Saturday, March 9, 2024

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema!
kwa sababu hukijui.

Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hatima ya watu wanaokufa wanapoenda! ukilinganisha pia kwamba kulikuwa na malumbano kati yao.



Ndio anawaambia kwamba, wanapotea kwa sababu HAWAJUI MAANDIKO!

Mtu yeyote asiyejua maandiko lazima apotee na uongo wa adui,

Shetani lazima amjaze uongo wake, na ataamini, kwa vile tu hajui maandiko.

KWA NINI UJUE MAANDIKO?
1. Ujue haki zako mbele za Mungu
2. Ujue majira na mopangi wa Mungu kwako kupitia Neno lake.
3. Ujue adui na njama zake- Neno la Mungu pekee ndio lina elezea kwa usahihi hila za adui, na si vinginevyo. usipojua ni rahisi sana kuangukia kwenye mafundisho potofu ya mashetani kama Neno la Mungu linavyosema.

AMUA leo kusoma na kujifunza Neno la Mungu ili kulijua, ili USIPOTEE!

#umebarikiwa!

Saturday, October 28, 2023

HAIJALISHI UNACHOFANYA...


Ni kweli uliowazi kwamba hakuna jambo jipya chini ya jua!



Lakini pia pamoja na kwamba hakuna jambo jipya ila utofauti upo kwenye nani analifanya jambo hilo na anaona nini kwenye hilo analolifanya!


...Wote mnaweza kuwa mnafanya biashara moja ya chakula kwa mfano, lakini kitakacho wa tofautisha ni mnaona nini kwenye hiyo biashara.


Kiwango cha kuona kwao wewe ndicho kitakachokutofautisha kwenye hicho unachokifanya!


Isikupe shida wote mnauza nguo, au wote mna toa huduma zinazofanana, kinachojalisha ni utofauti wa uonaji wenu!


...Unaona nini kwenye kile unacho kufanya?


Anza kuona kwa mtazamo wa tofauti kwenye kile unachokifanya na utaanza kuona mabadiliko makubwa!


Kile unachokiona ndicho kitaamua umbali utakaofika kwenye hicho unachofanya/biashara/kazi unayofanya!


Unaweza kuwa unafanya jambo la kawaida sana, lakini je unaliona likifika wapi?


Wewe ni fundi cherehani labda, umeshawahi kujiona ukimshonea raisi nguo?


…Au wewe ni mpishi wa chakula, ulishawahi kuona ukipika kwenye hafla kubwa za kimataifa? Au unajiona tu hapo hapo kibarazani/ kimgahawani?


Wewe ni dereva, ulishawahi kuona ukimwendesha raisi? Au unajiona ukibaki hapo hapo kuendesha abiria kutoka kariakoo kwenda mbagala? 


….Sio kazi mbaya lakini unachokiona ndicho kitategemea mwendo wako na bidii yako kwenye hicho unachokifanya!


Siku zote utofauti wa kile unachofanya wewe na anachofanya mwenzako hata kama vinafanana ni unachoona kwenye unachofanya!


Mwendo wako na bidii ya kufanya inategemea sana unaona nini!


…haijalishi unachokifanya, inajalisha unaona nini kwenye kile unachokifanya! 


Kupata jumbe kama hizi kwa whatsapp tuma neno JUMBE kwenda 0679300845


#Kuza kuona kwako, na unachokifanya kitafika mbali!


MAMBO YA KUANGALIA UNAPOAMUA KUWA RAFIKI WA MTU!

Kiwango cha maisha yako kinategemea sana aina ya marafiki kama ambavyo tumesema kwenye post zilizopita.


Kama hujazipitia, anza post za nyuma kupata mtiririko mzuri..



1/VIPAUMBELE VYA MAISHA.

Kuna marafiki wana influence kwako zaidi kuliko wewe ulivyo na influence kwao. Na hiyo inaathiri pia vipaumbele vyako.

Kama ni rafiki mzuri walau atakua na vipaumbele vizuri, lakini kama ni rafiki mbaya na vipamumbele vyake pia vitakua sio sahihi, na kukupelekea kupotea.

Mf. Kama wewe ni mwanafunzi, na una rafiki anayeku-influence kuwa na mahusiano kabla ya wakati ni wazi kwamba kipaumbele chako kitakua mahusiano na sio elimu, hiyo itakupelekea wewe kupoteza dira(focus) yako kielimu.


2/ KIWANGO CHA MALENGO

Aina ya rafiki anaamua kiwango cha ukubwa wa malengo utakachokuwa nacho maishani. Ukiwa na marafiki wenye malengo madogo madogo ya kawaida, utakua na malengo ya kawaida kawaida na wewe, ukiwa na marafiki wenye malengo makubwa na wewe utakuwa na malengo makubwa vivyo hivyo.

