Tuesday, October 30, 2012

MAMBO YALIVYOKUA MTBC MOSHI JUMAPILI HII

Manna Tabernacle Bible Church aka MTBC ni moja ya makanisa ambayo yanaleta mguso mkubwa katika mji wa Moshi na kwa wakazi wa mji wa Moshi na meneo ya jirani.
Kila jumapili ya mwisho wa mwezi kunakua na Ibada ya kusifu na kuabudu ambayo huongozwa na Praise Team ya MTBC ikiongozwa na Mama Mchungaji Elizabeth Mtalitinya wakishirikiana na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Moshi.
Jumapili hii ya tar 29 Oct, 2012 ilikua ni Ibada ya Tisa ya kusifu na kuabudu tangu Ibada hizi kuanzishwa pale MTBC.

Mungu alionekana kwa namna ya tofauti na kugusa maisha ya watu waliokuwa wamehudhuria katika ibada hiyo.Pichani ni baadhi tu ya ambavyo Ibada hiyo ilivyokua.

Mama Mchungaji Elizabeth Mtalitinya  akiwaongoza watu katika kumsifu Mungu.



Mchungaji Dickson Mtalitinya (aliyeshika microphone), Mchungaji kiongozi wa kanisa la MTBC Moshi, akiwaombea watu kupokea mahitaji yao kutoka kwa mungu.



MTBC Praise team wakiwa kazini, kumsifu Mungu!

 

Mchungaji Yustice Danga akisisitiza jambo wakati wa Ibada ya kusifu na kuabudu MTBC Moshi.



Watu Peopleeeeeeeeeeeeeeee


Mtumishi wa Mungu Dorcas Mtalitinya nae alikuwepo, Mungu azidi kukuinua!



Ester Bukuku, Mwimbaji wa nyimbo za Injili nae alikuwepo.


Daktari na Mtumishi wa Mungu Lightness Ng'unda akimsifu Mungu


Mr. Bez nae alikuwepo akimsifu Mungu
 
Aaron akiitendea haki mashine.
 
Pierre akiwa kikazi zaidi hapa
 
 
Drums zingekua zinaongea, zingesema zenyewe,mi sizisemei!
 
 
 
Na watoto nao wanamsifu Mungu
 
 
                       Kila mtu alikua busy akimsifu Mungu!

MTBC Praise team wakimsifu Mungu katika moja ya ibada za mwisho wa mwezi.



Ni kila jumapili ya mwisho wa mwezi pale MTBC Moshi mjini..Usikose mwezi ujao!

Saturday, October 20, 2012

NAMNA YA KUWA MTENDAJI WA NENO LA MUNGU


 
 
Katika utangulizi fahamu mambo matatu makubwa yafuatayo:

1. Wewe ni balozi wa Kristo na kwa ajili ya Kristo hapa ulimwenguni. “Basi tu wajumbe (mabalozi) kwa ajili ya Kristo….” (2Wakorintho 5:20)

2. Ikiwa wewe ni balozi, basi wewe si wa ulimwengu huu kama vile Kristo asivyo wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Uraia wako au wenyeji wako si wa hapa ulimwenguni, bali ni wa nyumbani mwake Mungu. “ Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” (Waefeso 2:19)

3. Ikiwa wenyeji wako ni mbinguni katika ufalme wa Mungu, nyumbani mwake Mungu unafanya nini hapa ulimwenguni? Kuna sababu kubwa za wewe kuwa hapa ulimwenguni. Ni kwa sababu umetumwa kama Kristo alivyotumwa. “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.” (Yohana 17:18)

Tunajua hukutumwa hapa ulimwenguni ili ufanye kazi peke yako. Tuko hapa ulimwenguni tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu. “ Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu…” (1Wakorintho 3:9)

Huwezi ukawa mfanyakazi pamoja na Mungu bila ya kuwa mtendaji wa Neno; kwa kuwa Mungu ni Neno (Yohana 1:1). Kuwa balozi wa Kristo maana yake ni kuwa mwakilishi wa Neno; kwa kuwa Kristo ni Neno (Yohana 1:14). Uwakilishi huu hauonekani kwa sabatu watu wa Mungu walio wengi hawaelewi namna ya kuwa watendaji wa Neno ili Neno lionekane hapa ulimwenguni.

