Monday, November 2, 2015

Unapoanza kuona Majitu,,jua unakarikibia kuingia Kanani!!






Kama bado hujaanza kuona majitu, bado una safari ndefu..kwa sababu majitu yako Kanani sio jangwani!!

Unapoyaona sasa, usijione kama panzi mbele yao, kwa sababu ndivyo watakavyokuona pia!!!

Majitu yasikutishe,,kwa sababu uliye naye ana nguvu kuliko hayo majitu!!

Usisahau kuwa Kanani kuna Maziwa na Asali,,sio majitu tuuu!!!

Hayo majitu ni ya muda tu, na unapaswa kuyaangamiza, na umepewa uwezo wa kuyaangamiza, ili upate hayo Maziwa na Asali ya Kaanani!!!

‪#‎NenoLaMunguTamuuu‬#

~Mwl Minna

Tuesday, June 23, 2015

#‎Kufunuliwa‬ Siri, Hukuvusha Kiwango Kingine#



 Daniel 2.

 Daniel na wenzie walitaka kuchanganywa na wale wachawi wa Babiloni wauwawe kwa pamoja, kwa sababu wale wachawi walishindwa kujiua ndoto ya Mfalme na tafsiri yake!
Daniel na wenzake WAKAMWOMBA MUNGU mfumbua mafumbo, awafunulie ile ndoto na kuwapa tafsiri yake!


 Mungu akamfunulia Daniel ile ndoto na tafsiri yake usiku katika njozi....
Daniel akaenda kwa mfalme na kumwambia A-Z ya alichokitoa na tafsiri yake!


Baada ya hapo, Daniel na wenzake wakapelekwa kiwango kingine, wakapewa nafasi kubwa katika serikali ya Babeli.

Kuna siri nyingi sana ambazo unatakiwa kuzijua kwa habari ya maisha yako,kazi yako,ndoa yako, biashara yako, masomo yako n.k na ni Mungu peke yake ndiye azijuaye na ndiye awezaye kuziweka wazi kwako.

Na ni kwa njia moja tu tunaweza kuzijua siri hizo- KUMWOMBA Mungu azifunue kwako.
Kuna siri usipozijua huwez kwenda kiwango kingine!

 Daniel asingefunuliwa ile ndoto asingepandishwa cheo.

Mwombe Mungu leo akufunulie siri unazopaswa kuzijua, ili kuvuka kwenda viwango vingine!

 

Monday, June 8, 2015

MOYO WA SHUKURANI

Kitendo tu cha kupumua bila kugombania hewa kinanitosha kumshukuru Mungu,nikitafakari kuwa kuna mwenzangu kawekewa mtungi wa kumsaidia kupumua..
Mimi sio kwamba nina mapafu mazuri sana ndio maana naweza kupumua bila shida mpaka leo bali NI KWA NEEMA ZA MUNGU TU!


Kitendo tu cha kuweza kutembea kwa miguu yote miwili bila kusaidiwa na chochote kinanitosha kumshukuru Mungu.
Nikikumbuka kuna mwenzangu anahitaji kifaa kimsaidie aweze kusogea japo hatua moja,au hawezi kusogea kabisa...
kwa sababu ni mgonjwa au kilema..
Mimi sio kwamba natembeaga kwa uangalifu sanaa ndio maana mpaka leo nna miguu yangu miwili mizima ina nguvu ya kutembea bila usaidizi bali NI KWA NEEMA ZA MUNGU TU!


 Kitendo tu cha kuweza kujitambua kuwa nasikia njaa,nimeshiba,nasikia baridi au joto,nimevaa nguo au niko uchi,nataka kulala au kukaa ni sababu tosha ya kumshukuru Mungu.
Nikikumbuka kuna mwenzangu ana mtindio wa ubongo au ni taahira hajielewi ale au alale au avae nguo au atembee mtupu na anahitaji kusaidiwa kufanya hivyo..
Sio kwamba mimi namempa Mungu dollari ndio maana niko nilivyo najitambua na hisia zangu zinafanya kazi bali NI KWA NEEMA YA MUNGU TU!

 

Hayo ni baadhi ya mambo machache ambayo kila mmoja w
etu ana sababu ya kumshukuru Mungu kwayo,kila tumapoamka tuna sababu ya kumshukuru Mungu,haijalishi tunapitia nini lakini bado IPO sababu ya Msingi ya kumahukuru Mungu.

