa sahihi ya Neno la Mungu ni kama upanga butu!

#Unaweza kunoa upanga wako kila siku kwa kuhakikisha unajifunza kila siku kitu kipya kuhusu Mungu.

#Upanga wako unavyozidi kuwa mkali, ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kuutumia!

Friday, January 20, 2017

#DarasaLaHekima #Jifunze kwa mnyama Simba


Leo ntazungumza na wewe kuhusu mnyama Simba,

🦁Simba sio kwamba ni mnyama mkubwa kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mwenye nguvu kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mjanja kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mwenye mbio kuliko wote mwituni..

🦁LAKINI SIMBA NDIO MFALME WA MWITU(King of the Jungle)

🤕Akinguruma wanyama wote wanaogopa

🏃🏿‍♀🏃🏼Akitokea wanyama wote na binadamu wanakimbiaaaa

🤔Unafikiri ni kwa nini?

🦁Kwa sababu ya MTAZAMO wake.

😋Yeye akiona mnyama au mtu anaona anaona chakula                        

 🍽Yeye hajawahi kuona analiwa bali yeye ndio anakula wengine

🦁Hiyo ni sifa moja inayompa ushindi mkubwa Simba.                        

 🐝Wale wapelelezi walioenda kuipeleleza nchi ya Kanani,waliporudi kuna walioona Majitu, na Joshua na Kalebu wao waliona maziwa na asali 

👀Kilichowatofautisha ni Mtazamo wao juu ya Kanaani.

❓Je wewe unaona nini kwenye ulilonalo?

❌Ishu sio TATIZO,ishu ni Mtazamo wako juu ya hilo tatizo.

🚥Namna unavyoona mambo, ndio inategemea matokeo utakayopata kutoka kwenye hilo jambo.

📝Hatua ya kwanza ya kubadilisha jambo lolote, inaanzia kwenye mtazamo wako juu ya hiyo jambo.                        

 ⛔Badili mtazamo na utaanza kuona mwanga wa namna ya kutoka hao ulipo.

...Tutaendelea sehemu ya pili kesho
#DarasaLaHekima
#Minna2017
#JifunzeKwaMnyamaSimba

Thursday, January 19, 2017

#DarasaLaHekima #TumiaTicketYakoVizuri

Mtu mmoja akasafiri kwenye ndege akiwa na ticketi iliyokua imelipwa nauli pamoja na chakula chake cha kula njiani kwenye ticketi yake.
Akasafiri na katikati ya safari, akaja mhudumu akimuuliza, amletee chakula gani,
Mtu yule akakataa kuagiza, akijua kuwa anatakiwa kujilipia gharama ya chakula na hakuwa na hela.
Mtu yule alishinda na njaa safari yote, na alipofika mwisho wa safari, akapokelewa na mwenyeji wake.
Mtu yule akaomba apewe chakula na maji kwa sababu hakuwa amekula safari yote.
Ndipo mwenyeji wake akamuuliza, kwa nini hakula, akasema hakuwa na hela ya kununua chakula.
Ndipo mwenyeji wake akamsikitikia sana, na kumwambia, kula kitu kilikua kimeshalipiwa kwenye ticketi yako.
Ulichotakiwa kufanya ni kuagiza uwezavyo!!

Yule mtu kuingalia ile ticketi yake vizuri, kweli akakuta ina na kuponi ya chakula ndani!!!

oooh maskini mtu yule!!!

Ndivyo ilivyo na kwako!
Ukiamua kumpokea Yesu unapata si tu tikcet ya kwenda mbinguni bali pamoja na "lunchbox" ya kula njiani unapoelekea mbinguni!
Lunch box yako ina kila chakula unachotaka,
ukitaka uponyaji, utajiri, amani, furaha, ujasiri, upendo, kilaaa aina ya menu unayotaka ipo!!
Ni wewe tu kutambua kuwa ticket yako imelipiwa si tu nauli bali na gharama za chakula cha njiani!!
Wakristu wengi wanasafiri njiani wakiwa na njaa wakijua tu wao ticketi yao ni a kwenda mbinguni tu, haijalipiwa gharama ya chakula, hivyo wanaishi maisha ya kung'ang'ana sana wakijaribu kujilipia wenyewe gharama ya lunch!!!

Sikiliza,
IMESHALIPWA NDANI YA TICKETI YAKOOO! WEWE AGIZA TU!

Usikae na njaa wakati ticket yako inakuruhusu kula njiani.
#KwaYesuKunaVyote
#TumiaTicketiYakoVizuri
#Minna2017
#DarasaLaHekima

Tuesday, January 17, 2017

MARKO SURA YA 4


 Mfano wa mpanzi unatufundisha mengi;

1.Mpanzi ni Mungu
2.Mbegu ni Neno
3.Udongo ni moyo wako.

