Monday, June 8, 2015

FANYA DIET YA MOYO!


Siku hizi kuna wimbi kubwa la wadada kutaka kupunguza uzito..na imekua fashion wadada kufanya diet ili kupunguza uzito wa mwili.
Yameingia madawa ya kila aina yanayopunguza uzito....
Zimeanza madarasa spesho kwa ajili ya lishe ya namna ya kupunguza uzito.

Kasi ya kufanya mazoezi ya mwili imeongezeka na kuwapa waona fursa nafasi ya kufungua biashara ya kufanyisha watu mazoezi!
Lakini kuna mahali tumesahau kupafanyia Diet.
Napo ni Moyoni
.

Umewahi kujiuliza moyo wako una kilo ngapi?
Na wingi wa kilo hizo umetokana na kubeba nini?
Mioyo ya wengi imebeba vitu visivyosahihi na kimoja wapo kikubwa ni watu wasio sahihi.
Watu wengi wamebeba watu mioyoni waliowaumiza kwa miaka mingi,Pengine kwa kujua au kwa kutokujua kwao.
Matokeo yake uzito wa moyo umelemewa!

Magonjwa mengi ya moyo,hutokana na uzito ulioko moyoni uliotokana na watu uliowabeba na kuwalundika moyoni kwa sababu tuuu walikutendea mambo ambayo hukutarajia na yakakuumiza.
Uliachwa miaka mingi na boyfriend/girlfriend lakini mpaka leo bado hujamsamehe, ulitapeliwa kwnye biashara miaka.mingi lakini mpaka leo bado umembeba tu huyo mtu,ulipewa ahadi akirudi tu atakuoa,akarudi kashaoa,lakini mpaka leo umembeba tu moyoni,mwenzio hana hata habari anasonga mbele na maisha wewe bado unawaza tu kwa nini alinifanyia vile..leo fanya diet ya moyo!mtoe huko..
hata kama ni mzazi alikufanyia mambo mabaya,leo amua kufanya diet ya moyo umtoe uone ambavyo baraka zitakufuata.

Usisahau kuwa unaishi na wanadamu na sio malaika.
Leo amua kufanya diet ya Moyo.

 Watoe watu wote uliowaweka na wakaongeza uzito wa moyo wako.
Biblia inasema tuchukuliane na kusameheana,na hata kama ipo sababu ya kumlaumu aliyekukosea wewe msamehe kama na wewe ulivyosamehewa.(wakolosai3:13)
Umewahi kujiuliza Mungu angekua anaweka waliomkosea moyoni ingekuwaje?
Sasa kama Mungu ameamua kutusamehe sisi,wewe ni nani uendelee kumshikilia mtu? na kuuongezea moyo wako uzito?

Kwa taarifa yako,amayeumiaga zaidi ni yule anayetakiwa kusamehe na sio anayetakiwa kusamehewa!
Leo fanya Diet ya Moyo.

Punguza Idadi ya watu uliowabeba ili moyo wako uwe na afya njema.
Moyo uliochangamka ni DAWA nzuri.Mith17:22
Wakati mwingine huhitaji dawa ya hospital kwa magonkwa yako, fanya tu Diet ya Moyo,utapona!
Fanya diet ya moyo leo uupunguzie moyo wako hatari ya kuvamiwa na jambazi presha huko baadae.
#‎TeamDietYaMoyo‬#‪#‎OperationPunguzaUzitoWaMoyo‬#

~Mwl Minna.

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...