‪#‎MoyoWaShukurani‬#MoyoWaIbada#

~Mwl Minna.

FANYA DIET YA MOYO!


Siku hizi kuna wimbi kubwa la wadada kutaka kupunguza uzito..na imekua fashion wadada kufanya diet ili kupunguza uzito wa mwili.
Yameingia madawa ya kila aina yanayopunguza uzito....
Zimeanza madarasa spesho kwa ajili ya lishe ya namna ya kupunguza uzito.

Kasi ya kufanya mazoezi ya mwili imeongezeka na kuwapa waona fursa nafasi ya kufungua biashara ya kufanyisha watu mazoezi!
Lakini kuna mahali tumesahau kupafanyia Diet.
Napo ni Moyoni
.

Umewahi kujiuliza moyo wako una kilo ngapi?
Na wingi wa kilo hizo umetokana na kubeba nini?
Mioyo ya wengi imebeba vitu visivyosahihi na kimoja wapo kikubwa ni watu wasio sahihi.
Watu wengi wamebeba watu mioyoni waliowaumiza kwa miaka mingi,Pengine kwa kujua au kwa kutokujua kwao.
Matokeo yake uzito wa moyo umelemewa!

Magonjwa mengi ya moyo,hutokana na uzito ulioko moyoni uliotokana na watu uliowabeba na kuwalundika moyoni kwa sababu tuuu walikutendea mambo ambayo hukutarajia na yakakuumiza.
Uliachwa miaka mingi na boyfriend/girlfriend lakini mpaka leo bado hujamsamehe, ulitapeliwa kwnye biashara miaka.mingi lakini mpaka leo bado umembeba tu huyo mtu,ulipewa ahadi akirudi tu atakuoa,akarudi kashaoa,lakini mpaka leo umembeba tu moyoni,mwenzio hana hata habari anasonga mbele na maisha wewe bado unawaza tu kwa nini alinifanyia vile..leo fanya diet ya moyo!mtoe huko..
hata kama ni mzazi alikufanyia mambo mabaya,leo amua kufanya diet ya moyo umtoe uone ambavyo baraka zitakufuata.

Usisahau kuwa unaishi na wanadamu na sio malaika.
Leo amua kufanya diet ya Moyo.

 Watoe watu wote uliowaweka na wakaongeza uzito wa moyo wako.
Biblia inasema tuchukuliane na kusameheana,na hata kama ipo sababu ya kumlaumu aliyekukosea wewe msamehe kama na wewe ulivyosamehewa.(wakolosai3:13)
Umewahi kujiuliza Mungu angekua anaweka waliomkosea moyoni ingekuwaje?
Sasa kama Mungu ameamua kutusamehe sisi,wewe ni nani uendelee kumshikilia mtu? na kuuongezea moyo wako uzito?

Kwa taarifa yako,amayeumiaga zaidi ni yule anayetakiwa kusamehe na sio anayetakiwa kusamehewa!
Leo fanya Diet ya Moyo.

Punguza Idadi ya watu uliowabeba ili moyo wako uwe na afya njema.
Moyo uliochangamka ni DAWA nzuri.Mith17:22
Wakati mwingine huhitaji dawa ya hospital kwa magonkwa yako, fanya tu Diet ya Moyo,utapona!
Fanya diet ya moyo leo uupunguzie moyo wako hatari ya kuvamiwa na jambazi presha huko baadae.
#‎TeamDietYaMoyo‬#‪#‎OperationPunguzaUzitoWaMoyo‬#

~Mwl Minna.

Thursday, June 4, 2015

VILE MUNGU ALIVYOKUUMBA BINTI, UNAPENDEZA! USIJARIBU KUMKOSOA MUUMBA WAKO!

Kila kitu Mungu alichokiumba aliona ya kuwa ni chema sana!

Vile vile kilivyokua alikiona ni kizuri.

Alivyokuumba mweusi alikuona ni mzuri hivyo hivyo na weusi wako....
Angetaka uwe mweupe angekuumba mweupe.


 Alivyokuumba na umbo lako hilo hilo aliona ni zuri,angetaka uwe tofauti angekuumba hivyo.

Sasa kwa nini umkosoe muumbaji wako?


Rangi na maumbile vimekua mtihani kwa wanawake wengi.