Katika upandaji tunaona kuwa mbegu zilianguka tofauti.

1. Kando ya njia.
-Ndege wakazila (shetani huliondoa moyoni lile Neno)

2. Kwenye Mwamba
-udongo mchache (hudumu moyoni kwa muda mchache,kwa sababu hamna mizizi)
-Jua likaja zikakauka.
(Dhiki na uzia kwa ajili ya lile neno likakauka)

3. Penye Miiba.
-Ikamea, ikalisonga, isizae.
(Miiba ni shughuli na dunia,mali na tamaa ya mambo mengine)

4. Penye Udongo mzuri.
Zikazaa 30,60,100!
(Zikazaa matunda,zikamea na kukua)

Udongo mzuri huandaliwa..ili mbegu inapokuja iweze kuzaa matunda.

#Andaa moyo wako ili Neno linapokuja liweze kumea,kukua na kuzaa matunda moja 30,60,100!
Uwe na siku njema
~Mwl Minna 

#DarasaLaHekima

Sio KILA KITU MUNGU ANACHOFANYA KWAKO AU ANACHOKWAMBIA UNAPASWA KUKISEMA KWA WATU!

VINGINE UNAPASWA KUNYAMAZA KIMYA,
VITU VINGINE UNAPASWA KUWAAMBIA AINA FULANI TU YA WATU ,

VITU VINGINE UNAWEZA KUMWAMBIA KILA MTU,

NA VINGINE HUSEMWA BAADA YA MUDA FULANI.

Mara nyingi YESU alipokuwa amemponya mtu, au kumtoa pepo aliwaonya watu hawa wasiseme baadhi ya vitu alivyokua anafanya,

lakini pia kuna mambo aliyokua anafanya na alikua anawaambia wakaseme, au kwa makuhani, au kwa mafarisayo au wakawaeleze watu kila Mungu alichowafanyia.

Na vingine alivyowaambia wanafunzi wake, aliwaambia wasiseme mpaka baada ya muda fulani.
#Minna2017
#DarasaLaHekima

USIPOJUA..

 Usipojua unachotaka chochote kijacho mbele yako utaenda nacho..

 Usipojua unataka kuwa nani,utasoma kozi yoyote itakayokuwepo mradi wengi ndio wanaisoma.. 

Usipojua unataka kuwa na familia ya aina gani,utaoa/kuolewa na yeyote ajae.. 

Usipojua unafaa kufanya biashara gani utafanya yoyote mradi umeambiwa inalipa.. 

Usipojua kuna maisha baada ya haya,utaishi tu kiholela bila YESU!..

 #KujuaNiKuamua
#AmuaLeoKujuaKusudiLako
#IshiMaishaYaKusudi
#DarasaLaHekima

Tuesday, January 10, 2017

#ToaMrejeshoChanyaKwaUPENDOwaYesu


UPENDO wa kweli unaonekana pale unapokua tayari kujitoa kwa ajili ya yule unayesema/unayedhani unampenda hata kama yeye haonekani kutoa mrejesho chanya kutokana na ule upendo wako!

Yesu ni mfano mzuri sana wa UPENDO huu!



Wakati mimi na wewe hatukua na habari kuwa kuna mtu alishatupenda zamani sana, halafu kuonyesha upendo wake akauweka kwenye vitendo, ilhali sisi hatukua na muda nae,

Alifanya hayo akijua kuwa siku moja atakuja kupata mrejesho chanya kutoka kwetu.

Unapoamua kumpa Yesu maisha yako,unakua umepokea ule UPENDO wake na kumpa mrejesho chanya.

Ukishaupekea ule UPENDO, Yesu anakutarajia kuusambaza kwa wengine kwa maneno na matendo, ili wajue kuwa nao WANAPENDWA NA YESU, ili nao wapeleke mrejesho chanya wa kuupokea huu UPENDO wake.

Kama bado hujaamua kupeleka mrejesho chanya kwake, kwa UPENDO wake kwako, fanya maamuzi mapema leo,
Ni uamuzi ambao huwezi kuujutia, ni uamuzi wa UPENDO!( Its a love decision)

#ToaMrejeshoChanyaKwaUPENDOwaYesu
#AnakusubiriWeweUfanyeMaamuzi

~Mwl Minna.

Wednesday, December 21, 2016

USICHOKE KUTENDA MEMA!

Hapa kwenye hii picha unaona nini?


Najua wengi mtaona hicho kialama cheusi!!

Lakini hiyo ni karatasi nyeupe yenye alama ndogo nyeusi!!


Ndivyo ilivyo hata kwenye maisha yetu ya kila siku!