Huwezi kuwa na marafiki ambao hawana malengo ya kujenga na kununua mashamba na ukakaa nao muda mrefu, ukadhani na wewe utakuwa tofauti na wao. Nawe utakuwa na mtazamo huo huo.

Chagua marafiki wenye malengo na maono makubwa utafika mbali.


3/ KUAMBUKIZWA TABIA

Hakuna namna utaambatana na mtu mlevi muda mrefu, na wewe usiwe mlevi. Iwe ni rafiki mwongo, lazima utaambukizwa uongo. Akiwa rafiki yako anadanga, ipo siku na wewe utashawishika kudanga. Kuwa na marafiki wenye tabia zenye tija ambazo zinakupekekea wewe kuwa mtu bora zaidi kuliko kuwa na rafiki ambaye anakuepelekea wewe kuwa mtu asiye na tija!

Tabia zako ndizo zinakutengeneza kuwa mtu wa aina fulani kesho!

Fanya tathmini ya marafiki ulionao. Unafaa kuendelea kuwa nao au la!


4/ MATUMIZI YA FEDHA.

Marafiki wanachangia sana matumizi yako ya fedha na wapi hasa unapeleka fedha yako.

Ukiwa na marafiki wanaotumia fedha nyingi kwenye starehe, ujue na wewe utakuwa mtu wa kutumia fedha nyingi kwenye starehe.

Hakuna namna wewe binti ukaambatana na mtu anayependa kufanya shopping ya nguo kila wiki, na wewe ukasema unanunua nguo mara mbili kwa mwaka. Ipo siku mko wote dukani hujapanga kununua nguo tamaa itakuingia na utajikuta umenunua na wewe, na haikuwa kwenye majeti yako.


Chagua marafiki vizuri kwa sababu wanaamua namna mambo haya manne kwenye maisha yako yatakavyokuwa.



Kupata jumbe kama hizi kwa whatsapp tuma neno JUMBE kwenda 0679300845


#KuwaRafikiwaFaida


~Firmina Victor

(Author,Youth Mentor)

KWA NINI UCHAGUE MARAFIKI?

 

...inaendelea kutoka kwenye post iliyopita..


...Marafiki zako wanaathiri sana aina ya maisha unayoishi sasa na ya badae.



Aina ya marafiki unaochagua kuwa nao ndio aina ya maisha unayochagua kuishi.


Kuna msemo unasema, "ukitaka kujua tabia ya mtu angalia aina ya marafiki zake."


Maisha yako ni mjumuiko wa marafiki watano unaokaa nao muda mwingi.


Mambo makubwa mawili ambayo huathiri maisha ya mtu.

1. Aina ya marafiki alionao.

2. Aina ya taarifa anazopokea 


Mambo haya ndio hupelekea mjumuiko wa maamuzi unayofanya kila siku ambayo huamua aina ya maisha yako kwa ujumla.


Rafiki yako anaweza kukupeka kwenye hatma yako nzuri,au anaweza kukuharibia hatma yako.


Watu wengi wamecheleweshwa kwenye maisha kwa sababu ya aina ya marafiki wanaokuwa nao.


...Kuna watu wamekosa nafasi na fursa kwa sababu ya marafiki wanaowazunguka.


Lakini pia wapo watu waliofikia hatma haraka sana kwa sababu walikuwa na marafiki sahihi..


Wapo ambao pia wamepata fursa na nafasi fulani kwa sababu ya rafiki yake!


Marafiki ulionao, wanachangia maisha yako kuendelea Au ndio wanakudidimiza kila siku.


Rafiki wa faida atakutoa kwenye madeni sio kukuingiza kwenye madeni!


Rafiki wa faida atakuepusha na hatari ijayo, na sio kukuelekeza panapohatarisha maisha yako hata kama ni kwa starehe ya muda mfupi.


Chagua marafiki vizuri, wanachangia sana  kuwa ulivyo.


Je,Wewe ni rafiki wa faida?



Firmina Victor

+255 BHVG679300845(Whatsapp)

UTAMJUAJE RAFIKI MZURI WA FAIDA?


Bila shaka umewahi na hata sasa unao marafiki wengi.


...Lakini ili kuwa mtu mwenye matokeo, uchaguzi wa aina ya marafiki ni jambo la msingi sana.



Si kila unayeongea nae anapaswa kuwa rafiki yako. Kuongea na mtu haimaanishi ni marafiki.


