Thursday, August 25, 2016
FURAHIA MAISHA KILA SIKU!
TUMEUMBWA KUTENDA MATENDO MEMA.
Efeso 2:10
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Kila mtu Mungu aliyemuumba hakumuumba awe mbaya, atende mabaya au afanyie wengine ubaya.
Mungu alipotuumba alituumba ili tutende matendo mema kila siku.
Hayo matendo, tayari yalishaawekwa tayari kwa ajili yetu kutenda. Sio sisi tunaanza kutaumba, au kuyatengeneza, bali yalishatengenezwa kwa ajili yetu.
Hivyo unapoanza siku yako,anza ukiwa na nia,na dhamira ya kutenda matendo mema.
Usianze siku yako na nia ya kutenda mabaya au kusema mabaya. bali anza siku ukiwa na lengo, ukiwa na nia ya kutenda matendo mema, uliyoandaliwa tayari kuyatenda.
Furahia maisha kila siku!
Mwl. Minna Matee Mboya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...
Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...
-
Some people would say that God is against prosperity, but these ten famous Christian businessmen would disagree. In fact, they would likel...
-
Bila shaka umewahi na hata sasa unao marafiki wengi. ...Lakini ili kuwa mtu mwenye matokeo, uchaguzi wa aina ya marafiki ni jambo la msingi ...
-
Ni kweli uliowazi kwamba hakuna jambo jipya chini ya jua! Lakini pia pamoja na kwamba hakuna jambo jipya ila utofauti upo kwenye nani analif...
No comments:
Post a Comment