Wednesday, July 19, 2017

#Majira kwenye maisha: (kwa ufupi tu)


Kuna majira makuu manne kwenye maisha.
1.Asubuhi ya maisha yako
2. Mchana ya maisha yako
3.Jion ya maisha yako.
4. Usiku wa maisha yako.

1. Asubuhi.
Asubui ni kipindi toka kuzaliwa mpaka kumaliza elimu yako na kuanza kujitegemea au kujisimamia mwenyewe.
unaweza ukawa na asubuhi nzuri sana au mbaya sana. lakini hiyo haizuii wewe kuwa na mchana mzuri.
Hapa wengine husahau kuwa asubuhi huwa inapita haraka sana na kuzembea au kupuuzia maelekezo wanayopewa na walioko mchana na jioni!

2. Mchana
Ni kipindi cha kufanyia kazi maarifa yote uliyoyapata asubui, ie kutoka kwa wazazi, kutoka shuleni, kutoka kwenye maeneo mbalimbali uliyojifunza.
Ni kipindi cha kujenga maisha yako huku ukijua siku moja jua litachwea, na itakua jioni.
Hapa vijana wengi hujisahau na kudhani siku zote itabaki kuwa mchana, hivyo jioni huwajia kwa kushtukiza.
Wapo wanaoitumia mchana yao vizuri na kuwa na uhakika na jioni njema sana.

3.Jioni
Hiki huwa ni kipindi cha kufaidi matunda ya kazi uliyoifanya mchana.
Huwa sio kipindi cha kufanya kazi, ila kama ulizembea na kuzubaa mchana, unaikuta inakulazimu kufanya shughuli ambazo ulipaswa uwe umezifanya ilipokua mchana wako
Hiki ni kipindi cha kujiandaa na usiku. maana usku huwa hauchelewi sana ikishafika jioni.
Chochote ulichokipanda mchana, hapa jioni ndio unakivuna sasa! na kinakua dhahiri kiasi kwamba hata walioko mchana wanaona.

4. Usiku
Hiki ni kipindi cha kujiandaa kupumzika. maana sasa ni usiku. huwezi tena kufanya kazi. giza limeingia.
hapa sasa kama ulitumia mchana na jioni yako vizuri, usiku wako utakua na mwanga, hivyo hutakaa gizani.
ila kama uliutumia vibaya, usiku wako utaishia kuwa gizani na hakuna atakayejua kama upo maana hutaonekana, ni usikuu!

Nimeeleza kwa ufupi sana.Nadhani utakua umeelewa na kujua wewe uko majira gani.

na kama unatumia majira yako vizuri huku ukijua kuwa hayo majira kuna siku yatapita utaingia majira mengine na hutaweza kufanya tena yale ya majira ya nyuma!

Usipoteze muda! Tumia muda wako vizuri. Majira hayagandi.
Ubarikiwe sana!
~Minna Matee

Friday, June 2, 2017

#UMRI MKUBWA HAUMAANISHI KUKUA NA KUKOMAA!


Webrania 5:13-14
13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 
14 Lakini CHAKULA KIGUMU ni cha WATU WAZIMA, ambao akili zao, kwa KUTUMIWA, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.