Na si kila rafiki atakusaidia kuwa mtu bora mwingine atakupeleka shimoni.


📌Marafiki ni miongoni mwa aina ya mahusiano yanayoathiri sana maisha ya mtu kwa ujumla ikiwemo maamuzi yake ya kila siku.



👉🏼Hizi ni ishara chache zitakazokupekekea kujua huyo rafiki yako ni wa faida au la:


1️⃣ Atakuelekeza na kukusisitiza kumpenda Mungu na kuishi maisha ya

kumpendeza Mungu.


Ukiona uko na rafiki ambaye hata hakusaidii kumwogopa Mungu, ujue muendako si salama.


2️⃣ Atakuelekeza na kukusisitiza kujikita kwenye mambo ya maendeleo zaidi.

Rafiki ya 'kula bata' huyo si rafiki wa faida,bali wa hasara.

 Ila atakayekuelekeza kufanya mambo ya maendeleo huyo mshikilie.


3️⃣ Ukikosea atakwambia kwa upendo, na hatanyamaza kwa kuogopa

kugombana na wewe au kuonekana mbaya. Atasema kweli siku zote.

Mpende rafiki anayekwsmbia ukweli na asiye mnafiki! Huyo msikilize.


Ila rafiki ambaye yeye kila siku anakusifia hata ukikosea na qewe ukajua umekosea yeye anakwambia ni sawa,mwogope! Ataona unaenda kifoni na atakwanbia nenda tu! Mkimbie huyo.


4️⃣ Atakuombea ufanikiwe.

Kila wakati atakuwazia mema na kukuombea mafanikio. Hata ukipata hasara atakusaidia namna ya kuinuka tena.


5️⃣ Hatakusema vibaya kwa watu wengine, bali atakuuliza moja kwa moja

jambo lolote atakalolisikia.


Akisikia jambo atakuface na kukuuliza na sio kukusema pembeni. Hatakuteta kitu ambacjo hatakua na ujasiri wa kukisema mbele yako. 


👉🏼Jifunze kuchagua marafiki na watu unaotumia muda mwingi nao kila isku

kwani wanachangia sana kuendelea kwako mbele,kukwama ulipo au kurudi nyuma kwako.


Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote(Mith17:17)

Kupokea jumbe kama hizi kwa njia ya watsap kila mara tuma neno JUMBE kwenda +255679300845.


Chagua rafiki wa faida!

UMETENGENEZWA KWA KAZI MAHUSUSI NA MAALUMU!


 Unapoenda kwa fundi kushona nguo, huwa anakupima vipimo atakavyotumia kwa ajili ya kukushonea nguo itakayokufaa kulingana na umbile lako la mwili. 


Nguo ile inakua ‘custom-made’ mahususi kwa ajili yako tu!


Na mtu mwingine hawezi kuivaa ikafanana kama ambavyo wewe itakukaa.


Hali kadhalika kila mwanadamu ametengenenzwa na Mungu muumbaji kwa ajili ya kazi mahususi na maalumu, ambayo yeye tu ndio anaweza kuifanya ipasavyo na kuikamilisha.


Unapaswa kujua kazi uliyoitiwa kuifanya hapa duniani. Na kisha kuifanya na kutokuacha.


Ukijua kwamba umetengenezwa mahususi kwa ajili ya kazi hiyo, hupaswi kukata tamaa kamwe kwenye kazi hiyo.(Efeso 2:10)


Hata kama changamoto zitakuja utaendelea kwa sababu utajua hii ndio sababu ya mimi kuwepo juu ya uso wa nchi.


Hata wewe chombo kisichokufaa jikoni kwako huwa kinatupwa au kuwekwa stoo,na kile vinachokufaa huwa unakitumia kila wakati,kukiosha na kukitunza kikufae tena na tena.


Hali kadhalika, unapoendelea kuwa wa kufaa na wa faida Mungu ataendelea kukutunza na kuhakikisha unakuwa bora zaidi ili akutumie zaidi!


Kupokea jumbe kama hizi kwa njia ya watsap kila mara tuma neno JUMBE kwenda +255679300845.

Kuwa bora zaidi!


USIKU UNAPOZIDI SANA UJUE ASUBUHI HUKARIBIA!

 

Haiwezi kuwa asubuhi kama usiku haijawa mnene!


Na usiku unapozidi kuwa mnene sanaaa! 

Ndio ishara ya asubuhi ya mapambazuko!



Haijalishi giza litatanda kiasi gani, ni LAZIMA kukuche!


Hiyo ni kanuni aliyoiweka Mungu tangu kuumbwa ulimwengu.