Wanaamini wakiwa na rangi nyeupe na makalio makubwa ndio wazuri..hivyo hukazana kujiongeza.Huo ni uongo wa shetani.wewe ni mzuri kwa namna Mungu alivyokuumba.

Uzuri wa kujiongezea unajulikana na huwa unaisha.

Mwanamke ukijitambua thamani yako,hutahitaji nyongeza bandia kwnye mwonekano wako.
Simaanishi usipendeze wala usijirembe, namaanisha kuwa nadhifu lakini ukiwa na urembo asilia..sio kujibadilisha rangi na kujiongezea makalio!

Wewe ni mzuri hivyo hivyo ulivyo!
‪#‎BintiJitambue‬#Wewe ni wa thamani#

~Mwl Minna.

UJANA MAJI YA MOTO, HUWA YANAPOA!


Vijana wengi huwa wanadhani watabaki vijana siku zote!
Ujana huwa ni hatua tu katika maisha ya mwanadamu ambayo huwa mtu hupitia akitokea utoto kwenda utu uzima!
Vijana wengi hujisahau na kudhani watabaki kuwa vijana milele!!!...

Usijisahau kijana,


 UJANA NI MAJI YA MOTO, HUWA YANAPOA!






Siku moja utavuka hatua ya ujana na kuwa mtu mzima.
Wakati wa ujana ni wakati wa kujijenga kwa kujiwekeza na maarifa yatakayokusaidia utu uzimani, kujijenga kwa kuwekeza kiuchumi kutakakokusaidia utu uzimani, ni wakati wa kuwekeza kimahusiano kutakakokusaidia utu uzimani,
ni wakati wa KUWEKEZA!

WEKEZA UJANANI, UVUNE UTU UZIMANI!

SIO wakati wa kujibomoa kwa kampani mbaya, SIO wakati wa kujibomoa kwa kubadili kila sampuli ya wanawake/wanaume, SIO wakati wa kujaribu kila kipitacho mbele yako kama madawa ya kulevya na sigara.

Ujana wako ni kielelezo tosha cha kujua utu uzima wako utakuwaje!

 Hujawahi kusikia mtu anasema, ningerudi kuwa kijana ningefanya mambo makubwa sana?
Huyo alipoteza muda wakati wa ujana, na sasa anajutia utu uzimani!


Usipoteze Muda kijana, Wekeza wakati wa ujana kujifunza maarifa katika maeneo mbalimbali ya maisha, na utu uzimani utavuna matunda ya kuwekeza kwako!

Soma vitabu, jifunze mambo mbali mbali, hudhuria mikutano na semina mbalimbali, jiongeze kielimu, fanya chochote, ili mradi Ujiwekeze, baada ya kuvuka hatua ya Ujana utaona matunda mema!

Acha vijana wakucheke wakuona mshamba, lakini unajua unachofanya!
Anza kufungua macho yako na kujiona miaka 20 mbele, unataka kuwaje,halafu anza kutengeneza mazingira ya kufika hapo.

Penda kutafakari Neno la Mungu kila siku, litakupa mwongozo wa maisha, na kujua cha kufanya na cha kuacha!

Kwa kufanya haya machache, nakuhakikishia Ujana wenye Ushindi!
‪#‎UjanaMajiYaMotoHuwaYanapoa‬#‪#‎KijanaJitambua‬#

~Mwl Minna

Wednesday, May 27, 2015

UMEKIONA UNACHOKITAFUTA?



Kila mtu kila kunapokucha huamka akiwa na matumaini ya kupata kile anachofatuta.
Wengine hudhani wakibadili kazi wanazofanya watakipata,
Wengine hudhani wakidabili biashara wanayofanya watakipata,
Au wakiongeza Elimu zaidi watakipata,
Au labda wakioa/kuolewa watakipata,
Na labda wakibadili mahali pa kuishi wakakiona!
Kila mtu huhangaika huku na kule kukitafuta, kwa namna yoyote ile, na kwa njia yoyote ile,
Lakini cha kusikitisha ni kwamba kati ya wengi wanaokitafuta, ni WACHACHE sana, hukiona!
Na wanapokiona wanakua wamekamilika katika kuishi kwao hapa duniani.
Ni nini basi kitu hiki?


Ni KUSUDI la kuumbwa kwako.

