Ni kweli uliowazi kwamba hakuna jambo jipya chini ya jua!
Lakini pia pamoja na kwamba hakuna jambo jipya ila utofauti upo kwenye nani analifanya jambo hilo na anaona nini kwenye hilo analolifanya!
...Wote mnaweza kuwa mnafanya biashara moja ya chakula kwa mfano, lakini kitakacho wa tofautisha ni mnaona nini kwenye hiyo biashara.
Kiwango cha kuona kwao wewe ndicho kitakachokutofautisha kwenye hicho unachokifanya!
Isikupe shida wote mnauza nguo, au wote mna toa huduma zinazofanana, kinachojalisha ni utofauti wa uonaji wenu!
...Unaona nini kwenye kile unacho kufanya?
Anza kuona kwa mtazamo wa tofauti kwenye kile unachokifanya na utaanza kuona mabadiliko makubwa!
Kile unachokiona ndicho kitaamua umbali utakaofika kwenye hicho unachofanya/biashara/kazi unayofanya!
Unaweza kuwa unafanya jambo la kawaida sana, lakini je unaliona likifika wapi?
Wewe ni fundi cherehani labda, umeshawahi kujiona ukimshonea raisi nguo?
…Au wewe ni mpishi wa chakula, ulishawahi kuona ukipika kwenye hafla kubwa za kimataifa? Au unajiona tu hapo hapo kibarazani/ kimgahawani?
Wewe ni dereva, ulishawahi kuona ukimwendesha raisi? Au unajiona ukibaki hapo hapo kuendesha abiria kutoka kariakoo kwenda mbagala?
….Sio kazi mbaya lakini unachokiona ndicho kitategemea mwendo wako na bidii yako kwenye hicho unachokifanya!
Siku zote utofauti wa kile unachofanya wewe na anachofanya mwenzako hata kama vinafanana ni unachoona kwenye unachofanya!
Mwendo wako na bidii ya kufanya inategemea sana unaona nini!
…haijalishi unachokifanya, inajalisha unaona nini kwenye kile unachokifanya!
Kupata jumbe kama hizi kwa whatsapp tuma neno JUMBE kwenda 0679300845
#Kuza kuona kwako, na unachokifanya kitafika mbali!