Uchungaji ni huduma mojawapo kati ya huduma tano zilizoainishwa kwenye biblia. Mchungaji anajukumu la kulitunza, kulilisha na kuliangalia kundi lake ili liweze kustawi na kuwa mbali na adui shetani. Kumtumikia Mungu kama mchungaji ni huduma njema sana na yenye kuheshimika lakini wachungaji wengi wamekuwa na wakati mgumu kutokana na lawama na kukatishwa tamaa na wale wanaowachunga bila kujali ugumu wa huduma. jinswanajitoa kwa ajili ya makanisa wanayoyac
Ni vizuri mshirika ukajifunza njia mbali mbali za kumtia moyo mchungaji wako na kujitahidi kuwa kondoo mwema ili kupokea baraka za kuwa chini ya mchungaji na pia kupunguza ugumu wa kazi kwa mchungaji wako na kumwezesha kuifanya kazi hii kwa furaha zaidi.
Kuna njia nyingi za kufanya hivi ila leo nitaziongelea njia chache ili kukukumbusha pale uliposahau kwa ajili ya ustawi wa kazi ya Mungu:
1. Kuwa Sehemu ya Huduma.
Kuwa sehemu ya Huduma kwa kuhusika moja kwa moja na shughuli zote zinazohusika na huduma ikiwa ni pamoja na kuhudhuria ibada kwa uaminifu na onyesha kuwa upo tayari kufuata uongozi wake. Hii kwanza itabariki maisha yako na itamtia moyo mchungaji wako pia. Onyesha mchango wako katika meneo mbalimbali kanisani kwa kutumia karama zako na vipawa. Uwe tayari kutumika bila kutarajia kupata chochote kutoka kwa mchungaji. Uwe mwepesi kuwashuhudia wenye dhambi neno la Mungu na kuwatia moyo wale waliovunjika moyo na kukata tamaa.
2. Wahi kwenye Ibada na Onyesha Uhai Wakati wa Ibada
Huwa inamtia moyo sana mhubiri, pale anapokuwa akihubiri na watu kuonyesha kuwa wapo pamoja naye na wanamsikiliza kwa makini.Onyesha uhai kwa kuitikia, kwa kupiga makofi, kwa kupunga mikono na hata kusimama pale wanapoguswa na ujumbe fulani. Kwanza atajua kuwa kuna watu wanamsikiliza na sio kusikiliza tu bali wanapokea kile wanachohubiriwa. Waweza kushiriki katika kuandaa ibada kwa kushiriki katika kufanya usafi, kupamba kanisa.
3. Muombee Mchungaji Wako
Mchungaji wako anakutana na changamoto nyingi katika utendaji wa kazi ya Mungu na anahitaji sana maombi yako maana kwa kibinadamu ni vigumu kuzikabili. Muombee ili Mungu amtie nguvu, ampe hekima, na kuzidi kumfunulia siri zake kwa ajili yenu ambao mpo chini ya uchungaji wake. Ombea familia yake, mke au mume wake na watoto wake pia.
2 Thesalonike 3:1-2 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.
4. Onyesha Utii Kwa Uongozi Wake
Biblia inaonyesha wazi kuwa ni lazima kuwaheshimu viongozi wetu wa kiroho. Ebrania 13:17 inasema “Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi”
Haipendezi wala haibariki kuwa kinyume na uongozi uliopo chini ya mchungaji wako na kwa yale ambayo anakuagiza kutenda maana yeye ndiye anayekesha kwa ajili ya roho yako.
5. Mheshimu
Mheshimu mchungaji wako hata zaidi ya unavyomheshimu mtu mwingine anayekuongoza. Ndio, unaweza ukawa unamazoea ya karibu na mchungaji wako lakini hii haikufanyi ukose heshima, muonyeshe heshima kwa maneno na kwa vitendo iwe ni kanisani au mahali pengine popote hata kama umemzidi kipato, elimu, umri n.k
1 Thesalonike 5:12-13Lakini, Ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
6. Simama Pamoja Naye Katika Nyakati Ngumu
Rafiki wa kweli ni yule anayesimama nawe katika hali zote za maisha, sio yule anayekuacha pale mambo yanapokuwa magumu. Simama na mchungaji wako katika hali zote, usiwe mshirika wa matukio na mafanikio bali simama naye katika nyakati zote. Mtie moyo pale anapopitia magumu iwe ni katika huduma au kifamilia na kumsapoti kwa hali na mali pia, na sio kusimama pembeni na kumsengenya au kumlaumu.
...fuatilia sehemu ya pili wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment