Saturday, October 28, 2023

MAMBO YA KUANGALIA UNAPOAMUA KUWA RAFIKI WA MTU!

Kiwango cha maisha yako kinategemea sana aina ya marafiki kama ambavyo tumesema kwenye post zilizopita.


Kama hujazipitia, anza post za nyuma kupata mtiririko mzuri..



1/VIPAUMBELE VYA MAISHA.

Kuna marafiki wana influence kwako zaidi kuliko wewe ulivyo na influence kwao. Na hiyo inaathiri pia vipaumbele vyako.

Kama ni rafiki mzuri walau atakua na vipaumbele vizuri, lakini kama ni rafiki mbaya na vipamumbele vyake pia vitakua sio sahihi, na kukupelekea kupotea.

Mf. Kama wewe ni mwanafunzi, na una rafiki anayeku-influence kuwa na mahusiano kabla ya wakati ni wazi kwamba kipaumbele chako kitakua mahusiano na sio elimu, hiyo itakupelekea wewe kupoteza dira(focus) yako kielimu.


2/ KIWANGO CHA MALENGO

Aina ya rafiki anaamua kiwango cha ukubwa wa malengo utakachokuwa nacho maishani. Ukiwa na marafiki wenye malengo madogo madogo ya kawaida, utakua na malengo ya kawaida kawaida na wewe, ukiwa na marafiki wenye malengo makubwa na wewe utakuwa na malengo makubwa vivyo hivyo.

Huwezi kuwa na marafiki ambao hawana malengo ya kujenga na kununua mashamba na ukakaa nao muda mrefu, ukadhani na wewe utakuwa tofauti na wao. Nawe utakuwa na mtazamo huo huo.

Chagua marafiki wenye malengo na maono makubwa utafika mbali.


3/ KUAMBUKIZWA TABIA

Hakuna namna utaambatana na mtu mlevi muda mrefu, na wewe usiwe mlevi. Iwe ni rafiki mwongo, lazima utaambukizwa uongo. Akiwa rafiki yako anadanga, ipo siku na wewe utashawishika kudanga. Kuwa na marafiki wenye tabia zenye tija ambazo zinakupekekea wewe kuwa mtu bora zaidi kuliko kuwa na rafiki ambaye anakuepelekea wewe kuwa mtu asiye na tija!

Tabia zako ndizo zinakutengeneza kuwa mtu wa aina fulani kesho!

Fanya tathmini ya marafiki ulionao. Unafaa kuendelea kuwa nao au la!


4/ MATUMIZI YA FEDHA.

Marafiki wanachangia sana matumizi yako ya fedha na wapi hasa unapeleka fedha yako.

Ukiwa na marafiki wanaotumia fedha nyingi kwenye starehe, ujue na wewe utakuwa mtu wa kutumia fedha nyingi kwenye starehe.

Hakuna namna wewe binti ukaambatana na mtu anayependa kufanya shopping ya nguo kila wiki, na wewe ukasema unanunua nguo mara mbili kwa mwaka. Ipo siku mko wote dukani hujapanga kununua nguo tamaa itakuingia na utajikuta umenunua na wewe, na haikuwa kwenye majeti yako.


Chagua marafiki vizuri kwa sababu wanaamua namna mambo haya manne kwenye maisha yako yatakavyokuwa.



Kupata jumbe kama hizi kwa whatsapp tuma neno JUMBE kwenda 0679300845


#KuwaRafikiwaFaida


~Firmina Victor

(Author,Youth Mentor)

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...