Hivyo mwanadamu hana wasiwasi kwamba kutakucha au la!


Kwa sababu ni kanuni ni lazima itachukua mkondo wake na kuleta matokeo.


Unapitia nini kinachoonekana kama giza zito na usiku mnene maishani mwako?


Huoni mbele kwa sababu ya giza zito?


Huelewi kesho itakwaje kwa sababu huoni nuru ikipambazuka?


Jambo moja usisahau uwapo hapo, asubuhi lazima itafika!



.... haina mashaka,na haijalishi hali ikoje,kuwe na jua kuwe na mvua,,asubuhi lazima itafika.



Inua macho uangalie mbele nawe utaanza kuona mwanagaza..


Usiangalie nyuma(yaliyopita), usiangalie usiku uliopita!


Angalia ASUBUHI IJAYO.

Ina nuru

Ina mwangaza


Inagalie hiyo na utaona njia ya kupita.


Mwanga huweka kila kitu wazi.

Mwanga huleta mwelekeo wa maisha.


Tazamia asubuhi yako maana haiko mbali.


Kumbuka: USIKU UNAPOZIDI SANA NDIPO ASUBUHI HUKARIBIA!


Inuka tena!


Kupokea jumbe kama hizi kwa njia ya watsap kila mara tuma neno JUMBE kwenda 0679300845

UMEWAHI KUONA NAMNA MCHWA WANAVOJENGA NYUMBA YAO ?

Ukiikuta imeisha unaweza kudhani ni mwanadamu ametengeneza...!




Lakini ukichunguza kwa makini utagundua hakuna mwanadamu wala kiumbe kingine chochote kimewasaidia bali ni bidii na juhudi yao wenyewe wakishirikiana kwa pamoja na kufanikisha ujenzi wa
jumba lao.

📍Siri kubwa hapo ni umoja, bidii na juhudi!

🪨Hakuna namna mafiga haya matatu yatakaa pamoja kisiive chakula kitamu!

Popote watu wanapoamua kufanya kitu kwa umoja kwa bidii na kwa juhudi lazima wapate matokeo.

Haijalishi kile wanachotaka kufanya ni kizuri au kibaya, lazima kitafanikiwa!

🛕Hapo zamani, watu wa Babeli walitaka kujenga mnara ili uwawezeshe wafike mbinguni!
Watu wale walikuwa na umoja kiasi cha kuongea lugha moja na kuwasaidia kuelewana wote.

Watu wale walikuwa na bidii sana katika kazi yao kwani waliifanya usiku na mchana.
Na watu wale walikua na juhudi sana katika kazi ile..

Na walifanikiwa kuanza kuujenga mnara ule, Ijapokuwa nia yao haikuwa njema.

Umoja huo ulivunjika baada ya lugha yao kuchanganywa na wao kushindwa kusikilizana!

Na ndipo lengo lao kushindwa kutimizwa.

Figa moja lilibomoka. Mafiga yale mawili hayakuweza kupika chakula(kutimiza lengo).

Mifano hii miwili ikawe chachu kwako kuwa na umoja, juhudi na bidii katika malengo yako ili kuyatimiza kwa kishindo!

Unaweza!
Firmina Victor
(Whatsapp +255679300845)

Sunday, April 11, 2021

HABARI YA RUTH



RUTH 1:

Tunaona kulikua na njaa katika Israel hivyo bwana mmoja aitwae Elimeleki na familia yake wakawa wanakimbia njaa..😩🏃🏃🏃👨👩👦👦
 
Wakaenda katika nchi ya Moab.umbali wa kama mile 30 au mwendo wa siku 7-10 kwa kutembea..🚶🚶🚶🚶 akiamini kupata chakula huko🍹🍞
 
Walikaa huko na Elimeleki akafa.
Wale wanae wawili wakaoa wanawake wa Moab..Opra na Ruthu.💃💃; wakaishi miaka 10 ya ndoa.
 
Baadae wale wana wa Naomi nao wakafa.💀
 
Akabaki  Naomi na wakweze.
 
Naomi akaamua kurudi KWAO Bethlehem maana alisikia Bwana ameutembelea mji kwa chakula(njaa imeisha)😋🌽🍇🍎.
Nacho kilikua kipindi cha mavuno.
 
 
FUNZO:
Elimeleki alikimbia mbali na Mungu(nchi ambapo Mungu aliwapa) kwa sababu ya njaa na badala ya kufanikiwa alikoenda aliishia kukutwa na mauti yeye na wanae..
Tunaona pia Abraham alikimbia njaa kufika Misri mkewe nusu wamuoe,Mungu akaingilia kati😳
Mwana mpotevu nae alikimbia nyumbani akidhan ataenda kufanikiwa zaidi huko mwishowe alirudi hom mikono mitupu🤔

 Uweponi mwa Mungu ni mahali salama hata kama tunaona mambo ni magumu,,tuchikilie tu Bwana atakukumbuka tuuu..huko Moab hakuna jema😟

KWA UPANDE WA MAMA MJANE-NAOMI.
 
Wakweze Naomi walikubali Kwenda nae Bethlehem,ila Naomi aliwasihi sana wabaki maana walikua bado wadogo hivyo walipaswa waolewe nao wawe na familia zao.
Mkwewe mmoja(Opra) akakubalkubaki🙋
Lakini mkwewe wa Pili(Ruthu) akakataa..akataka Kwenda na Naomi.
 
NAOMI
Alikua mwanamke aliyemjua Mungu wake,aliyeishi kwa Upendo na wakweze na kuwajali na kuwatendea mema.
maana waliishi nae zaidi ya miaka kumi,na bado walitaka kuendelea kuishi nae👍
Hata ulipofika wakati wa kuachana nae ikawa ngumu.
 
 
FUNZO:
Mwanamke anayemcha Mungu hutachoka kuishi nae.
Kwa kuwa Moyo wake wakati wote umejaa upendo na ukarimu.

Friday, January 22, 2021

JE,UTAKUBALI SHAMBA LAKO LIKAPANDWA MAGUGU KWA SABABU YA USINGIZI?

 


..lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

MT. 13:25 SUV



Usikubali shamba lako lipandwe magugu na adui kwa sababu ya usingizi.

Usingizi upo wa aina mbili

Wa kiroho na wa kimwili.


Wa kiroho ni pale ambapo unaacha kuwa rohoni yaan unaacha kuomba,kusoma neno,kutenda matendo mema,na kuliishi Neno la Mungu.


Hapo adui shetani kupitia mawakala wake anapata mlango wa kuingia kwenye himaya yako na kupanda magugu(uharibifu).

Yaan anapanda mbegu(wazo) ambalo huenda usijue kama ni gugu ukadhani ni ngano.


Na kwa vile umelala huwezi gundua.


Vyote vinakua na siku moja inagundulika haikuwa ngano lilikua gugu😱


Kila mtu anashangaa kulikoni huyu ndugu kafanya hivi au vile,

Kumbe ni gugu la muda mrefu lilipandwa bila mtu kujua kwa sababu alikua amelala.


Amka mpendaa tuwe macho rohoni kupitia maombi,kusoma neno kila siku,na kulitafakari ili kujilinda na adui anayesubiri tu tusinzie kidogo apandikize mbegu ya gugu ndani yetu.



Umebarikiwa!

Friday, January 15, 2021

OMBI LA LEO:MUNGU AMSHA ROHO ZA WATU WALIOKUSUDIWA KUSABABISHA KUTIMIA KWA NENO LAKO MAISHANI MWANGU MWAKA HUU 2021


 1.Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 


 5. Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.

EZR. 1:1‭, ‬5 SUV


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻

Omba Mungu aamshe roho za watu ambao wamekusudiwa kutumiwa nae kutimiza Neno lake maishani mwako



Ili kupenya maishani inahitajika watu Mungu aamshe roho zao watumike kukubariki,

Watumike kukuvusha mahali,

Watumike kukusemea mahali upate kibali,

Watu waamshwe roho zao watoe pesa zao,muda wao, mawazo yao kwako ili uvuke kwenda hatua nyingine ya maisha.


Ili kusudi la Mungu kwako 2021 litimie unahitaji watu.


*Na hao watu ni mpaka Mungu awe ameamsha roho zao kutenda kwako,* hawawezi kutenda tu hivi hivi.


Ombi letu leo,

Ee Mungu wangu amsha roho za watu waliokusudiwa kutenda kwangu ili Neno lako kwa mwaka huu 2021 litimie kwangu.


Hii ni kanuni mojawapo ya kiroho ya kusababisha mambo kutokea katika eneo/jambo lako lolote.

Omba Mungu aamshe roho za waliokusudiwa kukusaidia uvuke hapo ulipo.


Umebarikiwa!

UMESHAANDIKA MALENGO YAKO YA 2021?

Shalom Msomaji wangu.

Pokea salamu za mwaka mpya 2021!



Naamini kila mmoja wetu ameshaandika malengo yake ya 2021.

-kiroho

-kiuchumi

-kimaendeleo/uwekezaji

-kitaaluma/career

-kibiashara

-kiafya

-kihuduma


Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

Mithali 16:1 NEN


Wengi wanaishia kuwaza tu.