Mara nyingi huchukuliwa kuwa mtu akiwa na umri mkubwa amakua pia amekomaa na amekua kiasi cha kuweza kuchukua na kukabiliana na majukumu mbalimbali.
#kiuhalisia kumbe sivyo.
Mtu anaweza akawa na miaka mingi lakini akili yake ni kama anamiaka miwili!
#Hivyo hivyo na maisha ya kiroho!
Kuwa na miaka mingi katika wokovu sio kigezo cha kuwa mtu huyo amekua na amekomaa kiroho!
#Unaweza ukawa na miaka 10 ya wokovu na ukawa na tabia na mwenendo wa mtu aliyeokoka jana ambae anajifunza kutembea!
#Unaweza ukawa na miezi sita tu kwenye wokovu, na ukawa kama mtu mwenye miaka 5 kwenye wokovu!
#NINI HUSABABISHA HIZI TOFAUTI?
#ziko sababu nyingi,
mojawapi ni aina ya chakula unachokula na kukifanyia mazoezi.
Ukimpa mtoto chakula tu bila kumcheulisha au kumfanya acheze kile chakula hakitafanya kazi na kukua kwake kutakua na hitilafu!
#Ukila chakula kila siku na kubaki umekaa tu, chakula kile hakiwezi kufanya kazi! Lazima utoke, ufanye kazi au mazoezi ili chakula kile kifanye kazi vizuri katika mwili wako, nawe uweze kukua vizuri na kuwa na afya njema!
#Ndivyo ilivyo na maisha ya wokovu!
Aina ya chakula unachokula kinamchango mkubwa sana katika ukuaji wako.
#Mtoto wa miaka 5 huwezi kuendelea kumnywesha maziwa tuuuu!
kwanza hatashiba!
pili hatakua!
#Anapaswa kupewa vyakula vigumu, atafune mwenyewe mifupa!
#Mkristu wa miaka mitano kwenye wokovu bado anakunywa maziwa tuuuu ana hatari na afya yake.
# Unakuta bado anategemea kulishwa, hawezi kula mwenyewe, hiyo ni dalili mbaya.
#Hawezi kusoma Neno mwenyewe na kumsikia Mungu akisema nae, mpaka mchungaji wake amtafsirie kila kitu, huyo anashida kubwa.
#Akiumwa mafua tu anaenda kutafuta penye maombi akaombewe, huyo anashida kubwa!
#Lazima ufike umri uweze kujihudumia baadhi ya vitu, na ndio uanafunzi ambao Yesu anawafundisha wanafunzi wake.
#Aliwafundisha na baaday ya hapo akawatuma waende wakafanya kazi.
#Hawakukaa tuu wakiendelea kula bali walitoka wakaenda kufanyia kazi kile Yesu alichowafundisha na ndipo walipo kuwa na kuwa mitume wakubwa hata leo tunasoma habari zao.
#Jipime mwenyewe ujue uko wapi, ili uweze kuamka usingizini na kuishi maisha sawa na umri wako!
Minna Matee
 @2017

Tuesday, May 30, 2017

NENO LA MSALABA~NGUVU YA MUNGU-II

...Baada ya kuona sehemu ya kwanza ya somo hili, leo tutaangalia sehemu ya pili na somo lenye kichwa hiki:
NENO LA MSALABA-NGUVU YA MUNGU!

Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu. 
1Kor1:18



Hilo ndio andiko letu la kusimamia katika somo hili ambalo tumeweza kuangalia katika sehemu ya I (fuatilia post za nyuma kulisoma), mateso ya Yesu pale msalabani kwa jinsi ya mwili na namna alivyoteseka kwa ajili yangu na wewe.

Leo tutaangalia mateso aliyoyapata kiroho!


 #Hapo zamani za kale
 Zamani wana wa Israel iliwapasa kuchinja mwanakondoo kama sadaka ili damu yake iweze kuondoa dhambi zao,sawa na maagizo aliyopewa Musa na Mungu.Na mwanakondoo huyo alipaswa kutokua na kilema wala chongo yaani asiwe na hitilafu yoyote.

Zoezi hili likaonekana halifai tena na ndipo Mungu akaamua kumtuma Mwanae wa pekee, ili aweze kuwa huyo mwanakondoo na akishafanyika dhabihu mara moja, ni basi! tofauti na zamani ilibidi kila wanapotaka kujitakasa iliwapasa kutafuta mnyama wa kutoa dhabihu!

#Yesu hakuijua Dhambi ila Alifanyika Dhambi!
Kwa sababu alitakikana mwanakondoo asie na hitilafu, hali kadhalika ilimpasa Mungu kumchukua mwanae ambae hakuijua dhambi wala hakua na dhambi ili awe mwana kondoo wa ulimwengu amwage damu yake kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu.

#Haikuwa Rahisi
Haikuwa rahisi kabisa kwa Yesu kuwa dhambi (to become sin) wakati hakuwahi kuijua Dhambi(knew no sin). 2Korintho5:21.

#Aliomba kikombe kiepushwe
Yesu aliijua kazi iliyombele yake kuwa haikuwa rahisi na hasa ule wakati wa kuwa dhambi ilhali hakuijua dhambi.
Alipokua pale bustanini alimwomba Baba yake amwepushe ni hiki kikombe,lakini aliyaruhusu mapenzi ya Baba yatimie!

#Dhambi ilimtenga na Baba yake kwa sekunde kadhaa. 
Yesu hakuwahi kutengwa na Mungu kabisa hata sekunde moja.
 Lakini kwa sababu Mungu hakai mahali  penye dhambi, automatic ilimlazimu Yesu kutengwa na Baba kwa sekunde kadhaa ili awe dhambi kwa ajili yetu na sisi tufanyike Haki ya Mungu(the rightuousness of God) Hivyo kupitia yeye(Yesu) tumefanyika haki ya Mungu.

#ELoiEloi Lama Sabakitani
Yesu alipolia kuwa Mungu wangu,Mungu wangu mbona umeniacha (Mathayo27:46) alikua analia kwamba ameonja ilivyo mbaya na ngumu kutengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi!

Yesu anajua ilivyo, mwanadamu anapotenda dhambi na kuachwa na Mungu, ni mbaya sana(very bad experience), ambayo hakuitamani wala kuitaka ila kwa sababu ya kuukomboa ulimwengu alikubali mateso haya ya rohoni ili sisi tupate uhalali wakuwa Haki ya Mungu!

#Yote aliyafanya kwa Upendo Mwingi!
 Yesu aliyafanya haya yote kwa upendo mwingi na baada ya yooote,  #Alikirimiwa Jina lipitalo majina Yote! Wafilipi 2:9

#Nguvu ya Jina alilopewa
Sasa unaweza kuona uwezo na nguvu iliyopo kwenye Jina alilokirimiwa mwana wa Mungu, Alilifanyia kazi kubwa na ndio maana kwa Jina lake, kila goti linapigwa na kila ulimi unakiri kuwa Yeye ni Bwana juu ya vyote!

#Naamini kupitia Somo hili umeweza kuona namba ambavyo Neno la Msalaba kwetu sisi tunaoamini ni NGUVU YA MUNGU, ila kwao wasioelewa ni Upuuzi!

Mungu akubariki sana tukutane wakati mwingine kwa Somo lingine!

~Imeandikwa na Firmina Matee
watsap: 255 753 008 212
www.amenhalleluyah.blogspot.com
 @2017 

Thursday, May 18, 2017

NENO LA MSALABA~NGUVU YA MUNGU.

Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu.
1Kor1:18
~~~~~~~~~
Ukiangalia haraka haraka unaweza usielewe kwa undani ni kitu gani Yesu Alikifanya kwa ajili yako na yangu pale msalabani.

Hebu leo tuangalie mateso ya kimwili aliyopata:


#Alitemewa mate hadharani na kuzabwa vibao usoni.(Matayo 26:67)
Ilikua ni dharau kubwa mno kwa mtu kutemewa mate hadharani,kuzabwa vibao na akiambiwa maneno ya kejeli na kutukanwa na watu aliokua ameponya ndugu zao, amtoa pepo watoto wao na kuwalisha chakula cha bure wakiwa wanamsikiliza ilhali yeye hakuwa na kosa lolote.

#Alinyofolewa Ndevu (Isaiah 50:6)
Uliwahi kujaribu kujinyofoa kinyweleo chako kimoja tu au unywele wako mmoja tu hadi ukatoka! uliwahi kuwaza hayo maumivu yakoje? Sasa Pata picha Yesu alinyofolewa ndevu zake zote hadi zikaisha. Na ujue wakati ule wayahudi walifuga ndevu, na ndevu ilikua ishara ya uanaume na mamlaka kama mwanaume. Mtu kuwa na mzuzu ilikua ni fahari kwao. Sasa Yesu akanyofolewa moja baada ya nyingine.

#Alipigwa na mjeledi (Marko 15:15)
Mjeledi huu haukua kama huu unaoujua wachunga mbuzi na ngombe wanaotumia. Huu Mjeledi ulikua ni ngozi zimeunganishwa pamoja kama mikanda mingi pamoja, halafu kila kimkanda kimechomekwa vipande vya mifupa au meno wanayama ilimradi iwe imechongoka.

#Upigwaji wa mijeledi
Namna walivyokua wanaipiga sio juu juu! Yaani wanauvuta kutoka juu halafu unaingia kisawasawa ndani na kutoka na vinyamanyama na zoezi hilo lilifanyika sio mara moja, tu alikua akipigwa mijeleji hata 100. Maana yake, mpaka anafika mara ya 10 ameshatoka na nyama za kutosha na damu nyingi sana zimeshamwagika.Hivyo wengi waliokua wanapewa adhabu hiyo walifia njian kabla ya kutimiza idadi ya viboko kwa sababu ya kupoteza damu nyingi sana! Hata hivyo iliwashangaza sana wayahudi kuwa Yesu hakufa hapo, wakasahau kuwa Unabii ulipaswa kutimia kuwa ...aliangikwa mtini... hivyo Yesu alipaswa kuimaliza kazi.

#Alivalishwa Taji la Miiba.(Yohana19:2)
Yaani miiba ilitengenezwa kuweza kufunika kichwa chake. Maana yake kichwa chote kilikua kinatobolewa na hiyo miiba kwa muda wote kwanzia alipovishwa mpaka anaangikwa msalabani.

#Kumbuka, usiku wa kuamkia siku hii, Yesu hakulala kabisa alikua bustanini akimwomba Mungu Baba.

Kwa hiyo unaweza kupata picha hasa hali ya mwili wa Yesu ilivyokua kama mwanadamu wa kawaida, mwenye nyama na damu. Kama si uwezeshaji wa kiUngu ndani yake haya ni mateso makali mno.

#Alibebeshwa Msalaba mzito.
Msalaba huu unasadikiwa kuwa na uzito wa zaidi ya paund 300 sawa na kilogramu 150.(paund 1 ni sawa na kg 0.5). uzito huu aliubeba katika mwili ambao tayari ulijaa majeraha ya kupigwa mijeledi na kichwa kilichovikwa miiba.

Mpaka hapo unaweza kuanza kupata walau picha kile Yesu alichokipitia bila kusahau kuwa hakuwa ametenda kosa lolote! Na haya yote aliyapitia kwa ajili yako na mimi. Maana yake mimi na wewe ndio tulitakiwa kuyapitia haya ila badala yake yeye aliyabeba ili sasa hivi mimi na wewe tusiyapitie hayo tena!
Mpaka hapo unaweza kujiuliza sasa kwa nini mimi niko hapa napitia magonjwa, huzuni, umaskini, kukataliwa wakati tayari Yesu alipitia hayo yote ili mimi sasa hivi niishi katika viwango vingine?

Ni mpaka IAMINI ile kazi ya msalaba na kuiona kuwa ya thamani sana kuliko chochote, ndipo utaanza kuona ikiwa halisi kwako.

ndipo maana kwetu sisi TULIOOKOLEWA, kazi ya MSALABA ni NGUVU YA MUNGU, ila kwao WANAOPOTEA ni UPUUZI!!!!

Tutaendelea kesho..endelea kutafakari kwanza hii.

~Firmina Matee
@2017.

Friday, April 28, 2017

#BatimayoKipofu -(II) #Marko10


Yesu alipomwita huyu kipofu alimuuliza swali moja.
"Unataka nikufanyie nini?"
Batimayo Kipofu akajibu haraka, "nataka kuona."

Usipojua unachotaka hata ukikutana na msaada wa kukutoa ulipo bado hutaweza kutoka hapo.
Usipojua unapaswa kutoka hapo ulipo na kwenda wapi? hutajua msaada wa kukutoa hapo uko wapi.
Batimayo aliposikia Yesu anapita, alijua huyu ndiye Jibu la Ombi langu.
Akaanza kumwita kwa sauti kuu bila kujali nani anasema nini.
Tambua unataka nini, ili msaada wa kukuvusha utakapokuja uweze kuutambua na kuutumia vizuri.

#BatimayoKipofu #Marko10


Kulikua na kipofu mmoja wakati wa Yesu, alimwita Yesu kwa sauti ili amponye upofu wake.
Waliomsikia walikua wanamkataza asipige kelele..
Yesu alipomsikia akawaambia wamwache, nae akaja kwa Yesu akaponywa.



Kwenye maisha kuna aina ya watu utakutana nao, wao kazi yao ni kukunyamazisha ili usipate ule msaada utakaokutoa ulipo.
Wao wanafurahi tu kukuona kila siku uko ulipo.
Ukitaka kutoka hapo, wataanza kukwambia haiwezekani ukawa hicho unachotaka.
Utaambiwa huwezi kuonana na yule au kufanya kazi na huyu, ni mtu mkubwa sana kwako.
Lakini yule kipofu, aliendelea kumwita Yesu!
Na hiyo ndio ilikua pona yake.
Angenyamaza asingepata muujiza wake!
Usikate tamaa, hata kama kuna wanaokunyamazisha!
Endelea tu, siku moja utasikika!

Friday, February 17, 2017

#Leo Nizungumze na Binti.


Unajua kwamba wewe ni wa THAMANI sana kuliko chochote pesa inaweza kununua?
Unajua kwamba wewe ulipoumbwa MUNGU aliona mama wa Vizazi vingi ndani yako?
Unajua kwamba umebeba HATMA ya mume wako na watoto wako?
Unajua kwamba ukiamua KUJITAMBUA utakua umesaidia wangapi?
Image may contain: shoes and closeup
#Sasa Basi kwa hayo machache,
Nataka,
Uinuke,
Ufute machozi,
Ujiangalie kwenye Kioo,
Alafu ujiambe haya..
#Mimi ni wa thamani sana.
Hakuna pesa inaweza fikia thamani nliyonayo!
#Mimi ni mzuri na mrembo kwa sababu Nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha.
#Mimi nitaishi kutimiza kusudi la Mungu na si vinginevyo
#Hakuna mtu wala mazingira yatakayonikwamisha kwa sababu Yesu aliye ndani yangu ni mkuu kuliko mazingira na hali zozote zinazonipinga.
##Wewe ni Shujaa
##Wewe ni Shujaa
##Wewe ni shujaa

#KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU!

Hivi ulishawahi kukutana na mlevi aliyezoea pombe?

ukimkaribia tu hata kama hajanywa pombe utasikia harufu ya Pombe, yaani huhitaji kuuliza utajua tu ni mlevi!

Kwa sababu kile kilevi kimemwingia ndani yake haswaaa!
Je wale wenzetu, wanaopenda kula vitunguu swaumu sana,,
yaani ukimsogelea tu, utasikia harufu ya vitunguu saumu na vile viungo vyao vingine!Akiongea ndio usiseme!!

Kwa sababu vile viungo viko ndani yake.

#Kwenye Yohana 15, Yesu anatuambia TUKAE NDANI YAKE NAE NDANI YETU!

