Saturday, October 28, 2023

UMEWAHI KUONA NAMNA MCHWA WANAVOJENGA NYUMBA YAO ?

Ukiikuta imeisha unaweza kudhani ni mwanadamu ametengeneza...!




Lakini ukichunguza kwa makini utagundua hakuna mwanadamu wala kiumbe kingine chochote kimewasaidia bali ni bidii na juhudi yao wenyewe wakishirikiana kwa pamoja na kufanikisha ujenzi wa
jumba lao.

πŸ“Siri kubwa hapo ni umoja, bidii na juhudi!

πŸͺ¨Hakuna namna mafiga haya matatu yatakaa pamoja kisiive chakula kitamu!

Popote watu wanapoamua kufanya kitu kwa umoja kwa bidii na kwa juhudi lazima wapate matokeo.

Haijalishi kile wanachotaka kufanya ni kizuri au kibaya, lazima kitafanikiwa!

πŸ›•Hapo zamani, watu wa Babeli walitaka kujenga mnara ili uwawezeshe wafike mbinguni!
Watu wale walikuwa na umoja kiasi cha kuongea lugha moja na kuwasaidia kuelewana wote.

Watu wale walikuwa na bidii sana katika kazi yao kwani waliifanya usiku na mchana.
Na watu wale walikua na juhudi sana katika kazi ile..

Na walifanikiwa kuanza kuujenga mnara ule, Ijapokuwa nia yao haikuwa njema.

Umoja huo ulivunjika baada ya lugha yao kuchanganywa na wao kushindwa kusikilizana!

Na ndipo lengo lao kushindwa kutimizwa.

Figa moja lilibomoka. Mafiga yale mawili hayakuweza kupika chakula(kutimiza lengo).

Mifano hii miwili ikawe chachu kwako kuwa na umoja, juhudi na bidii katika malengo yako ili kuyatimiza kwa kishindo!

Unaweza!
Firmina Victor
(Whatsapp +255679300845)

Sunday, April 11, 2021

HABARI YA RUTH



RUTH 1:

Tunaona kulikua na njaa katika Israel hivyo bwana mmoja aitwae Elimeleki na familia yake wakawa wanakimbia njaa..πŸ˜©πŸƒπŸƒπŸƒπŸ‘¨πŸ‘©πŸ‘¦πŸ‘¦
 
Wakaenda katika nchi ya Moab.umbali wa kama mile 30 au mwendo wa siku 7-10 kwa kutembea..🚢🚢🚢🚢 akiamini kupata chakula huko🍹🍞
 
Walikaa huko na Elimeleki akafa.
Wale wanae wawili wakaoa wanawake wa Moab..Opra na Ruthu.πŸ’ƒπŸ’ƒ; wakaishi miaka 10 ya ndoa.
 
Baadae wale wana wa Naomi nao wakafa.πŸ’€
 
Akabaki  Naomi na wakweze.
 
Naomi akaamua kurudi KWAO Bethlehem maana alisikia Bwana ameutembelea mji kwa chakula(njaa imeisha)πŸ˜‹πŸŒ½πŸ‡πŸŽ.
Nacho kilikua kipindi cha mavuno.
 
 
FUNZO:
Elimeleki alikimbia mbali na Mungu(nchi ambapo Mungu aliwapa) kwa sababu ya njaa na badala ya kufanikiwa alikoenda aliishia kukutwa na mauti yeye na wanae..
Tunaona pia Abraham alikimbia njaa kufika Misri mkewe nusu wamuoe,Mungu akaingilia kati😳
Mwana mpotevu nae alikimbia nyumbani akidhan ataenda kufanikiwa zaidi huko mwishowe alirudi hom mikono mitupuπŸ€”

 Uweponi mwa Mungu ni mahali salama hata kama tunaona mambo ni magumu,,tuchikilie tu Bwana atakukumbuka tuuu..huko Moab hakuna jema😟

KWA UPANDE WA MAMA MJANE-NAOMI.
 
Wakweze Naomi walikubali Kwenda nae Bethlehem,ila Naomi aliwasihi sana wabaki maana walikua bado wadogo hivyo walipaswa waolewe nao wawe na familia zao.
Mkwewe mmoja(Opra) akakubalkubakiπŸ™‹
Lakini mkwewe wa Pili(Ruthu) akakataa..akataka Kwenda na Naomi.
 