Ni vizuri *kuandika*


Na kuyaweka mahali ambapo utakua unayaona mara kwa mara.


_Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi: *“Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma.*_

Habakuki 2:2 BHN


Unaweza kuandika na kuyabandika mahali ambapo utakua unayaona kila siku.

Ili ukumbuke kutafanya isifike june ukawa umeshasahau na umeendelea na mambo mengine ambayo hayakuwa kwenye malengo yako.


Au kwenye diary ambayo unaitumia kila wakati ili ufunguapo uwe *unayaona*



*Kwa nini uandike?*

1.Itakua kufocus kwenye kile ulichopanga na hutatoka nje ya mstari.

2.utakumbuka na hutakua na kisingizio kwamba ulisahau.

3.ili uwe unajipongeza kila unapotimiza lengo mojawapo ya uliloandika.


Kuna watu hapa wanaandika malengo ya makampuni wanayofanyia kazi na mpango mkakati wa kuyatimiza lakini hajiandikii ye mwenyewe malengo yake ya mwaka na hana mpango mkakati binafsi.

Kama kampuni ingekua genius ingeandika kichwani isingeweka kwenye maandishi.😜

Ndio maana mwaka ukiisha ukimuuliza mtu ulifanya nini mwaka huu anakwambia hata sioni..zaidi ya kula tu asubui mchana jioni😃


Au akienda sana atakutajia kitu kimoja au viwili tu.

Kweli miez 12 umepewa na Mungu kufanya kitu kimoja au viwili tu! Si ni utumiaji mbaya wa muda huo?

Hayo yanatokea kwa sababu malengo hayaandikwi.

Na yakiandikwa notebook inawekwa kabatini kujaa vumbi.


Hayatengenezewi mkakati wa namna ya kufanyika,hivyo hayawez kutokea tu..lazima yasababishwe kutokea.


Mwaka 2021 TUAZIMIE KUWA NA MALENGO YA KUELEWEKA NA TUWE NA MPANGO MKAKATI WA KUYATIMIZA.


 Unaweza kutumia mchanganuo kama nlioweka mwanzo au ukaongezea vingine kulingana na wewe mwenyewe.


Hii ndio siri mojawapo ya waliofanikiwa!


Uwe na siku njema!

Thursday, June 11, 2020

MTIRIRIKO SAHIHI NI HUU.


SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 4


✍🏾Mungu husikia maombi na kutufanyia nafasi wakati wa shida.
Unapokua kwenye shida ina maana umebanwa mahali,ndio maana Daudi anamwomba Mungu amfanyie nafasi katika kipindi cha shida na Mungu anamsikia.
.
📌UKIWA NA SHIDA JAMBO LA KWANZA LIWE KUMWOMBA MUNGU NA SIO KUTAFUTA MSAADA KWA WANADAMU.
.
📌MARA NYINGI TUKIPATWA NA SHIDA TUNAWAZA NIMPIGIE NANI SIMU AU NIMWAMBIE NANI ANIKOPESHE🤔
.
📌Msaada wa Kwanza na wa Haraka ni Mungu.MUNGU YUKO NASI WAKATI WOTE MAHALI POPOTE.
.
YEYE ANAWEZA KUTATUA SHIDA AMBAZO HATA MWANADAMU HAWEZI.
.
NA BAADA YA KUMWOMBA NDIPO ATAKUONGOZA NANI WA KUMTAFUTA ALIYEBEBA MAJIBU YAKO,MAANA SI KILA MTU ANA JIBU LA SHIDA YAKO.

Mstari 8
Hii ni dozi nzuri sana kila siku kabla ya kulala
.
✍🏾 ikariri na uwe unaisema kama sehemu ya sala yako ya kulala na utaona jinsi utalala kwa Amani.
.
📌WATU WENGI IKIFIKA USIKU WANAOGOPA KULALA.
NA HASA KAMA ANALALA KWENYE NYUMBA PEKE YAKE.
.
LAKINI UKIZOEA KUOMBA HUU MSTARI WA NNE UTAGUNDUA KWAMBA;
.
📌MUNGU HUTUPA AMANI NA USINGIZI MAANA NDIYE ATUPAYE USALAMA.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 15 0ZA ZABURI - ZABURI 3


✍🏾 (Mstari1-3)Lazima ujue kuwa UNAO MAADUI(Watesi),na sio maadui tu,bali MAADUI WENGI.
Na wanajisemea "tumwone,anajidai na Mungu,tuone kama Mungu atamsaidia"
.
📌Lakini,lazima umjue Mungu wako.
YEYE ni NGAO yako pande zote.
YEYE ni UTUKUFU wako,
YEYE ni MWINUA KICHWA chako
.
📌thats all you NEED,,
.
👉🏻Uhakika wa ulinzi wa Mungu(NGAO) dhidi ya adui zako,
.
Uhakika wa Uwepo wa Mungu(UTUKUFU) kwako adui wanapokujia
.
Uhakika wa Ushindi(MWINUA KICHWA) dhidi ya adui.