Katika somo hili tunajifunza juu ya namna ya kuwa mtendaji wa Neno, ili ufanye kazi ya ubalozi wa Kristo vizuri. Ni maombi yetu kwa Mungu ya kuwa somo hili lizae matunda katika maisha yako ya kiroho katika Kristo.
 
 
UMUHIMU WA KUWA MTENDAJI WA NENO
Ikiwa kuna swali kubwa ambalo linawatatanisha wakristo wengi, basi ni swali la kukua kwa imani yao ya kikristo. Wengine wanaita ni kukua kiroho kwa wakristo.
Ukiwauliza wakristo wengi ya kuwa ni tatizo gani wanaloliona kubwa, linalowakwamisha katika maisha yao ya kikristo; walio wengi watasema ni tatizo la imani.
Tatizo hili linatokea kati ya watu wa Mungu, kwa kuwa hawajui imani ni nini, na kwamba inapatikanaje. Na wengine wamekuwa wakijitahidi kuomba kwa Mungu kwa muda mrefu ili imani zao zikue, lakini bila mafanikio ya kuridhisha.
Kwani imani maana yake nini?
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1)
Katika mstari huu tunaona mambo mawili makubwa.
  1. Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo; na 2. Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Imani inakupa uhakika sasa juu ya mambo ambayo unayoyatarajia. Imani inaweka wazi (bayana) mambo yasiyoonekana.
Chanzo cha imani ndicho pia chanzo cha uhakika wako katika maisha ya kikristo; pia ni chanzo cha uwazi wa mambo ya rohoni yasiyoonekana. Chanzo cha imani ndicho pia kinakupa uhakika wa maisha yako ya wokovu.
Chanzo cha imani ni nini? Imani huwa mtu anaipataje? Kwa maneno mengine unaweza ukauliza, chanzo cha uhakika ulio nao wa wokovu na ukristo ni kitu gani?
Mara nyingi watu wa mataifa huwa wanauliza maswali yafuatayo: Mtu atawezaje kuwa na uhakika wa kuokoka akiwa hapa duniani? Mtu atawezaje kuwa na uhakika ya kuwa amesamehewa dhambi wakati bado yupo duniani?
Maswali haya huwa yanatokea mara kwa mara kwa sababu hawajui uhakika wa mambo hayo unatoka wapi. Laiti wangejua, basi wangekuwa na usemi mwingine midomoni mwao juu ya wokovu.
Biblia inasema wazi kabisa kwamba yote yawezekana kwake aaminiye (Marko 9:23). Na kama biblia ambayo ni Neno la Mungu inasema yote yawezekana kwake aaminiye, mwanadamu ni kitu gani mbele za Mungu hata apinge?
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Imani chanzo chake ni nini?
“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo” (Warumi 10:17)
Mstari huu wa biblia unatufahamisha kuwa imani chanzo chake ni kusikia Neno la Kristo. Hii ina maana ya kuwa uhakika wa wokovu, au ukristo na misingi yake unapatikana kutokana na kusikia Neno la Kristo.
Watu wengi utawasikia wakiomba na wakati mwingine kwa kufunga na kwa kuomboleza ili Mungu awape imani. Lakini mabadiliko katika maisha yao hayaonekani.
Biblia inatufahamisha wazi kabisa kuwa ‘imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo. Imani huja kwa Neno la Kristo. Imani huja kwa kusikia Neno la Kristo!
Watu wengi wamekuwa wakiomba imani na wanapoona haionekani katika maisha yao, wanaanza kumkemea shetani bila mafanikio yoyote. Watu wengi wanajikuta wamo katika hali ya kukwama kiroho na kudumaa kwa sababu hawajawa wasikiaji wa Neno la Kristo.
“Lakini iweni watendaji wa Neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu” (Yakobo 1:22)
Kwa mstari huu tunapata upeo mkubwa kidogo juu ya chanzo cha imani. Tunaweza sasa kusema, imani chanzo chake ni kusikia na kulitenda neno la Kristo.
Imani huja kwa kulisikia na kulitenda neno la Kristo. Uhakika tulio nao katika Njia hii ya wokovu katika Kristo unatokana na Neno la Kristo tulilolisikia na kulitenda.
