Saturday, October 28, 2023

UMEWAHI KUONA NAMNA MCHWA WANAVOJENGA NYUMBA YAO ?

Ukiikuta imeisha unaweza kudhani ni mwanadamu ametengeneza...!




Lakini ukichunguza kwa makini utagundua hakuna mwanadamu wala kiumbe kingine chochote kimewasaidia bali ni bidii na juhudi yao wenyewe wakishirikiana kwa pamoja na kufanikisha ujenzi wa
jumba lao.

📍Siri kubwa hapo ni umoja, bidii na juhudi!

🪨Hakuna namna mafiga haya matatu yatakaa pamoja kisiive chakula kitamu!

Popote watu wanapoamua kufanya kitu kwa umoja kwa bidii na kwa juhudi lazima wapate matokeo.

Haijalishi kile wanachotaka kufanya ni kizuri au kibaya, lazima kitafanikiwa!

🛕Hapo zamani, watu wa Babeli walitaka kujenga mnara ili uwawezeshe wafike mbinguni!
Watu wale walikuwa na umoja kiasi cha kuongea lugha moja na kuwasaidia kuelewana wote.

Watu wale walikuwa na bidii sana katika kazi yao kwani waliifanya usiku na mchana.
Na watu wale walikua na juhudi sana katika kazi ile..

Na walifanikiwa kuanza kuujenga mnara ule, Ijapokuwa nia yao haikuwa njema.

Umoja huo ulivunjika baada ya lugha yao kuchanganywa na wao kushindwa kusikilizana!

Na ndipo lengo lao kushindwa kutimizwa.

Figa moja lilibomoka. Mafiga yale mawili hayakuweza kupika chakula(kutimiza lengo).

Mifano hii miwili ikawe chachu kwako kuwa na umoja, juhudi na bidii katika malengo yako ili kuyatimiza kwa kishindo!

Unaweza!
Firmina Victor
(Whatsapp +255679300845)

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...