NAOMI
Alikua mwanamke aliyemjua Mungu wake,aliyeishi kwa Upendo na wakweze na kuwajali na kuwatendea mema.
maana waliishi nae zaidi ya miaka kumi,na bado walitaka kuendelea kuishi naeπŸ‘
Hata ulipofika wakati wa kuachana nae ikawa ngumu.
 
 
FUNZO:
Mwanamke anayemcha Mungu hutachoka kuishi nae.
Kwa kuwa Moyo wake wakati wote umejaa upendo na ukarimu.

Friday, January 22, 2021

JE,UTAKUBALI SHAMBA LAKO LIKAPANDWA MAGUGU KWA SABABU YA USINGIZI?

 


..lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

MT. 13:25 SUV



Usikubali shamba lako lipandwe magugu na adui kwa sababu ya usingizi.

Usingizi upo wa aina mbili

Wa kiroho na wa kimwili.


Wa kiroho ni pale ambapo unaacha kuwa rohoni yaan unaacha kuomba,kusoma neno,kutenda matendo mema,na kuliishi Neno la Mungu.


Hapo adui shetani kupitia mawakala wake anapata mlango wa kuingia kwenye himaya yako na kupanda magugu(uharibifu).

Yaan anapanda mbegu(wazo) ambalo huenda usijue kama ni gugu ukadhani ni ngano.


Na kwa vile umelala huwezi gundua.


Vyote vinakua na siku moja inagundulika haikuwa ngano lilikua gugu😱


Kila mtu anashangaa kulikoni huyu ndugu kafanya hivi au vile,

Kumbe ni gugu la muda mrefu lilipandwa bila mtu kujua kwa sababu alikua amelala.


Amka mpendaa tuwe macho rohoni kupitia maombi,kusoma neno kila siku,na kulitafakari ili kujilinda na adui anayesubiri tu tusinzie kidogo apandikize mbegu ya gugu ndani yetu.



Umebarikiwa!

Friday, January 15, 2021

OMBI LA LEO:MUNGU AMSHA ROHO ZA WATU WALIOKUSUDIWA KUSABABISHA KUTIMIA KWA NENO LAKO MAISHANI MWANGU MWAKA HUU 2021


 1.Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 


 5. Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.

EZR. 1:1‭, ‬5 SUV


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻

Omba Mungu aamshe roho za watu ambao wamekusudiwa kutumiwa nae kutimiza Neno lake maishani mwako



Ili kupenya maishani inahitajika watu Mungu aamshe roho zao watumike kukubariki,

Watumike kukuvusha mahali,

Watumike kukusemea mahali upate kibali,

Watu waamshwe roho zao watoe pesa zao,muda wao, mawazo yao kwako ili uvuke kwenda hatua nyingine ya maisha.


Ili kusudi la Mungu kwako 2021 litimie unahitaji watu.


*Na hao watu ni mpaka Mungu awe ameamsha roho zao kutenda kwako,* hawawezi kutenda tu hivi hivi.


Ombi letu leo,

Ee Mungu wangu amsha roho za watu waliokusudiwa kutenda kwangu ili Neno lako kwa mwaka huu 2021 litimie kwangu.


Hii ni kanuni mojawapo ya kiroho ya kusababisha mambo kutokea katika eneo/jambo lako lolote.

Omba Mungu aamshe roho za waliokusudiwa kukusaidia uvuke hapo ulipo.


Umebarikiwa!

UMESHAANDIKA MALENGO YAKO YA 2021?

Shalom Msomaji wangu.

Pokea salamu za mwaka mpya 2021!



Naamini kila mmoja wetu ameshaandika malengo yake ya 2021.

-kiroho

-kiuchumi

-kimaendeleo/uwekezaji

-kitaaluma/career

-kibiashara

-kiafya

-kihuduma


Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

Mithali 16:1 NEN


Wengi wanaishia kuwaza tu.

Ni vizuri *kuandika*


Na kuyaweka mahali ambapo utakua unayaona mara kwa mara.


_Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi: *“Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma.*_

Habakuki 2:2 BHN


Unaweza kuandika na kuyabandika mahali ambapo utakua unayaona kila siku.

Ili ukumbuke kutafanya isifike june ukawa umeshasahau na umeendelea na mambo mengine ambayo hayakuwa kwenye malengo yako.