Kuwa msikiaji tu wa Neno la Kristo haitoshi bila ya kuwa mtendaji wake. Neno la Kristo lililosikiwa na mtu, lisipowekwa katika matendo haliwezi kuonekana na watu wengine.
Watu wengi sana ni wasikiaji wa Neno la Kristo, utawakuta makanisani, wakiliskiliza Neno, utawakuta kwenye mikutano ya kiroho pia utawakuta kwenye semina za Neno la Mungu; lakini watendaji wa Neno hilo la Kristo wanalolisikiliza ni wachache sana.
Wasomaji wa biblia ni wengi sana, lakini watendaji wa Neno hilo wanalolisoma ni wachache sana. Na kwa sababu hii siku hizi ni vigumu sana kuweza kutofautisha kati ya mkristo na mtu wa kawaida, au mtu aliyeokoka na mtu asiyeokoka, kwa kuwaangalia matendo yao.
Mtu anajiita mkristo au ameokoka lakini matendo yake yako mbali sana na Neno la Kristo. Huu ni unafiki mkubwa – unaohitaji kutafutiwa ufumbuzi.
Wakati umefika, na wakati wenyewe ndiyo huu wa watu kujulikana maisha yao ya kikristo yamesimama katika msingi upi. Ikiwa msingi huo ni Neno la Kristo, basi neno hilo ni budi lionekane katika matendo yao ya kila siku.
Imeandikwa; “Lakini iweni watendaji wa Neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”.
Kuwa mtendaji wa Neno la Kristo maana yake nini?
Kuwa mtendaji wa Neno la Kristo maana yake ni kuwa mtumiaji wa Neno la Kristo ulilolisikia. Kuwa mtendaji wa Neno ni kulitumia Neno na Neno nalo likutumie wewe.
Wewe unakuwa ndani ya Neno la Kristo na Neno la Kristo linakuwa ndani yako. Neno la Kristo lililondani yako unalitumia kuwa utukufu wa Mungu. Na wewe ukiwa ndani ya Neno la Kristo, unatumiwa na Neno hilo kumtwalia Mungu utukufu.
Ndiyo maana Yesu Kristo alisema;
“Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni, yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu,” (Yohana 15:4-8)
Kwa mistari hii tunaona kuwa imani ya kikristo ni matokeo ya mtu kuunganishwa na Kristo mwenyewe. Na matokeo ya matunda mazuri ya kikristo yanategemea jinsi ambavyo mtu anavyolisikia na kulitenda Neno la Kristo.
Pia, tunaona kuwa matokeo ya maombi ya mtu aliye mtendaji wa Neno la Kristo ni mazuri na yenye mafanikio kuliko matokeo ya mtu aliye msikiaji tu wa Neno na wala si mtendaji.
Watu wengi ni wasikiaji wa Neno la Kristo, lakini hawalitumii wala Neno haliwatumii kabisa. Na wengine ni wasikiaji na watumiaji wa Neno la Kristo katika sehemu chache tu za maisha yao.
Lakini imeandikwa wazi kabisa kuwa hao wanajidanganya nafsi zao wenyewe, wala hawamdanganyi Mungu, shetani wala mtu yeyote, bali wao wenyewe; kwa kuwa wamekuwa wasikiaji wa neno la Kristo lakini si watendaji.
Na ndiyo maana Roho wa Mungu aliomboleza kwa kupitia kwenye kinywa cha Nabii Hosea akisema; “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ……” (Hosea 4:6)
Na Yesu Kristo, pia, alikuwa na haya ya kusema juu ya watu wa namna hiyo:
“Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mathayo 22:29)
Ni kweli kabisa kuwa kanisa ambalo ni mwili wa Kristo, limekuwa katika hali ngumu kiroho kwa sababu ya kukosa maarifa ya Mungu yanayotokana na kulisikia na kulitenda Neno la Kristo.
Imeandikwa;
“Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.” (Yakobo 1:22-24)
Tunakumbuka wakati fulani tulikuwa tunaongea na mtu mmoja juu ya maisha yake ya wokovu. Tulimuuliza swali hili; “Ni kitu gani kinachokutofautisha wewe na mkristo mwingine wa kawaida?”
Akasema; “Ni kwa sababu nimemwamini Mungu”
Tukasema; “ Hiyo haitoshi kwa sababu hata wao wanamwamini Mungu. Je! hujasoma ya kuwa mashetani nao wanaamini na kutetemeka?”
Akauliza; “Sasa kitu gani kinacholeta tofauti?”
Tukasema; “ Ni maisha yako mapya yanayopatikana baada ya kumpokea Kristo moyoni mwako”.