Mstari 4
📌Maombi ni mawasiliano kati yako na Mungu.
Sio maongezi ya MTU MMOJA, ni ya WAWILI
.
👉🏻LAZIMA KUWE NA MREJESHO
.
📌UKIONA UNAOMBA TU WEWEEEE HALAFU HUSIKII JIBU,,IKO SHIDA MAHALI,JIFANYIE TATHMINI.
.
Mstari 6-8
📌USIOGOPE WINGI WA ADUI KWANI BWANA AMEKWISHA WAPIGA KIBAO CHA SHAVU NA KUWAVUNJA MENO😂
(Ndivyo Biblia inasema)
.
👉🏻Adui yako asikuogopeshe kwani tayari ni KIBOGOYO😂😂😂
.
Sijui kama unaelewa hii
.
👇🏽
.
Hivi KIBOGOYO anaweza kuongea kweli? Sasa Maneno ya adui yanakutisha nini wakati hayasikiki hata vizuri🤷🏻‍♀️
.
📌 USITISHWE NA MANENO YA ADUI YAKO
.
WEWE MTAZAMAE BWANA.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 2


✍🏾Mawazo yasiyopendeza juu ya Mungu na watumishi wake, Mungu hapendi
.
✍🏾Pale ambapo mtu au watu wanajipanga kuwa kinyume na mtumishi wa Mungu ni sawa na kuwa kinyume na Mungu mwenyewe
.
✍🏾Na mtu anapowaza uovu huo, mbinguni Mungu ANAMCHEKA na kumeangalia kwa DHARAU
.
📌 Ndipo hasira yake inapowaka juu ya mtu huyo
.
📌UNAJIULIZA,mbona hiki hakiendi au kile hakiendi,,
.
JICHUNGUZE,je,umewahi kumwazia mabaya mtumishi wa Mungu na Mungu mwenyewe? Basi hasira yake imewaka juu yako! TUBU LEO.
.
📌JIZOEZE kuwaombea wale wanaofanya kazi ya Mungu badala ya kuwasema vibaya, hata kama walichofanya ni kibaya, SIO KAZI YAKO wewe kuanza kuwasema vibaya.
.
📌ACHA MUNGU MWENYEWE atashughulika nao,
.
📌USIJITAFUTIE LAANA ZISIZO NA ULAZIMA NA ZINAZOEPUKIKA.


✍🏾mstari wa 8.
UNIOMBE, NAMI NITAKUPA MATAIFA KWA URITHI WAKO.NA MIISHO YA DUNIA KUWA MILKI YAKO.
.
📌MUNGU mwenyewe anatupa prayer point..
MUNGU anataka uone kwa mtazamo wa kidunia sio wa kimtaa unachoishi.
.
UNAPOOMBA, kuwa na Global Vision.
(Wanasema Think Global but Start Local) .
LAZIMA MTAZAMO WAKO UWE WA MATAIFA,UWE WA MIISHO YA DUNIA,,ILI maombi yako yawe pia ya aina hiyo..inaanzia kwenye mindset.
.
📌Je,UNA MAONO GANI?KUJUSU KAZI YAKO,BIASHARA YAKO,HUDUMA YAKO?
.
JE,YANAISHIA MTAANI KWAKO,MKOANI KWAKO,NCHINI KWAKO,AU DUNIANI KOTE?
.
👀 Macho yako yafunguke leo uone jinsi Mungu anavyokuona..yeye anakuona kama a GLOBAL PERSONALITY.
SO SHOULD YOUR PRAYERS BE.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 1

Heri(Amebarikiwa)mtu yule;
1.Asiyekwenda(asiyetembea) katika shauri (majadiliano/maamuzi) ya wasio haki.
2. Hakisimama katika njia ya wakosaji
3.Hakuketi barazani na wanaofanya mizaha.

📌Badala yake mtu huyu,
1.Anafurahishwa na Neno la Mungu.
2.Analitafakari wakati wote(usiku na mchana) .

👉🏻Matokeo yake:
1.Atakua kama mti ukiopandwa kando ya maji,na kuzaa matunda yake kwa wakati.
2.Jani lake halitanyauka.
3.KILA alitendalo litafanikiwa.

