Wednesday, April 17, 2013

Wamiliki blogu za dini waja na Chomoza


Pichani ni waanzilishi wa kipindi cha Chomoza Samuel Sasali na James Temu


WAMILIKI wa blogu za dini, James Temu na Samuel Sasali, wanatarajiwa kusikika katika kipindi kipya cha ‘Chomoza’ kitakachorushwa na Clouds TV.
Kipindi hicho, kitasheheni habari mbalimbali za muziki na wanamuziki wa injili, taarifa za injili nchini na burudani ya muziki wa ndani na nje ya Tanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Temu na Sasali walisema kuwa kipindi hicho ni cha kinabii, kwani wazo la kukianzisha lilitengenezwa kwa neno la ufunuo wa Mungu mwenyewe.
“Kama ambavyo tumeanza kusema katika Isaya 60:1, Biblia inasema, ‘Arise and shine, your light has come’, tunaamini kuwa, huu ni muda wa kipindi cha kanisa kusimama, hiki ni kipindi cha watu kumjua Mungu, kupenya, kuibuka, kusimama kama ambavyo Shedrak, Meshack na Abdinego walivyochomoza katikati ya watu wa Babeli,” walisema.
Temu alisema kuwa mashabiki watapata ladha halisi ya ‘Chomoza’, kwa sababu kila atakayekuwa anatamka neno hilo la kinabii, maisha yake yatainuliwa. Kipindi hicho kitarushwa kila Jumapili kuanzia saa tano asubuhi.

Chanzo: Tanzania Daima 17, Apr 2013.


 
 

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...