Tukamsomea waraka wa pili kwa Wakorintho Sura ya tano na mstari wa kumi na saba, unaosomeka hivi; “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya”
Unapompokea Kristo (Neno) moyoni mwako unapewa uzima wa Mungu ndani yako, na tabia mpya inayoongozwa la Neno la Kristo.
Ni vigumu sana kumtofautisha mtu wa Mungu na mtu wa kawaida kwa kusikia wanachosema tu peke yake. Ni lazima maisha mapya ndani ya Kristo, maisha ya wokovu yaandamane na tabia mpya.
Tabia mpya hiyo haionekani siku hizi kwa sababu, watu hawajawa watendaji wa Neno. Yakobo anauliza:
“Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?.....
Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:14,17)
Hii maana yake mtu asipokuwa mtumiaji wa Neno la Kristo, anaonekana kama vile si mkristo. Utafahamu ni mkristo kwa sababu anakwenda kanisani jumapili au jumamosi, lakini si kwa sababu umeona matendo ya kikristo maishani mwake.
Na hata watu wengi waliookoka wanaliabisha Jina la Bwana kwa kujiita wao ni watu wa Mungu, watoto wa Mungu, wana wa mfalme, watumishi wa Bwana; kwa sababu matendo yao hayafanani na maneno wanayosema.
Yafaa nini basi, mtu kusema ameokoka wakati bado anatawaliwa na matendo ya dunia? Yafaa nini, basi mtu kusema yeye ni mkristo, wakati maisha yake yana matendo kama ya mtu asiyemjua Kristo?
“Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu KWA NJIA YA MATENDO YANGU”. (Yakobo 2:18)
KWA NJIA YA MATENDO watu watajua kuwa imani yako ni ipi. Kwa njia ya matendo yako watu watajua ya kuwa wewe in mkristo au La.
Imani yako na ijulikane mbele za watu kwa njia ya kuwa mtendaji wa Neno.
Umefanyika kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo, kwa hiyo matendo yako ni mapya, pia, matendo ya kale yamepita. Kwa matendo yako yaliyosimama ndani ya Neno la Kristo, ulimwengu utajua ya kuwa umeokoka au La.
“Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?....
Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:19,20,26)
Mashetani yanamjua Mungu ya kuwa ni mmoja, na yanaamini hivyo na kutetemeka. Mashetani yana hofu ya Mungu, lakini watu wengi hawana hofu ya Mungu ndani yao.
Kwa kutokuwa mtendaji wa Neno, unajikuta kuwa utamu wa maombi, utamu wa kushuhudia, utamu wa Neno la Mungu unafifia ndani yako.
Imani haiji kwa kuomba, kukua kwa imani yako hakutakuja kwa kuomba, bali huja kwa kusikia na kulitenda Neno la Kristo.
Si kwamba tunadharau sehemu ya maombi katika maisha ya mkristo, la hasha. Maombi ni muhimu sana kwa mkristo kama vile petroli ilivyo muhimu kwa ajili ya gari.
Ukijaza petroli kwenye gari haina faida yoyote hadi hapo utakapoingia ndani ya gari na kuliendesha toka mahali lilipo na kwenda mahali pengine unapotaka.
Maombi bila kuwa mtendaji wa Neno, ni bure. Maombi PAMOJA na utendaji wa Neno vinaleta mafanikio makubwa katika kukua kiroho. Neno ndilo linakuongoza unapotaka kusogea kiroho.
Maombi PAMOJA na utendaji wa Neno ni muunganiko wenye maana kubwa katika kuifanikisha kazi yetu tuliyotumwa kuifanya hapa ulimwenguni; kazi ya kuwa wajumbe (mabalozi) kwa ajili ya Kristo.
Lakini tunajua kuwa “sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu” (1Wakoritho 3:9). Kuwa mfanyakazi pamoja na Mungu maana yake ni kuwa mfanyakazi pamoja na Neno, kwa sababu Mungu ni Neno (Yohana 1:1)
Kuwa mfanyakazi pamoja na Neno maana yake ni kuwa mtenda kazi pamoja na Neno; ni kuwa mtendaji wa Neno; ni kuwa mtumiaji wa Neno.
Si kwamba watu wanapenda kutokuwa watendaji wa Neno, bali wengi hawafahamu ni namna gani ambavyo watafanya ili neno la Kristo walilolisikia au kulisoma lionekana katika maisha yao.