Unaweza kutenda mema mengi sanaaaa(lile eneo kubwa jeupe) lakini siku ukitenda kosa moja tuuuuu( ile alama nyeusi ndogo) utashangaa lile kosa dogo ndilo litaonekana kwa haraka zaidi kuliko yale mema mengi uliyotenda!

Hata hivyo usichoke kutenda mema kwa sababu iko siku ile alama nyeusi itafutika kabisa na weupe utabaki kuwa mwingi zaidi, ndipo itaonekama karatasi yote ni nyeupe!

2Thesalonike 3:13 "Lakini nyinyi ndugu, msichoke kutenda mema."


Friday, December 16, 2016

Happiness is a choice!


Ukifika levo ya kufanya furaha kuwa kitu unachochagua kuwa nacho basi,umekomaa!

Lakini Kama furaha yako unaipata kwenye vitu,matukio,watu mazingira ulionayo kwa wakati fulani,pesa,kazi au chochote kilicho nje uwe na uhakika ni ya muda...na hivyo visababishi vikitoweka basi furaha nayo hutoweka.!
Njia pekee ya kuwa na furaha wakati wote ni kufanya MAAMUZI ya lazima kuwa ije mvua au liwake jua utakua na furaha.

Ukiona unakazana kutetea hali unayopitia ujue bado unataka kuendelea kuwa nayo!

Usipochoshwa na hali unayopitia huwezi kuhama hapo!
Ni mpaka hali uliyonayo uichoke ndipo utaanza kuona namna ya kutoka hapo.

Unajuaje Kama hali uliyonayo hujaichoka bado?
Wewe ni mtu wa kusema;
-Ndio maisha yalivyo...
-Ndio hali Halisi..
-Tunasogeza siku tu..
-Aha wengi walijaribu kutoka hapa lakini hawakuweza Mimi ntawezea wapi..
Na maneno yanayofanana na hayo,
#Ukiona unakazana kuitetea ujue Bado unataka kuendelea kuwa nayo!

~Mwl Minna

Hazina kubwa imefichwa kwenye maandishi!

Utajiri mwingi umefichwa kwenye maandishi!
Siri kubwa ziko kwenye maandishi!
Hekima nyingi imefichwa kwenye maandishi!
Sasa wale wavivu wa kusoma, wanaotaka kuangalia picha,
imekula kwao!

Hata viungo muhimu vya mwili vimefichwa!!
moyo umefichwa ndani, ubongo umefichwa ndani!!
Utaniambia Minna Matee Mboya, hata miguu na mikono ni muhimu, ndio sijakataa,kila kiungo kina umuhimu wake lakini levo ya umuhimu unatofautiana!!
Unaweza kuishi hata kama huna mikono, lakini huwezi kuishi kama huna moyo.
Unaweza kuishi hata kama huna miguu, lakini huwezi kuishi kama huna ubongo!!
#Hazina kubwa imefichwa kwenye maandishi!

Monday, December 12, 2016

WORDS OF WISDOM

"When people look at you they see a woman/man with your past,
When GOD looks at you He sees your Purpose!"

WORDS OF WISDOM

"Where people put a full stop,God begins a new sentence!"

WORDS OF WISDOM!

When people look at you they see a woman/man with a problem,
When GOD looks at you He sees a woman/man with potential!

WORDS OF WISDOM!

Your words create your World!
Watch what you say to yourself.


Thursday, December 8, 2016

NI NINI SIRI YA MAFANIKIO?

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristu,

Kila mtu anashauku ndani yake ya kufanikiwa na kufikia hatua au kiwango fulani cha maisha.

Kufanikiwa ni nini?

Kufanikiwa ni neno pana sana, tofauti na wengi wanavyodhani.


Tunapoongelea kufanikiwa hatusemi tu kufanikiwa katika yanayoonekana kama kuwa na nyumba, gari, pesa n.k, tunaongelea kufanikiwa kama package iliyokamili katika maeneo yote, yaani kimwili, kiakili, kiafya, kielimu, kiroho n.k. 

Tunapoongelea mafanikio tunongelea kutimiza kile ambacho unapaswa kukifanya, au lile kusudi la kuwepo kwako hapa duniani.
Unapoweza kulitimiza, basi wewe umefanikiwa!
Hivyo basi leo tuangalie watu wawili ambao wako katika maisha yao walifanikiwa sana na katika maeneo mengi sana,

Wa kwanza ni Mfalme Daudi.
Mfalme huyu alikua mfalme aliyemcha Mungu, na kuwa na ukaribu na Mungu hata kufikia hatua ya Mungu kumwita mtu aliyeupendeza moyo wake(Mungu).

