Thursday, June 4, 2015

UJANA MAJI YA MOTO, HUWA YANAPOA!


Vijana wengi huwa wanadhani watabaki vijana siku zote!
Ujana huwa ni hatua tu katika maisha ya mwanadamu ambayo huwa mtu hupitia akitokea utoto kwenda utu uzima!
Vijana wengi hujisahau na kudhani watabaki kuwa vijana milele!!!...

Usijisahau kijana,


 UJANA NI MAJI YA MOTO, HUWA YANAPOA!






Siku moja utavuka hatua ya ujana na kuwa mtu mzima.
Wakati wa ujana ni wakati wa kujijenga kwa kujiwekeza na maarifa yatakayokusaidia utu uzimani, kujijenga kwa kuwekeza kiuchumi kutakakokusaidia utu uzimani, ni wakati wa kuwekeza kimahusiano kutakakokusaidia utu uzimani,
ni wakati wa KUWEKEZA!

WEKEZA UJANANI, UVUNE UTU UZIMANI!

SIO wakati wa kujibomoa kwa kampani mbaya, SIO wakati wa kujibomoa kwa kubadili kila sampuli ya wanawake/wanaume, SIO wakati wa kujaribu kila kipitacho mbele yako kama madawa ya kulevya na sigara.

Ujana wako ni kielelezo tosha cha kujua utu uzima wako utakuwaje!

 Hujawahi kusikia mtu anasema, ningerudi kuwa kijana ningefanya mambo makubwa sana?
Huyo alipoteza muda wakati wa ujana, na sasa anajutia utu uzimani!


Usipoteze Muda kijana, Wekeza wakati wa ujana kujifunza maarifa katika maeneo mbalimbali ya maisha, na utu uzimani utavuna matunda ya kuwekeza kwako!

Soma vitabu, jifunze mambo mbali mbali, hudhuria mikutano na semina mbalimbali, jiongeze kielimu, fanya chochote, ili mradi Ujiwekeze, baada ya kuvuka hatua ya Ujana utaona matunda mema!

Acha vijana wakucheke wakuona mshamba, lakini unajua unachofanya!
Anza kufungua macho yako na kujiona miaka 20 mbele, unataka kuwaje,halafu anza kutengeneza mazingira ya kufika hapo.

Penda kutafakari Neno la Mungu kila siku, litakupa mwongozo wa maisha, na kujua cha kufanya na cha kuacha!

Kwa kufanya haya machache, nakuhakikishia Ujana wenye Ushindi!
‪#‎UjanaMajiYaMotoHuwaYanapoa‬#‪#‎KijanaJitambua‬#

~Mwl Minna

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...