Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu.
1Kor1:18
~~~~~~~~~
Ukiangalia haraka haraka unaweza usielewe kwa undani ni kitu gani Yesu Alikifanya kwa ajili yako na yangu pale msalabani.
Hebu leo tuangalie mateso ya kimwili aliyopata:
#Alitemewa mate hadharani na kuzabwa vibao usoni.(Matayo 26:67)
Ilikua ni dharau kubwa mno kwa mtu kutemewa mate hadharani,kuzabwa vibao na akiambiwa maneno ya kejeli na kutukanwa na watu aliokua ameponya ndugu zao, amtoa pepo watoto wao na kuwalisha chakula cha bure wakiwa wanamsikiliza ilhali yeye hakuwa na kosa lolote.
#Alinyofolewa Ndevu (Isaiah 50:6)
Uliwahi kujaribu kujinyofoa kinyweleo chako kimoja tu au unywele wako mmoja tu hadi ukatoka! uliwahi kuwaza hayo maumivu yakoje? Sasa Pata picha Yesu alinyofolewa ndevu zake zote hadi zikaisha. Na ujue wakati ule wayahudi walifuga ndevu, na ndevu ilikua ishara ya uanaume na mamlaka kama mwanaume. Mtu kuwa na mzuzu ilikua ni fahari kwao. Sasa Yesu akanyofolewa moja baada ya nyingine.
#Alipigwa na mjeledi (Marko 15:15)
Mjeledi huu haukua kama huu unaoujua wachunga mbuzi na ngombe wanaotumia. Huu Mjeledi ulikua ni ngozi zimeunganishwa pamoja kama mikanda mingi pamoja, halafu kila kimkanda kimechomekwa vipande vya mifupa au meno wanayama ilimradi iwe imechongoka.
#Upigwaji wa mijeledi
Namna walivyokua wanaipiga sio juu juu! Yaani wanauvuta kutoka juu halafu unaingia kisawasawa ndani na kutoka na vinyamanyama na zoezi hilo lilifanyika sio mara moja, tu alikua akipigwa mijeleji hata 100. Maana yake, mpaka anafika mara ya 10 ameshatoka na nyama za kutosha na damu nyingi sana zimeshamwagika.Hivyo wengi waliokua wanapewa adhabu hiyo walifia njian kabla ya kutimiza idadi ya viboko kwa sababu ya kupoteza damu nyingi sana! Hata hivyo iliwashangaza sana wayahudi kuwa Yesu hakufa hapo, wakasahau kuwa Unabii ulipaswa kutimia kuwa ...aliangikwa mtini... hivyo Yesu alipaswa kuimaliza kazi.
#Alivalishwa Taji la Miiba.(Yohana19:2)
Yaani miiba ilitengenezwa kuweza kufunika kichwa chake. Maana yake kichwa chote kilikua kinatobolewa na hiyo miiba kwa muda wote kwanzia alipovishwa mpaka anaangikwa msalabani.
#Kumbuka, usiku wa kuamkia siku hii, Yesu hakulala kabisa alikua bustanini akimwomba Mungu Baba.
Kwa hiyo unaweza kupata picha hasa hali ya mwili wa Yesu ilivyokua kama mwanadamu wa kawaida, mwenye nyama na damu. Kama si uwezeshaji wa kiUngu ndani yake haya ni mateso makali mno.
#Alibebeshwa Msalaba mzito.
Msalaba huu unasadikiwa kuwa na uzito wa zaidi ya paund 300 sawa na kilogramu 150.(paund 1 ni sawa na kg 0.5). uzito huu aliubeba katika mwili ambao tayari ulijaa majeraha ya kupigwa mijeledi na kichwa kilichovikwa miiba.
Mpaka hapo unaweza kuanza kupata walau picha kile Yesu alichokipitia bila kusahau kuwa hakuwa ametenda kosa lolote! Na haya yote aliyapitia kwa ajili yako na mimi. Maana yake mimi na wewe ndio tulitakiwa kuyapitia haya ila badala yake yeye aliyabeba ili sasa hivi mimi na wewe tusiyapitie hayo tena!
Mpaka hapo unaweza kujiuliza sasa kwa nini mimi niko hapa napitia magonjwa, huzuni, umaskini, kukataliwa wakati tayari Yesu alipitia hayo yote ili mimi sasa hivi niishi katika viwango vingine?
Ni mpaka IAMINI ile kazi ya msalaba na kuiona kuwa ya thamani sana kuliko chochote, ndipo utaanza kuona ikiwa halisi kwako.
ndipo maana kwetu sisi TULIOOKOLEWA, kazi ya MSALABA ni NGUVU YA MUNGU, ila kwao WANAOPOTEA ni UPUUZI!!!!
Tutaendelea kesho..endelea kutafakari kwanza hii.
~Firmina Matee
@2017.
No comments:
Post a Comment