Yeye akikaa ndani yetu ni zaidi ya hiyo mifano nliyoitoa hapo juu!!
Yaani maana yake utakua unanukia yeye, ukizungumza tutasikia yeye, iko ndani yako!

Vipi kuhusu,sisi tukikaa ndani yake inakuwaje?
Uliwahi kuwa ndani ya nyumba alafu akapita mtu kwa nje, unadhani yule mtu atakuona?
Hapana, ni mpaka aingie ndani au wewe utoke nje!
yaani ile nyumba inakua imekuficha kwa sababu uko ndani yake!

Sasa, Yesu anasema KAENI NDANI YANGU,

Yaani ukikaa ndani yake, ni wazi kuwa ili uonekane lazima au wewe utoke nje au aliyeko nje aingie ndani kupitia yeye(mlango) ndio muonane!

#SASA CHANGANYA HIZI MBILI,
KAENI NDANI YANGU, NAMI NDANI YENU!!
Yaani unakua ndani Yesu, Nje Yesu!

Kote kote Yesu!

Alafu anasema Ukishafanya hivyo, OMBA LOLOTE KWA JINA LANGU, Nawe Utapata!

#Hebu pata picha katika hicho kiwango kuna uwezekano wa kukosa utakacho?,, wakati YEYE YUKO NDANI YAKO, NA WEWE UKO NDANI YAKE!

#Amua Leo Kuwa Ndani Yake, nae Ndani Yako!
#YesuNdaniYangu!!

Tuesday, February 7, 2017

# Darasa La Hekima #KWA WAZAZI WOTE na WAZAZI WATARAJIWA WOTE.

Mzazi mpende mwanao leo,
Mwonyeshe upendo leo,
Mfundishe kumpenda Mungu leo,
Mwambie unampenda leo,

Huwezi kujua Mungu amekupa kuwa nae kwa muda gani!
Yaweza kuwa muda mfupi sana au miaka mingi sana!

Ila fanya leo.


Ukiondoka hawezi kukumbuka mali ulizoacha.. Ila ataukumbuka upendo wako..
hekima zako..
busara zako..

Usijidai uko busy sana na kazi, ukasahau familia yako..
Watoto wanakuona usiku kwa usiku au baada ya siku kadhaa..

Jua kuwa wanahitaji upendo wako..

Kama kuna kitu cha thamani unaweza kuwapa wanao leo ni MUDA wako.

Ongea nao
Sali nao
Cheza nao
Cheka nao

Ni rahisi kukumbuka tabasamu lako kuliko hata zawadi uliyowaletea!

Ni rahisi kukumbuka sala yako kuliko maneno uliyosema ulipokua unawagombeza..

Ni rahisi kukumbuka kuwa uliwaambia unawapenda kuliko matusi uliyowahi kuwatukana..

#Fanya leo
#Onyesha Upendo Leo

Wednesday, February 1, 2017

#DarasaLaHekima #TendaMemaWakatiWote

Hatufanyi mema kwa sababu tunalipa wema,
au kwa sababu tunatafuta kuja kufanyiwa mema,

#Tunafanya mema kwa sababu ni asili yetu!

#Tunafanya mema kwa sababu tumeumbiwa hayo kuyafanya!

#Tunafanya mema kwa sababu aliye ndani yetu ni mtenda mema!

#Tunafanya mema kwa sababu ni wajibu wetu!

#Tunafanya mema kwa sababu ni utamaduni wa ufalme wetu kutenda mema!

Monday, January 30, 2017

#DarasaLaHekima #NoaUpangaWako


Upanga ni upanga uwe mKali au mButu.

Lakini tofauti kati yake itaonekana wakati wa matumizi.

Upanga ulionoelewa ni mkali na unapotumika huleta maangamizi makubwa kwa wakati mmoja.

Upanga butu, hutumika pia ila madhara yake ni madogo, na huenda mtumiaji akatumia nguvu kubwa sana wakati wa kuutumia!

Maombi ni kama upanga,

Maombi yenye maarifa sahihi ya Neno la Mungu, ni kama upanga ulionolewa!

Maombi yasiyo na maarifa sahihi ya Neno la Mungu ni kama upanga butu!

#Unaweza kunoa upanga wako kila siku kwa kuhakikisha unajifunza kila siku kitu kipya kuhusu Mungu.

#Upanga wako unavyozidi kuwa mkali, ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kuutumia!

Friday, January 20, 2017

#DarasaLaHekima #Jifunze kwa mnyama Simba