Au kwenye diary ambayo unaitumia kila wakati ili ufunguapo uwe *unayaona*



*Kwa nini uandike?*

1.Itakua kufocus kwenye kile ulichopanga na hutatoka nje ya mstari.

2.utakumbuka na hutakua na kisingizio kwamba ulisahau.

3.ili uwe unajipongeza kila unapotimiza lengo mojawapo ya uliloandika.


Kuna watu hapa wanaandika malengo ya makampuni wanayofanyia kazi na mpango mkakati wa kuyatimiza lakini hajiandikii ye mwenyewe malengo yake ya mwaka na hana mpango mkakati binafsi.

Kama kampuni ingekua genius ingeandika kichwani isingeweka kwenye maandishi.😜

Ndio maana mwaka ukiisha ukimuuliza mtu ulifanya nini mwaka huu anakwambia hata sioni..zaidi ya kula tu asubui mchana jioniπŸ˜ƒ


Au akienda sana atakutajia kitu kimoja au viwili tu.

Kweli miez 12 umepewa na Mungu kufanya kitu kimoja au viwili tu! Si ni utumiaji mbaya wa muda huo?

Hayo yanatokea kwa sababu malengo hayaandikwi.

Na yakiandikwa notebook inawekwa kabatini kujaa vumbi.


Hayatengenezewi mkakati wa namna ya kufanyika,hivyo hayawez kutokea tu..lazima yasababishwe kutokea.


Mwaka 2021 TUAZIMIE KUWA NA MALENGO YA KUELEWEKA NA TUWE NA MPANGO MKAKATI WA KUYATIMIZA.


 Unaweza kutumia mchanganuo kama nlioweka mwanzo au ukaongezea vingine kulingana na wewe mwenyewe.


Hii ndio siri mojawapo ya waliofanikiwa!


Uwe na siku njema!

Thursday, June 11, 2020

MTIRIRIKO SAHIHI NI HUU.


SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 4


✍🏾Mungu husikia maombi na kutufanyia nafasi wakati wa shida.
Unapokua kwenye shida ina maana umebanwa mahali,ndio maana Daudi anamwomba Mungu amfanyie nafasi katika kipindi cha shida na Mungu anamsikia.
.
πŸ“ŒUKIWA NA SHIDA JAMBO LA KWANZA LIWE KUMWOMBA MUNGU NA SIO KUTAFUTA MSAADA KWA WANADAMU.
.
πŸ“ŒMARA NYINGI TUKIPATWA NA SHIDA TUNAWAZA NIMPIGIE NANI SIMU AU NIMWAMBIE NANI ANIKOPESHEπŸ€”
.
πŸ“ŒMsaada wa Kwanza na wa Haraka ni Mungu.MUNGU YUKO NASI WAKATI WOTE MAHALI POPOTE.
.
YEYE ANAWEZA KUTATUA SHIDA AMBAZO HATA MWANADAMU HAWEZI.
.
NA BAADA YA KUMWOMBA NDIPO ATAKUONGOZA NANI WA KUMTAFUTA ALIYEBEBA MAJIBU YAKO,MAANA SI KILA MTU ANA JIBU LA SHIDA YAKO.

Mstari 8
Hii ni dozi nzuri sana kila siku kabla ya kulala
.
✍🏾 ikariri na uwe unaisema kama sehemu ya sala yako ya kulala na utaona jinsi utalala kwa Amani.
.
πŸ“ŒWATU WENGI IKIFIKA USIKU WANAOGOPA KULALA.
NA HASA KAMA ANALALA KWENYE NYUMBA PEKE YAKE.
.
LAKINI UKIZOEA KUOMBA HUU MSTARI WA NNE UTAGUNDUA KWAMBA;
.
πŸ“ŒMUNGU HUTUPA AMANI NA USINGIZI MAANA NDIYE ATUPAYE USALAMA.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 15 0ZA ZABURI - ZABURI 3


✍🏾 (Mstari1-3)Lazima ujue kuwa UNAO MAADUI(Watesi),na sio maadui tu,bali MAADUI WENGI.
Na wanajisemea "tumwone,anajidai na Mungu,tuone kama Mungu atamsaidia"
.
πŸ“ŒLakini,lazima umjue Mungu wako.
YEYE ni NGAO yako pande zote.
YEYE ni UTUKUFU wako,
YEYE ni MWINUA KICHWA chako
.
πŸ“Œthats all you NEED,,
.
πŸ‘‰πŸ»Uhakika wa ulinzi wa Mungu(NGAO) dhidi ya adui zako,
.
Uhakika wa Uwepo wa Mungu(UTUKUFU) kwako adui wanapokujia
.
Uhakika wa Ushindi(MWINUA KICHWA) dhidi ya adui.


