Upanga ni upanga uwe mKali au mButu.
Lakini tofauti kati yake itaonekana wakati wa matumizi.
Upanga ulionoelewa ni mkali na unapotumika huleta maangamizi makubwa kwa wakati mmoja.
Upanga butu, hutumika pia ila madhara yake ni madogo, na huenda mtumiaji akatumia nguvu kubwa sana wakati wa kuutumia!
Maombi ni kama upanga,
Maombi yenye maarifa sahihi ya Neno la Mungu, ni kama upanga ulionolewa!
Maombi yasiyo na maarifa sahihi ya Neno la Mungu ni kama upanga butu!
#Unaweza kunoa upanga wako kila siku kwa kuhakikisha unajifunza kila siku kitu kipya kuhusu Mungu.
#Upanga wako unavyozidi kuwa mkali, ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kuutumia!
#Efeso6:17
No comments:
Post a Comment