Inawezekana
umezunguka kila mahali ukitafuta upendo wa kweli,
Umeingia
kwenye mahusiano ukidhani huko utapata upendo wa kweli, lakini ukaishia
kuumizwa!
Ukadhani
ukiwa na pesa utapata upendo wa kweli, nako ukakuta hakuna upendo.
Ukadhani umaarufu
ndio utakupa upendo wa kweli, lakini ukweli ni kwamba watu wengi maarufu huwa
wapweke sana.
Wanadamu
wawawezi kukupa upendo wa kweli.hata kama akikuonyesha upendo leo, lazima
atataka kulipwa upendo ule na jambo fulani.
Lakini yupo
ambae ni mwanzilishi wa upendo, nae ana upendo wa kweli, usio na madai.
Yeye
alikupenda hata kabla hujafikiria kumpenda! (najua unawaza hili linawezekanaj!)
Lakini
nikwambie, hilo linawezekana na lilishafanyika, Zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Yupo ambae
alibeba kila mzigo wako tayari ili wewe uishi maisha huru bila mizigo.
Upendo wake
haupungui wala hauchuji.
Uko vile
vile tangu siku ya kwanza na milele.
Naye ni
muumba wako na Mungu aliyetuumba sisi wanadamu.
Alitupenda
mnoo akaamua kumtuma mwanae wa peke Yesu Kristu ili aje afe msalabani kwa ajili
ya dhambi zangu mimi na wewe.(Yohana3:16)
Ili kila
atakayemwamini, asipotee bali awe na uzima wa milele.
Leo basi
fanya uamuzi wa kuupokea huu upendo wa Mungu ndani ya moyo wako.
Mkubali awe
Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na ataujaza moyo wako kwa upendo mwingi nawe
utafanyika upendo kwa wengine.
Fuatisha
sala hii pamoja nami:
Bwana Yesu,ninakuja kwako, naukubali
upendo wako na kile ulichofanya kwa akiji yangu. Natoka maisha yangu
kwako,kwanzia leo nikutegemee wewe peke yako, na kukuishia wewe peke yako. Ninatubu
dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe. Nisaidie kuishi maisha ya kukupendeza
wewe siku zangu zote.sasa nimeokoka. Katika Jina la Yesu nimeomba.Amina.
Hongera kwa
kuokoka na kuingia katika familia wa wana wa Mungu.
Tafuta
kanisa lililo karibu nawe linalofundisha Neno la Mungu na uende ukajifunze
hapo.
Waweza pia
kutujulisha kuhusu uamuzi wako kwa namba hizi: 0753008212, 0714303330.
Au kwa barua
pepe:kingjesustz@gmail.com
Imeandaliwa na:
King Jesus International Ministries,
Kimara Temboni,
Dar- Es- Salaam,Tanzania.
Simu: +255753008212
Email: kingjesustz@gmail.com.
No comments:
Post a Comment