Mstari 4
πŸ“ŒMaombi ni mawasiliano kati yako na Mungu.
Sio maongezi ya MTU MMOJA, ni ya WAWILI
.
πŸ‘‰πŸ»LAZIMA KUWE NA MREJESHO
.
πŸ“ŒUKIONA UNAOMBA TU WEWEEEE HALAFU HUSIKII JIBU,,IKO SHIDA MAHALI,JIFANYIE TATHMINI.
.
Mstari 6-8
πŸ“ŒUSIOGOPE WINGI WA ADUI KWANI BWANA AMEKWISHA WAPIGA KIBAO CHA SHAVU NA KUWAVUNJA MENOπŸ˜‚
(Ndivyo Biblia inasema)
.
πŸ‘‰πŸ»Adui yako asikuogopeshe kwani tayari ni KIBOGOYOπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
.
Sijui kama unaelewa hii
.
πŸ‘‡πŸ½
.
Hivi KIBOGOYO anaweza kuongea kweli? Sasa Maneno ya adui yanakutisha nini wakati hayasikiki hata vizuri🀷🏻‍♀️
.
πŸ“Œ USITISHWE NA MANENO YA ADUI YAKO
.
WEWE MTAZAMAE BWANA.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 2


✍🏾Mawazo yasiyopendeza juu ya Mungu na watumishi wake, Mungu hapendi
.
✍🏾Pale ambapo mtu au watu wanajipanga kuwa kinyume na mtumishi wa Mungu ni sawa na kuwa kinyume na Mungu mwenyewe
.
✍🏾Na mtu anapowaza uovu huo, mbinguni Mungu ANAMCHEKA na kumeangalia kwa DHARAU
.
πŸ“Œ Ndipo hasira yake inapowaka juu ya mtu huyo
.
πŸ“ŒUNAJIULIZA,mbona hiki hakiendi au kile hakiendi,,
.
JICHUNGUZE,je,umewahi kumwazia mabaya mtumishi wa Mungu na Mungu mwenyewe? Basi hasira yake imewaka juu yako! TUBU LEO.
.
πŸ“ŒJIZOEZE kuwaombea wale wanaofanya kazi ya Mungu badala ya kuwasema vibaya, hata kama walichofanya ni kibaya, SIO KAZI YAKO wewe kuanza kuwasema vibaya.
.
πŸ“ŒACHA MUNGU MWENYEWE atashughulika nao,
.
πŸ“ŒUSIJITAFUTIE LAANA ZISIZO NA ULAZIMA NA ZINAZOEPUKIKA.


✍🏾mstari wa 8.
UNIOMBE, NAMI NITAKUPA MATAIFA KWA URITHI WAKO.NA MIISHO YA DUNIA KUWA MILKI YAKO.
.
πŸ“ŒMUNGU mwenyewe anatupa prayer point..
MUNGU anataka uone kwa mtazamo wa kidunia sio wa kimtaa unachoishi.
.
UNAPOOMBA, kuwa na Global Vision.
(Wanasema Think Global but Start Local) .
LAZIMA MTAZAMO WAKO UWE WA MATAIFA,UWE WA MIISHO YA DUNIA,,ILI maombi yako yawe pia ya aina hiyo..inaanzia kwenye mindset.
.
πŸ“ŒJe,UNA MAONO GANI?KUJUSU KAZI YAKO,BIASHARA YAKO,HUDUMA YAKO?
.
JE,YANAISHIA MTAANI KWAKO,MKOANI KWAKO,NCHINI KWAKO,AU DUNIANI KOTE?
.
πŸ‘€ Macho yako yafunguke leo uone jinsi Mungu anavyokuona..yeye anakuona kama a GLOBAL PERSONALITY.
SO SHOULD YOUR PRAYERS BE.
.
#umebarikiwa
#siku150zazaburi

SIKU 150 ZA ZABURI - ZABURI 1

Heri(Amebarikiwa)mtu yule;
1.Asiyekwenda(asiyetembea) katika shauri (majadiliano/maamuzi) ya wasio haki.
2. Hakisimama katika njia ya wakosaji
3.Hakuketi barazani na wanaofanya mizaha.