👉🏻SIRI YA KUFANIKIWA NA KUSTAWI KWENYE KILA ENEO MAISHANI IKO HAPA.

 👉🏻KWANZA,,KUTAFAKARI NENO LA MUNGU WAKATI WOTE.
SIO KUSOMA TU,BALI NA KUTAFAKARI.
KUNA TOFAUTI HAPO
 👉🏻PILI,KUIPENDA SHERIA YA BWANA..YAANI KULIPENDA NENO LA MUNGU.
Kuna watu wanasoma Neno kwa sababu tu wanalazimishwa,au na wazazi au kanisa lake au mazingira aliyopo.

👉🏻LAKINI SIRI MOJAWAPO YA KUFANIKIWA IPO KWENYE KULIPENDA NENO LA MUNGU.
YAANI ULIPENDE TU.
UPENDEZWE NALO.

UKILIPENDA INA MAANA,
📌UTATAKA KULISIKIA KILA SAA
📌HUTACHOKA KULISOMA
📌UTATAKA KULIJUA ZAIDI

Na hizi ndio siri kubwa za kufanikiwa kiMungu,maana Neno lina siri zote unahitaji kuweza kuishi hapa duniani kwa ushindi.

JIZOEZI KULIPENDA NA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU KILA SIKU.


#Umebarikiwa!
#siku150zazaburi

Sunday, June 7, 2020

JE WAJUA?

MAAMUZI YAKO YA JANA NDIO MATOKEO YAKO YA LEO, NA MAAMUZI YAKO YA LEO NDIO YATAKUWA MATOKEO YAKO YA KESHO.

AMUA VEMA LEO ILI UWE NA KESHO NZURI.

USIBAKI KULALAMIKA TU AU KULALAMIKIA WATU KWA SABABU WALIKUAMULIA MAMBO FULANI NA YAMELETA MADHARA KWENYE MAISHA YAKO

AMUA LEO KUFANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO YA KESHO.

USISUBIRI MTU AJE AKUAMULIE,
AU SERIKALI NDIO IKUSAIDIE KUAMUA KESHO UWEJE.

WEWE NDIO UNA UAMUZI WA UNATAKA KESHO YAKO IWEJE.

 

WEWE NDIO UNAAMUA KESHO UWE MTU WA AINA GANI
WEWE NDIO UNAAMUA KESHO UISHI WAPI
WEWE NDIO UNAAMUA,

NA USIPOAMUA WEWE UTAAMULIWA NA WATU WENGINE,

LAKINI LAZIMA MAAMUZI YAFANYIKE,NDIO MAMBO YATOKEE.



#DontBlamethepastbookreview
#bookreview
#author

LEAVING A LEGACY!

We are so used to see even receive a legacy from those who went ahead of us particularly of material things such as houses,cars,plots and education.

But this will only stay for few years and with few individuals.




 


Very few precious people think beyond that.
A legacy that will surely live eternally.
A legacy that generations after you will treasure.

I was just wondering if I leave a house and riches for my children and my children's children that will be so selfish!
Although it is so important to do so as the Bible instructs us to do so.


But we can do more than that.

We ought to leave a legacy of Glory!


You are Blessed!

JE,UNAJIONA DHAIFU NA MASIKINI?

IJAPOKUWA UNAJIONA DHAIFU NA MASIKINI, MUNGU ANAKUONA HODARI NA UNAYEWEZA KUISHINDA VITA.

Hata Gidioni,alikua kijana aliyejiona hivyo pale alipotokewa na malaika.
Waamuzi 6:1-6 inaeleza wasifu wa kijana huyu

Alijiona masikini
Alijioni mdhaifu sana
Alijiona haiwezi vita iliyokua mbele yake.

Lakini Mungu hakumwona kwa staili hiyo.

MUNGU ALIMWONA NI HODARI NA SHUJAA AWEZAE KUIPIGANA VITA NA KUISHIDA.

 


HATA WEWE LEO HII,
USIJIONE MDHAIFU,
USIJIONE MASIKINI,

JIONE KAMA MUNGU ANAVYOKUONA!

ANAKUONA HODARI,
ANAKUONA UNAWEZA,
ANAKUONA MSHINDI,

NA NDIVYO ULIVYO.

USIYUMBISHWE NA HALI ULIYONAYO SASA,

HATA WANAJESHI WAKIANGALIA IDADI YA ADUI HAWATAPIGANA VITA,

HIVYO UANGALIE UKUU WA MUNGU
NA UTAISHINDA VITA.

UWE NA MWEZI WENYE USHINDI TELE!

#author
#kalamuyangu✍


MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...