Kila mtu anashauku ndani yake ya kufanikiwa na kufikia hatua au kiwango fulani cha maisha.
Kufanikiwa ni nini?
Kufanikiwa ni neno pana sana, tofauti na wengi wanavyodhani.
Tunapoongelea kufanikiwa hatusemi tu kufanikiwa katika yanayoonekana kama kuwa na nyumba, gari, pesa n.k, tunaongelea kufanikiwa kama package iliyokamili katika maeneo yote, yaani kimwili, kiakili, kiafya, kielimu, kiroho n.k.
Tunapoongelea mafanikio tunongelea kutimiza kile ambacho unapaswa kukifanya, au lile kusudi la kuwepo kwako hapa duniani.
Unapoweza kulitimiza, basi wewe umefanikiwa!
Hivyo basi leo tuangalie watu wawili ambao wako katika maisha yao walifanikiwa sana na katika maeneo mengi sana,
Wa kwanza ni Mfalme Daudi.
Mfalme huyu alikua mfalme aliyemcha Mungu, na kuwa na ukaribu na Mungu hata kufikia hatua ya Mungu kumwita mtu aliyeupendeza moyo wake(Mungu).
Mfalme huyu tunajua kuna maeneo ambayo alimkosea Mungu lakini bado alibaki kuwa kipenzi cha Mungu.
Mwanzo kabisa wa kitabu cha Zaburi ambacho kimeandikwa na Daudi tunaona kuwa ameanisha wazi siri kuu ya mafanikio yake.
Nayo ni kutafakari Neno la Mungu katika Zaburi 1:1-3.
Daudi alikua mtu ambae alitafakari sana Neno la Mungu na ndio maana katika maeneo mengi ya Zaburi utaona ameandika uzuri wa kulitafakari Neno.
Daudi anasema kuwa mtu anayelitafakari Neno la Mungu mchana na usiku, hakika, kila alifanyalo litafanikiwa!
Wa pili ni Yoshua.
Yoshua alipewa kuwaongoza wana wa Israel kuingia Kanaani baada ya Musa aliyekuwa kiongozi mkuu kufa.
Mungu hapa tunaona akimpa Yoshua maelekezo au Siri ya yeye kuweza kutimiza ile kazi aliyopewa.
Kitabu hca Yoshua 1:8 tunaona Mungu alimwambia Yoshua kuwa Kitabu cha Torati kisiondoke kinywni mwake, yaani akitafakari mchana na usiku,ndipo atakapostawi sana na kufanikiwa sana.
Hivyo basi kutoka kwa hwa watu wawili tunaweza kuona kuwa mafanikio yamefungwa kwenye siri hii kubwa nayo ni KUTAFAKATI Neno la Mungu.
Anza leo kuwa na ushirika na Neno la Mungu na kulitafakari uone namna ambavyo litaleta mabadiliko maishani mwako.
Mimi ni shuhuda nambri moja wa namna Neno la Mungu limenibadilisha, na ni kwa njia ya kulitafakari.Mafanikio yangu yote ni kwa sababu nimejizoeza kulitafakari Neno la Mungu.
KWA NINI KUTAFAKARI?
Kwa sababu ndilo pekee lina uwezo wa kuleta badiliko.
taarifa nyingine zinahabarisha tu, ila Neno la Mungu lilabadilisha!
Izoeze akili yako kuliwaza Neno, yazoeze macho yako kuangalia Neno na ndipo na matendo yako yataenda Neno!
Mungu akubariki sana!
No comments:
Post a Comment