πŸ“ŒBadala yake mtu huyu,
1.Anafurahishwa na Neno la Mungu.
2.Analitafakari wakati wote(usiku na mchana) .

πŸ‘‰πŸ»Matokeo yake:
1.Atakua kama mti ukiopandwa kando ya maji,na kuzaa matunda yake kwa wakati.
2.Jani lake halitanyauka.
3.KILA alitendalo litafanikiwa.

πŸ‘‰πŸ»SIRI YA KUFANIKIWA NA KUSTAWI KWENYE KILA ENEO MAISHANI IKO HAPA.

 πŸ‘‰πŸ»KWANZA,,KUTAFAKARI NENO LA MUNGU WAKATI WOTE.
SIO KUSOMA TU,BALI NA KUTAFAKARI.
KUNA TOFAUTI HAPO
 πŸ‘‰πŸ»PILI,KUIPENDA SHERIA YA BWANA..YAANI KULIPENDA NENO LA MUNGU.
Kuna watu wanasoma Neno kwa sababu tu wanalazimishwa,au na wazazi au kanisa lake au mazingira aliyopo.

πŸ‘‰πŸ»LAKINI SIRI MOJAWAPO YA KUFANIKIWA IPO KWENYE KULIPENDA NENO LA MUNGU.
YAANI ULIPENDE TU.
UPENDEZWE NALO.

UKILIPENDA INA MAANA,
πŸ“ŒUTATAKA KULISIKIA KILA SAA
πŸ“ŒHUTACHOKA KULISOMA
πŸ“ŒUTATAKA KULIJUA ZAIDI

Na hizi ndio siri kubwa za kufanikiwa kiMungu,maana Neno lina siri zote unahitaji kuweza kuishi hapa duniani kwa ushindi.

JIZOEZI KULIPENDA NA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU KILA SIKU.


#Umebarikiwa!
#siku150zazaburi

Sunday, June 7, 2020

JE WAJUA?

MAAMUZI YAKO YA JANA NDIO MATOKEO YAKO YA LEO, NA MAAMUZI YAKO YA LEO NDIO YATAKUWA MATOKEO YAKO YA KESHO.

AMUA VEMA LEO ILI UWE NA KESHO NZURI.

USIBAKI KULALAMIKA TU AU KULALAMIKIA WATU KWA SABABU WALIKUAMULIA MAMBO FULANI NA YAMELETA MADHARA KWENYE MAISHA YAKO

AMUA LEO KUFANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO YA KESHO.

USISUBIRI MTU AJE AKUAMULIE,
AU SERIKALI NDIO IKUSAIDIE KUAMUA KESHO UWEJE.

WEWE NDIO UNA UAMUZI WA UNATAKA KESHO YAKO IWEJE.

 

WEWE NDIO UNAAMUA KESHO UWE MTU WA AINA GANI
WEWE NDIO UNAAMUA KESHO UISHI WAPI
WEWE NDIO UNAAMUA,

NA USIPOAMUA WEWE UTAAMULIWA NA WATU WENGINE,

LAKINI LAZIMA MAAMUZI YAFANYIKE,NDIO MAMBO YATOKEE.



#DontBlamethepastbookreview
#bookreview
#author

LEAVING A LEGACY!

We are so used to see even receive a legacy from those who went ahead of us particularly of material things such as houses,cars,plots and education.

But this will only stay for few years and with few individuals.




 


Very few precious people think beyond that.
A legacy that will surely live eternally.
A legacy that generations after you will treasure.

I was just wondering if I leave a house and riches for my children and my children's children that will be so selfish!
Although it is so important to do so as the Bible instructs us to do so.


But we can do more than that.

We ought to leave a legacy of Glory!


You are Blessed!

JE,UNAJIONA DHAIFU NA MASIKINI?

IJAPOKUWA UNAJIONA DHAIFU NA MASIKINI, MUNGU ANAKUONA HODARI NA UNAYEWEZA KUISHINDA VITA.