Utakapogundua KWA NINI UPO HAPA DUNIANI , hapo ndipo utapata furaha ya kweli,kwa sababu UTAKUA UNAFANYA KILE ULICHOUMBWA KUFANYA.

Siku zote mtengeneza Gari hujua matumizi yake.
Na anapolitengeneza hulipa kila kinachohitajika ili kutimiza lengo ya yeye kulitengeneza.

Kadhalika na wewe,

Aliyekuumba anajua unachotakiwa kufanya, Na amekuwekea kila unachokihitaji kutimiza kile alichokuumbia kufanya.
Sasa, ili kujua kile ambacho umeumbiwa kufanya lazima UMUULIZE ALIYEKUUMBA.

...itaendelea
                                                                                                  ~minnamatee

Wednesday, April 29, 2015

EVERY PROBLEM HAS AN EXPIRE DATE:

We usually think that whatever we go thought in life, is there to stay. But we forget that before that situation started it was not there ,and it is not there to stay, it is just passing by.



There is a story of a women who had a problem in her life and thought that the problem had become part of her life in Luke 8. But after some years her problem came to an end because Every problem has an expire date!

She was bleeding for 12 years. Everyday of her life for 12 years she experienced that problem.
I believe when it started, she had hope tomorrow its going to stop, tomorrow came, the problem was still there.

She thought that next week, the bleeding would stop, but it didn't stop. She thought may be this year is the last year for my problem, but the problem still persisted!
She used all the money she had to visit all the doctors she knew in her town but still the problem persisted!

The first year, the second year, the fifth year, the tenth year..it went on and on to 12 years and one day was the last day for her problem.

She was not tired of seeking for solutions to her problem.

A day she didn't know that it was the Expiry date of her problem came.

Then she decided to move and get out of her normal zone, she received her healing.

One day a man called Jesus, passed in her town, and she heard that, that man heals people.
And as usual she visits every doctor, she also went to Jesus. And because of her problem, even the society segregated her.

So she thought in her mind, I have to go to Jesus, but my people won't allow me. Because according to their customs and traditions she was unclean and should not mix with the society.

So she decided to squeeze herself between the crowd and made sure that even if she won't talk to him, she will touch the herm of His garment, and she will be healed.

She did so, and that day marked the end of her problem!

That day was the expire date of her problem.

From the story of this woman we are assured that, every problem has an expire date. and as long as the sun rises and goes down that expire date will come.

It might not be today, but there is a day that problem will expire, if only you do not give up.

REMEMBER: EVERY PROBLEM HAS AN EXPIRE DATE!


Remain Blessed,
Minna

Saturday, March 14, 2015

MAFANIKIO YAKO YANATEGEMEA SANA UNAHUSIANA NA NANI.



Mafanikio yako yako mikononi mwa watu! Baraka zako ziko mikononi mwa watu! Isaya 43:4, inasema Mungu analeta watu kwa ajili yako,,

Kuzipokea Baraka hizo itategemea sana, unahusianaje na watu wanaokuja maishani mwako.

Kiwango cha kupokea Baraka zako kinategemewa na namna unavyowapokea watu Mungu anaowaleta kwenye maisha yako.

Hakuna mtu anayekuja kwa bahati mbaya kwako. kila mtu anakuja kwneye maisha yako anakuja kwa kusudi, na kwa wakati Fulani.

Watu wengine huja wakawaida sana, na hawaonekani kama ndio wenye hizo Baraka, na kwa sababu wanadamu wanaangalia sura ya nje, hujikuta wanakosa zile Baraka.

Dhahabu huchimbwa chini sana kwenye udongo, uksiema hutaki kuchafuka na udongo huwezi kuipata dhahabu!

Kuna vitu hasa vyenye thamani, huwezi kuvipata juujuu, ukiona umekipata juujuu ujue sio dhahabu hilo ni jiwe la kawaida!

 Uwe na Jumamosi njema.

 Minna!

 

Wednesday, January 7, 2015

HAPPY NEW YEAR 2015!!!!!!

 
HAPPY NEW YEAR 2015!
This is how we received and celebrated this new year at Dar Es Salaam Pentecosal Chruch(DPC)
 
 
 

Rivers of Life Worship Team Dancing before the Lord thanking Him for 2014!

Eagrly waiting for the new year!


Receiving the new year 2015!











Worship in His Presence!





MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...