Leo ntazungumza na wewe kuhusu mnyama Simba,

🦁Simba sio kwamba ni mnyama mkubwa kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mwenye nguvu kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mjanja kuliko wote mwituni,

🦁Wala sio mnyama mwenye mbio kuliko wote mwituni..

🦁LAKINI SIMBA NDIO MFALME WA MWITU(King of the Jungle)

🤕Akinguruma wanyama wote wanaogopa

🏃🏿‍♀🏃🏼Akitokea wanyama wote na binadamu wanakimbiaaaa

🤔Unafikiri ni kwa nini?

🦁Kwa sababu ya MTAZAMO wake.

😋Yeye akiona mnyama au mtu anaona anaona chakula                        

 🍽Yeye hajawahi kuona analiwa bali yeye ndio anakula wengine

🦁Hiyo ni sifa moja inayompa ushindi mkubwa Simba.                        

 🐝Wale wapelelezi walioenda kuipeleleza nchi ya Kanani,waliporudi kuna walioona Majitu, na Joshua na Kalebu wao waliona maziwa na asali 

👀Kilichowatofautisha ni Mtazamo wao juu ya Kanaani.

❓Je wewe unaona nini kwenye ulilonalo?

❌Ishu sio TATIZO,ishu ni Mtazamo wako juu ya hilo tatizo.

🚥Namna unavyoona mambo, ndio inategemea matokeo utakayopata kutoka kwenye hilo jambo.

📝Hatua ya kwanza ya kubadilisha jambo lolote, inaanzia kwenye mtazamo wako juu ya hiyo jambo.                        

 ⛔Badili mtazamo na utaanza kuona mwanga wa namna ya kutoka hao ulipo.

...Tutaendelea sehemu ya pili kesho
#DarasaLaHekima
#Minna2017
#JifunzeKwaMnyamaSimba

Thursday, January 19, 2017

#DarasaLaHekima #TumiaTicketYakoVizuri

Mtu mmoja akasafiri kwenye ndege akiwa na ticketi iliyokua imelipwa nauli pamoja na chakula chake cha kula njiani kwenye ticketi yake.
Akasafiri na katikati ya safari, akaja mhudumu akimuuliza, amletee chakula gani,
Mtu yule akakataa kuagiza, akijua kuwa anatakiwa kujilipia gharama ya chakula na hakuwa na hela.
Mtu yule alishinda na njaa safari yote, na alipofika mwisho wa safari, akapokelewa na mwenyeji wake.
Mtu yule akaomba apewe chakula na maji kwa sababu hakuwa amekula safari yote.
Ndipo mwenyeji wake akamuuliza, kwa nini hakula, akasema hakuwa na hela ya kununua chakula.
Ndipo mwenyeji wake akamsikitikia sana, na kumwambia, kula kitu kilikua kimeshalipiwa kwenye ticketi yako.
Ulichotakiwa kufanya ni kuagiza uwezavyo!!

Yule mtu kuingalia ile ticketi yake vizuri, kweli akakuta ina na kuponi ya chakula ndani!!!

oooh maskini mtu yule!!!

Ndivyo ilivyo na kwako!
Ukiamua kumpokea Yesu unapata si tu tikcet ya kwenda mbinguni bali pamoja na "lunchbox" ya kula njiani unapoelekea mbinguni!
Lunch box yako ina kila chakula unachotaka,
ukitaka uponyaji, utajiri, amani, furaha, ujasiri, upendo, kilaaa aina ya menu unayotaka ipo!!
Ni wewe tu kutambua kuwa ticket yako imelipiwa si tu nauli bali na gharama za chakula cha njiani!!
Wakristu wengi wanasafiri njiani wakiwa na njaa wakijua tu wao ticketi yao ni a kwenda mbinguni tu, haijalipiwa gharama ya chakula, hivyo wanaishi maisha ya kung'ang'ana sana wakijaribu kujilipia wenyewe gharama ya lunch!!!

Sikiliza,
IMESHALIPWA NDANI YA TICKETI YAKOOO! WEWE AGIZA TU!

Usikae na njaa wakati ticket yako inakuruhusu kula njiani.
#KwaYesuKunaVyote
#TumiaTicketiYakoVizuri
#Minna2017
#DarasaLaHekima

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...