Hata Gidioni,alikua kijana aliyejiona hivyo pale alipotokewa na malaika.
Waamuzi 6:1-6 inaeleza wasifu wa kijana huyu

Alijiona masikini
Alijioni mdhaifu sana
Alijiona haiwezi vita iliyokua mbele yake.

Lakini Mungu hakumwona kwa staili hiyo.

MUNGU ALIMWONA NI HODARI NA SHUJAA AWEZAE KUIPIGANA VITA NA KUISHIDA.

 


HATA WEWE LEO HII,
USIJIONE MDHAIFU,
USIJIONE MASIKINI,

JIONE KAMA MUNGU ANAVYOKUONA!

ANAKUONA HODARI,
ANAKUONA UNAWEZA,
ANAKUONA MSHINDI,

NA NDIVYO ULIVYO.

USIYUMBISHWE NA HALI ULIYONAYO SASA,

HATA WANAJESHI WAKIANGALIA IDADI YA ADUI HAWATAPIGANA VITA,

HIVYO UANGALIE UKUU WA MUNGU
NA UTAISHINDA VITA.

UWE NA MWEZI WENYE USHINDI TELE!

#author
#kalamuyangu✍


Friday, September 27, 2019

Enyi mataifa yote,msifuni Bwana,

Zab 117:1-2
"Halleluya 
Enyi mataifa yote,msifuni Bwana,
Enyi watu wote mhimidini,
Maana fafhili zake kwetu sisi ni kuu,Na uaminifu wa Bwana ni wa milele." 

Watu wote wa kabila zote na aina zote wanaitwa KUMSIFU na KUMHIMIDI Bwana.

Watu wote bila kujali kabila,dini,itikadi,uraia,tabia wala rangi!

Yaan ile kwamba ni MTU unaitwa na kuwajibika kumsifu na kumhimidi Mungu.

Kwanini?

Kwa sababu FADHILI na UAMINIFU wake ni wa milele.. Mwanadamu anaweza akakufadhili kwa muda tu,kwa wakati Fulani tu,lakini Mungu haangalii mvua wala jua,haangalii umeamkaje au utamlipa nini yeye FADHILI zake ni za siku zote(milele)

Mwanadamu anaweza kuwa mwaminifu kwa wakati tu,au kwa muda tu,,lakini Mungu UAMINIFU wake ni wa milele.. Hata unapokua sio mwaminifu yeye badooo anabaki kuwa mwaminifu!

Ndio maana mtunga zaburi anamwita KILA MTU kutoka kila mahali ili TUMSIFU HUYU MUNGU AMBAE FADHILI ZAKE NA UAMINIFU WAKE NI WA MILELE YOTE.

Wednesday, January 30, 2019

#HAUFANANISHWI

 
Ukiwa na mtoto wako ambae hamjawahi kuonana kwa sura lakini huwa mnaongea kwenye simu,na huwa unamwambia ulivyo.
Huwa anakusoma maana ulimpa kitabu ili akusome ajue ulivyo.
Na kila wakati akikuuliza unafanana na nani?nini?
Unamwambia #Haufananishwi!
Na unamwambia asiweke chochote kama mfano wako maana haufanani nacho kabisa.
Anajaribu kuchukua ng'ombe akizani utakua unafanana nae,
Ila unamwambia #Haufananishwi
Anaendelea na kuangalia labda ni jua au mlima mkubwa lakini unamwbia hapana! #Haufananishwi
Au unajaribu kuhisi atafanana na Mali au pesa lakini anakwambia hivyo vyote navimiliki na siwez kufanana navyo.
Au sanamu ya mzungu mwenye nywele ndefu na ndevu labda ndio mfanano wako ila unamwambia Haufananishwi!! Unaendelea kumwambia kuwa #Haufananishwi kamweeee!
#Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristu ni mkuu sana.
YEYE NI BABA YETU NA SISI NI WATOTO WAKE.
YEYE ALIUMBA KILA KIUMBE TUKIONACHO,KILA KITU KILICHOPO YEYE AMETENGENEZA.
ANAWEZAJE KUFANANA NAVYO?
Aliyetengeneza simu anaweza kufanana na simu?? Au use me fundi anafanana na nguo?? Au mjenzi anafanana na matofali??? Haiwezekani!
Mungu hafananishwi na chochote.
#HAFANANISHWI
#HAFANANISHWI
#HAFANANISHWI KAMWE!

