1.Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
5. Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.
EZR. 1:1, 5 SUV
✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
Omba Mungu aamshe roho za watu ambao wamekusudiwa kutumiwa nae kutimiza Neno lake maishani mwako
Ili kupenya maishani inahitajika watu Mungu aamshe roho zao watumike kukubariki,
Watumike kukuvusha mahali,
Watumike kukusemea mahali upate kibali,
Watu waamshwe roho zao watoe pesa zao,muda wao, mawazo yao kwako ili uvuke kwenda hatua nyingine ya maisha.
Ili kusudi la Mungu kwako 2021 litimie unahitaji watu.
*Na hao watu ni mpaka Mungu awe ameamsha roho zao kutenda kwako,* hawawezi kutenda tu hivi hivi.
Ombi letu leo,
Ee Mungu wangu amsha roho za watu waliokusudiwa kutenda kwangu ili Neno lako kwa mwaka huu 2021 litimie kwangu.
Hii ni kanuni mojawapo ya kiroho ya kusababisha mambo kutokea katika eneo/jambo lako lolote.
Omba Mungu aamshe roho za waliokusudiwa kukusaidia uvuke hapo ulipo.
Umebarikiwa!
No comments:
Post a Comment