Saturday, August 27, 2016

FURAHIA MAISHA KILA SIKU!



MAMBO YA AJABU MNO!
Waefeso3:20.
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno,kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo,kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.


Yako mambo unaomba na Mungu anajibu,na kuna mambo unaweza ukawaza tu na Mungu akayafanya.

Unapokuwa na uhusiano na Mungu binafsi, sio kila kitu unachopata kutoka kwake unakuwa umemwomba.

Vingine,unaviwaza tu na vinatokea,kwa sababu unakuwa unawaza sawa na mawazo yake.
Na mambo haya sio ya kawaida tu,bali ni ya ajabu mno!!

Hivyo usiogope kuomba au kuwaza mambo makubwa ya ajabu,kwa sababu Mungu ameahidi kuyatenda. Tena sio ya ajabu tu bali ni ya AJABU MNOOO!

Lakini sentensi ya mwisho inasema,Kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu..
Kiwango cha nguvu ya Mungu kilicho ndani yako,ndicho kinategemea utendaji wa yale unayoomba na\au kuwaza.

Hivyo siri ya kuona yale uombayo na kuwaza yakiwa halisi,ni kuongeza nguvu ya Mungu ndani yako kwa kujaza maarifa ya Neno lake ndani yako, na kuyatendea kazi.
Na baada ya kupokea,tutamtukuza Mungu kama Paulo alivyoanza na kumtukuza mwanzoni mwa mstari huu!

Umebarikiwa,
Furahia Maisha kila Siku!
~Minna.


Friday, August 26, 2016

FURAHIA MAISHA KILA SIKU!

UNAYAWEZA YOTE!
Wafilipi 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Uwezo wa kufanya vitu uko ndani ya kila mtu anayetiwa nguvu.
Nguvu ndizo zinatupa kufanya vitu bila kuchoka. Bila nguvu huwezi kumaliza jambo, lazima utachoka njiani na kuacha.
Mungu ndiye anayetupa nguvu za kuweza kufanya vitu na kuvimaliza.
Ukiutambua uwezeshaji wake kwako leo, atakuwezesha kufanya na kutimiza yale malengo yako uliyojiwekea.
Ulishawahi kukutana na watu ukashangaa wamewezaje kufanya mambo fulani ambayo kwa kawaida yasingewezekana?
Waliweza kwa sababu waliwezeshwa kwa kupewa nguvu na Mungu.
Mkaribishe Mungu kwenye siku yako leo akupe nguvu ya kufanya mambo yote ambayo umetamani kuona unayafanya.

Umebarikiwa!
~Minna

Thursday, August 25, 2016

FURAHIA MAISHA KILA SIKU!


TUMEUMBWA KUTENDA MATENDO MEMA.
Efeso 2:10
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Kila mtu Mungu aliyemuumba hakumuumba awe mbaya, atende mabaya au afanyie wengine ubaya.
Mungu alipotuumba alituumba ili tutende matendo mema kila siku.
Hayo matendo, tayari yalishaawekwa tayari kwa ajili yetu kutenda. Sio sisi tunaanza kutaumba, au kuyatengeneza, bali yalishatengenezwa kwa ajili yetu.
Hivyo unapoanza siku yako,anza ukiwa na nia,na dhamira ya kutenda matendo mema.
Usianze siku yako na nia ya kutenda mabaya au kusema mabaya. bali anza siku ukiwa na lengo, ukiwa na nia ya kutenda matendo mema, uliyoandaliwa tayari kuyatenda.

Furahia maisha kila siku!
Mwl. Minna Matee Mboya.

Thursday, August 11, 2016

UPENDO WA KWELI!




Inawezekana umezunguka kila mahali ukitafuta upendo wa kweli,
Umeingia kwenye mahusiano ukidhani huko utapata upendo wa kweli, lakini ukaishia kuumizwa!

Ukadhani ukiwa na pesa utapata upendo wa kweli, nako ukakuta hakuna upendo.
Ukadhani umaarufu ndio utakupa upendo wa kweli, lakini ukweli ni kwamba watu wengi maarufu huwa wapweke sana.

Wanadamu wawawezi kukupa upendo wa kweli.hata kama akikuonyesha upendo leo, lazima atataka kulipwa upendo ule na jambo fulani.
Lakini yupo ambae ni mwanzilishi wa upendo, nae ana upendo wa kweli, usio na madai.
Yeye alikupenda hata kabla hujafikiria kumpenda! (najua unawaza hili linawezekanaj!)

Lakini nikwambie, hilo linawezekana na lilishafanyika, Zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Yupo ambae alibeba kila mzigo wako tayari ili wewe uishi maisha huru bila mizigo.

Upendo wake haupungui wala hauchuji.
Uko vile vile tangu siku ya kwanza na milele.
Naye ni muumba wako na Mungu aliyetuumba sisi wanadamu.
Alitupenda mnoo akaamua kumtuma mwanae wa peke Yesu Kristu ili aje afe msalabani kwa ajili ya dhambi zangu mimi na wewe.(Yohana3:16)
Ili kila atakayemwamini, asipotee bali awe na uzima wa milele.
Leo basi fanya uamuzi wa kuupokea huu upendo wa Mungu ndani ya moyo wako.

Mkubali awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na ataujaza moyo wako kwa upendo mwingi nawe utafanyika upendo kwa wengine.

Fuatisha sala hii pamoja nami:
Bwana Yesu,ninakuja kwako, naukubali upendo wako na kile ulichofanya kwa akiji yangu. Natoka maisha yangu kwako,kwanzia leo nikutegemee wewe peke yako, na kukuishia wewe peke yako. Ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe. Nisaidie kuishi maisha ya kukupendeza wewe siku zangu zote.sasa nimeokoka. Katika Jina la Yesu nimeomba.Amina.

Hongera kwa kuokoka na kuingia katika familia wa wana wa Mungu.
Tafuta kanisa lililo karibu nawe linalofundisha Neno la Mungu na uende ukajifunze hapo.
Waweza pia kutujulisha kuhusu uamuzi wako kwa namba hizi: 0753008212, 0714303330.
Au kwa barua pepe:kingjesustz@gmail.com

Imeandaliwa na:
King Jesus International Ministries,
Kimara Temboni,
Dar- Es- Salaam,Tanzania.
Simu: +255753008212
Email: kingjesustz@gmail.com.

 

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...