Friday, September 14, 2018

Nini kinaendesha maisha yako?


Wengine, ni Hatia.

Mtu anaishi chini ya hatia kwa sababu ya mambo aliyofanya nyuma au aliwahi kufanyiwa!


Anaishi akiwa na majuto na aibu ya Yale yaliyotokea zamani!
Anaruhusu jana yake kuitawala Leo yake na kumfanya asione mwanga wa kesho!

Anajiadhibu mwenyewe na kuteka mafanikio yake mwenyewe,

Ni kweli tu matokeo ya jana zetu,lakini sio ticket ya kuwa mfungwa wa jana yako!
Kusudi la Mungu kwako halifungwi na jana yako,




#Alimgeuza muuaji Musa kuwa kiongozi mzuri wa Waisraeli,

#Alimgeuza Gideoni mnyonge,kuwa mtu hodari na mkuu.

Mungu amebobea kwenye kuwapa watu mianzo mipya(mwanzo mpya)

Yeye ni mtaalamu kwenye hilo eneo!

Unamkumbuka Sauli kwenye agano jipya,
Kama kuna mtu asingefaa kabisa alikua ni yeye,, Ila Mungu alimgeuza kuwa mtumishi wake mkubwa sana,,na Leo hii tunasoma kitabu cha Agano Jipya ambacho sehemu kubwa ya zile barua aliziandika yeye! 

Unadhani kesi ya imeshindikana??? Hapana!

Mruhusu Mungu akuoneshe sababu ya yeye kukuweka hapa duniani,usiishi tena chini ya hatia bali uishi maisha yanayoongozwa na kusudi la Mungu.

@minna_book_club_tz
@minna_blessed
# TunaendeleaKusoma
#ReadingMarathon
#JoinTheClub
#YouAreNotLateForSeptemberReading

MINNA BOOK CLUB BRINGS YOU....

Tayari Mungu alishapanga uzaliwe lini,uzaliwe wapi,na hata wazazi gani uzaliwe kwao.

Inawezekana kwa wazazi wao waliona umezaliwa nje ya ratiba yao,ila kwa Mungu huo ndio ulikua muda sahihi kabisa wa wewe kuzaliwa!

#UmeumbwaKwaKusudi
#Karibu tusome pamoja

NI HATARI SANA!

Ni hatari sana huo mwavuli wa juu kabisa unapokua haupo,,pale husband anapokua wa mwisho anakua kwenye hatari kubwa sana,

Ni hatari sana kama hiyo miamvuli miwili ya juu haipo,,wife anakua danger zone,, Na ni hatari zaidi kama hiyo miavuli mitatu ya juu haipo,child anakua kwenye hatari isiyoelezeka!

Familia yoyote isiyo na Mwavuli wa Kristo ipo hatarini kupatwa na lolote maana haijafunikwa na haiko salama.


Unaweza kudhania pesa zitakulinda,

Unaweza kudhania ukiwa na nyumba,magari na dhahabu nyingi zitakulinda,

Unaweza kudhania jina kubwa na kujulikana kila mahali ni ulinzi kwako,

Ila waulize,
Waliokuwa na pesa na shida ilipokuja ikazishinda-kuna vitu pesa haina majiibu yake

Waulize waliokuwa na majumba,magari na dhahabu,,kuna shida ziliwavamia hata hizi asset hazikua na msaada kwao,

Waulize watu maarufu,,watakwambia kuna saa hata majina yao hayana msaada kwao,walotafuat nani anawajua,na hakukua hata na mmoja wao aliyejitokeza!

Funikwa na mwavuli wa Yesu Kristo utakua salama muda wote!
#Ije mvua lije jua,huna mashaka kwa sababu uko salama!
#Zaburi91:1

@minna_blessed

Thursday, May 10, 2018

LIFE HAS NO DUPLICATE!

...Those are not my words, but as I read them this afternoon from one servant of God, they struck my mind and i had to read them twice.

She wrote:
"LIFE HAS NO DUPLICATE.LIVE IT TO THE FULLEST!LIKE YOURSELF. LOVE YOURSELF. LAUGH ALOT. HONOR GOD AND HELP PEOPLE" ~Rev. Funke-Felix Adejumo.



I got this revelation as I was reading, that many are times we take our lives for granted. we assume that we are here just to count days and that is all!