Mfalme huyu tunajua kuna maeneo ambayo alimkosea Mungu lakini bado alibaki kuwa kipenzi cha Mungu.

Mwanzo kabisa wa kitabu cha Zaburi ambacho kimeandikwa na Daudi tunaona kuwa ameanisha wazi siri kuu ya mafanikio yake.
Nayo ni kutafakari Neno la Mungu katika Zaburi 1:1-3.

Daudi alikua mtu ambae alitafakari sana Neno la Mungu na ndio maana katika maeneo mengi ya Zaburi utaona ameandika uzuri wa kulitafakari Neno.

Daudi anasema kuwa mtu anayelitafakari Neno la Mungu mchana na usiku, hakika, kila alifanyalo litafanikiwa!

Wa pili ni Yoshua.
Yoshua alipewa kuwaongoza wana wa Israel kuingia Kanaani baada ya Musa aliyekuwa kiongozi mkuu kufa.
Mungu hapa tunaona akimpa Yoshua maelekezo au Siri ya yeye kuweza kutimiza ile kazi aliyopewa.
Kitabu hca Yoshua 1:8 tunaona Mungu alimwambia Yoshua kuwa Kitabu cha Torati kisiondoke kinywni mwake, yaani akitafakari mchana na usiku,ndipo atakapostawi sana na kufanikiwa sana.

Hivyo basi kutoka kwa hwa watu wawili tunaweza kuona kuwa mafanikio yamefungwa kwenye siri hii kubwa nayo ni KUTAFAKATI Neno la Mungu.

Anza leo kuwa na ushirika na Neno la Mungu na kulitafakari uone namna ambavyo litaleta mabadiliko maishani mwako.
Mimi ni shuhuda nambri moja wa namna Neno la Mungu limenibadilisha, na ni kwa njia ya kulitafakari.Mafanikio yangu yote ni kwa sababu nimejizoeza kulitafakari Neno la Mungu.

KWA NINI KUTAFAKARI?
Kwa sababu ndilo pekee lina uwezo wa kuleta badiliko.
taarifa nyingine zinahabarisha tu, ila Neno la Mungu lilabadilisha!

Izoeze akili yako kuliwaza Neno, yazoeze macho yako kuangalia Neno na ndipo na matendo yako yataenda Neno!

Mungu akubariki sana!

Friday, September 9, 2016

JINSI YA KUONA CHANGAMOTO UNAZOPITIA KAMA FURSA NA SIO KIKWAZO-Sehemu ya 1

Yapo majira mbalimbali katika mzunguko wa dunia ,hali kadhalika maisha yana majira na nyakati mbalimbali.



Si kila siku itakua kiangazi, au kila siku itakua masika, au kila siku itakua vuli au kipupwe!
Majira ni lazima yawepo na yapo ili kutupa mazuri zaidi na mema zaidi kila siku.

Kinapokua kipindi cha masika huwa ni kipindi cha mvua nyingi, na hata mfumo wa maisha hubadilika.

Huwezi kukuta mtu amevaa fulana nyepesi wakati wa mvua kwa sababu anahitaji nguo nzito inayousitiri mwili wake dhidi ya hali ya hewa ya wakati huo.

Lakini pia huwezi kukuta mtu amevaa koti kubwa wakati wa kiangazi, vinginevyo atakua na matatizo ya kiafya. Lazima atavaa nguo nyepesi inayopitisha hewa kwa sababu kipindi cha kiangazi ni kipindi cha jua kali na joto jingi.

Kwa mmoja majira fulani yanaweza kuwa changamoto ila kwa mwingine yakawa fursa.

Kwa mfano, kipindi cha kiangazi ni fursa kubwa sana kwa mfanya biashara anayeuza barafu kwa sababu ni wakati ambao barafu huhitajika sana.

Lakini kipindi hiki ni changamoto kwa muuza myavuli, kwa sababu kwake hatauza sana kwa sababu sio msimu wake.
Kadhalika majira yanapobadilika na kuwa masika, muuza barafu kwake ni changamoto kupata wateja, lakini kwa muuza myavuli ni fursa kwake kwa sababu yeye ndio atakua anahitajika zaidi kwa kipindi hiki.

Vivyo hivyo katika maisha ya kila siku kuna majira mbalimbali(Mhubiri 3:1).
Kuna wakati wa kuwa na vingi na kuwa na vichache. Kuna wakati wa kupita kwenye hali ngumu na wakati wa kupita kwenye utele.

Sasa basi, unawezaje kufanya majira yote yakawa fursa kwako na sio tatizo, na ukayafurhia yote yanapokuja kwako?

...Ungana nami kesho hapa hapa tuendelee

~Minna
*Furahia maisha kila siku*

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...