...Baada ya kuona sehemu ya kwanza ya somo hili, leo tutaangalia sehemu ya pili na somo lenye kichwa hiki:
NENO LA MSALABA-NGUVU YA MUNGU!
Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu.
1Kor1:18
Hilo ndio andiko letu la kusimamia katika somo hili ambalo tumeweza kuangalia katika sehemu ya I (fuatilia post za nyuma kulisoma), mateso ya Yesu pale msalabani kwa jinsi ya mwili na namna alivyoteseka kwa ajili yangu na wewe.
Leo tutaangalia mateso aliyoyapata kiroho!
#Hapo zamani za kale
Zamani wana wa Israel iliwapasa kuchinja mwanakondoo kama sadaka ili damu yake iweze kuondoa dhambi zao,sawa na maagizo aliyopewa Musa na Mungu.Na mwanakondoo huyo alipaswa kutokua na kilema wala chongo yaani asiwe na hitilafu yoyote.
Zoezi hili likaonekana halifai tena na ndipo Mungu akaamua kumtuma Mwanae wa pekee, ili aweze kuwa huyo mwanakondoo na akishafanyika dhabihu mara moja, ni basi! tofauti na zamani ilibidi kila wanapotaka kujitakasa iliwapasa kutafuta mnyama wa kutoa dhabihu!
#Yesu hakuijua Dhambi ila Alifanyika Dhambi!
Kwa sababu alitakikana mwanakondoo asie na hitilafu, hali kadhalika ilimpasa Mungu kumchukua mwanae ambae hakuijua dhambi wala hakua na dhambi ili awe mwana kondoo wa ulimwengu amwage damu yake kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu.
#Haikuwa Rahisi
Haikuwa rahisi kabisa kwa Yesu kuwa dhambi (to become sin) wakati hakuwahi kuijua Dhambi(knew no sin). 2Korintho5:21.
#Aliomba kikombe kiepushwe
Yesu aliijua kazi iliyombele yake kuwa haikuwa rahisi na hasa ule wakati wa kuwa dhambi ilhali hakuijua dhambi.
Alipokua pale bustanini alimwomba Baba yake amwepushe ni hiki kikombe,lakini aliyaruhusu mapenzi ya Baba yatimie!
#Dhambi ilimtenga na Baba yake kwa sekunde kadhaa.
Yesu hakuwahi kutengwa na Mungu kabisa hata sekunde moja.
Lakini kwa sababu Mungu hakai mahali penye dhambi, automatic ilimlazimu Yesu kutengwa na Baba kwa sekunde kadhaa ili awe dhambi kwa ajili yetu na sisi tufanyike Haki ya Mungu(the rightuousness of God) Hivyo kupitia yeye(Yesu) tumefanyika haki ya Mungu.
#ELoiEloi Lama Sabakitani
Yesu alipolia kuwa Mungu wangu,Mungu wangu mbona umeniacha (Mathayo27:46) alikua analia kwamba ameonja ilivyo mbaya na ngumu kutengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi!
Yesu anajua ilivyo, mwanadamu anapotenda dhambi na kuachwa na Mungu, ni mbaya sana(very bad experience), ambayo hakuitamani wala kuitaka ila kwa sababu ya kuukomboa ulimwengu alikubali mateso haya ya rohoni ili sisi tupate uhalali wakuwa Haki ya Mungu!
#Yote aliyafanya kwa Upendo Mwingi!
Yesu aliyafanya haya yote kwa upendo mwingi na baada ya yooote, #Alikirimiwa Jina lipitalo majina Yote! Wafilipi 2:9
#Nguvu ya Jina alilopewa
Sasa unaweza kuona uwezo na nguvu iliyopo kwenye Jina alilokirimiwa mwana wa Mungu, Alilifanyia kazi kubwa na ndio maana kwa Jina lake, kila goti linapigwa na kila ulimi unakiri kuwa Yeye ni Bwana juu ya vyote!
#Naamini kupitia Somo hili umeweza kuona namba ambavyo Neno la Msalaba kwetu sisi tunaoamini ni NGUVU YA MUNGU, ila kwao wasioelewa ni Upuuzi!
Mungu akubariki sana tukutane wakati mwingine kwa Somo lingine!
~Imeandikwa na Firmina Matee
watsap: 255 753 008 212
www.amenhalleluyah.blogspot.com
@2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...
Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...

-
Some people would say that God is against prosperity, but these ten famous Christian businessmen would disagree. In fact, they would likel...
-
The Pencil Maker took the pencil aside, just before putting him into the box. "There are 5 things you need to know," he to...
-
Many people assume that listening and hearing are one and the same. However, there is a big difference between the two. Unless they were ...
No comments:
Post a Comment