No, we are all here for a mission and a purpose. and yes, as we are born for a purpose we ought to be purposing all the time!

And as we purpose in life, lets do it cheerfully and with love. Because the greatest satisfaction in life is when what you do makes you happy, and you are happy doing it! If whatever you do does not make you happy you will never be satisfied! Here, i don't mean that if you take drugs and feel happy that's it! No!
I am talking about true happiness that has no regrets!

The bible is clear that the blessing of the Lord, makes one rich, and it has no sorrow mixed with it!

Provebs 10:22. "The blessing of the LORD makes a person rich, and he adds no sorrow with it."

If any happiness inside it has an ingredient of sorrow then that's not from the Lord. And its obvious from the evil one.

When i was a little girl i used to think that all the rich people are happy! and i thought that the poor people and not happy.

But that was because I was a child.

Little did I know that most rich people have happiness poverty! 

Yes, many rich people that have material things, are do not live a happy life. This is all because what is holding their happiness is not God.

As we read previously, that it is only the blessing of the Lord that makes one rich with no sorrow. Any other source,mixes the blessing with sorrow! No wonder we have unhappy rich people around.

Life is no a duplicate.When we live today, its gone, tomorrow is another day. when whatever prepared for today passes, its gone. Even if tomorrow it seems to be the same, but it is different!

So, live your life to its fullest because there is no duplicate for a day! Every day has its own package!

Enjoy life today!

~Minna Matee

Wednesday, July 19, 2017

#Majira kwenye maisha: (kwa ufupi tu)


Kuna majira makuu manne kwenye maisha.
1.Asubuhi ya maisha yako
2. Mchana ya maisha yako
3.Jion ya maisha yako.
4. Usiku wa maisha yako.

1. Asubuhi.
Asubui ni kipindi toka kuzaliwa mpaka kumaliza elimu yako na kuanza kujitegemea au kujisimamia mwenyewe.
unaweza ukawa na asubuhi nzuri sana au mbaya sana. lakini hiyo haizuii wewe kuwa na mchana mzuri.
Hapa wengine husahau kuwa asubuhi huwa inapita haraka sana na kuzembea au kupuuzia maelekezo wanayopewa na walioko mchana na jioni!

2. Mchana
Ni kipindi cha kufanyia kazi maarifa yote uliyoyapata asubui, ie kutoka kwa wazazi, kutoka shuleni, kutoka kwenye maeneo mbalimbali uliyojifunza.
Ni kipindi cha kujenga maisha yako huku ukijua siku moja jua litachwea, na itakua jioni.
Hapa vijana wengi hujisahau na kudhani siku zote itabaki kuwa mchana, hivyo jioni huwajia kwa kushtukiza.
Wapo wanaoitumia mchana yao vizuri na kuwa na uhakika na jioni njema sana.

3.Jioni
Hiki huwa ni kipindi cha kufaidi matunda ya kazi uliyoifanya mchana.
Huwa sio kipindi cha kufanya kazi, ila kama ulizembea na kuzubaa mchana, unaikuta inakulazimu kufanya shughuli ambazo ulipaswa uwe umezifanya ilipokua mchana wako
Hiki ni kipindi cha kujiandaa na usiku. maana usku huwa hauchelewi sana ikishafika jioni.
Chochote ulichokipanda mchana, hapa jioni ndio unakivuna sasa! na kinakua dhahiri kiasi kwamba hata walioko mchana wanaona.

4. Usiku
Hiki ni kipindi cha kujiandaa kupumzika. maana sasa ni usiku. huwezi tena kufanya kazi. giza limeingia.
hapa sasa kama ulitumia mchana na jioni yako vizuri, usiku wako utakua na mwanga, hivyo hutakaa gizani.
ila kama uliutumia vibaya, usiku wako utaishia kuwa gizani na hakuna atakayejua kama upo maana hutaonekana, ni usikuu!

Nimeeleza kwa ufupi sana.Nadhani utakua umeelewa na kujua wewe uko majira gani.

na kama unatumia majira yako vizuri huku ukijua kuwa hayo majira kuna siku yatapita utaingia majira mengine na hutaweza kufanya tena yale ya majira ya nyuma!

Usipoteze muda! Tumia muda wako vizuri. Majira hayagandi.
Ubarikiwe sana!
~Minna Matee

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...