....fuatilia sehemu ya pili wiki ijayo

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUA SIKU YA JANA 19.10.2012 KTK JIJI LA DSM KWANZIA MAJIRA YA SAA SABA MCHANA.

.

                                 HABARI KATIKA PICHA


Maeneo ya Morocco

Maeneo ya Kariakoo


Maeneo ya Posta


Potsa mpya


Kariakoo


 
Ikiwa jana ni siku ya pili tangu vurugu zilizoanza zinazofanywa na Waumini wa dini ya Kiislam kutetea maslahi ya Waislam kutoka kwenye mfumo dume uliopo Tanzania.

Maandamano yalikuwa rasmi kwa ajili ya Kupinga kukamatwa kwa Katibu Wa Wanaharakati wa Kiislam Shekhe Ponda Issa Ponda ambapo walikuwa wakishinikiza Kuachiliwa kwa shekhe huyo aliyefikishwa Mahakamani siku ya Juzi. Waumini hao walishinikiza Serikali kama Mpaka Mchana swala ya Ijumaa itakapokuwa inamalizika kama shekhe huyo hata achiliwa basi wataandamana Jiji zima kushinikiza kuachiliwa kwa shekhe huyo.

Mchana wa jana majira ya saa 6 Mkuu wa Mkoa wa Dar, aliutangazia uma kupitia Radio One kuwa Maandamano hayo hayana baraka za Serikali ni Batili, hivyo watu wasiandamane. Mara baada ya swala ya Ijumaa Waislam wakakaidi amri hiyo kwa kuandamana.

Hii ni wiki ya nne Waislam kuandama kila baada ya Swala ya Ijumaa, wiki iliyopita Waumini wa dini hiyo walichoma Makanisa Kadha wa Kadha kuonesha hasira zao za Kijana mwenye umri wa miaka 12 kukojolea kitabu chao Kitakatifu cha Quran.

Jana Jeshi la Polisi, FFU na Jeshi la JWTZ wamefanikiwa kutawanya maandamano hayo yaliyotokea kona mbali mbali za Dar, maeneo ambayo mabumu ya machozi yalitumika ni Kariakoo, Posta Mpya, Magomeni, Kinondoni na Maeneo ya Buguruni
 
Source:samsasali.blogspot.com

Friday, October 19, 2012

MABINTI MSIKOSE WEEKEND HII ! TAR 19-21 OCT 2012, NI PALE LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE!

 
 

SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM


 
Askofu Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Alex G. Malasusa(kushoto)
 
SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.


Wapendwa Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.
Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).

      Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.

Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.


Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:

      Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.

Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.

       Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.


Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:

      Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.

Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.

      Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania

Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.

      Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:
 

 
      Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?

Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.

Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini

  Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.

       Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,

      Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini


Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

Daima tukumbuke kuwa, “KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” (Waefeso 6: 12).
Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,

     Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani

     Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki

     Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini

     Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati

     Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe

     Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini

    Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati

   Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi

   Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria

   Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara

   Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero

   Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde

   Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
   
  Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa

   Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro

   Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu

   Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru

   Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare

   Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma

   Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati




Mbagala, DSM, 18 Oktoba 2012



 

Thursday, October 18, 2012

NAMNA YA KUMTIA MOYO MCHUNGAJI WAKO ( Sehemu ya Kwanza)

Uchungaji ni huduma mojawapo kati ya huduma tano zilizoainishwa kwenye biblia. Mchungaji anajukumu la kulitunza, kulilisha na kuliangalia kundi lake ili liweze kustawi na kuwa mbali na adui shetani. Kumtumikia Mungu kama mchungaji ni huduma njema sana na yenye kuheshimika lakini wachungaji wengi wamekuwa na wakati mgumu kutokana na lawama na kukatishwa tamaa na wale wanaowachunga bila kujali ugumu wa huduma. jinswanajitoa kwa ajili ya makanisa wanayoyac
Ni vizuri mshirika ukajifunza njia mbali mbali za kumtia moyo mchungaji wako na kujitahidi kuwa kondoo mwema ili kupokea baraka za kuwa chini ya mchungaji na pia kupunguza ugumu wa kazi kwa mchungaji wako na kumwezesha kuifanya kazi hii kwa furaha zaidi.
Kuna njia nyingi za kufanya hivi ila leo nitaziongelea njia chache ili kukukumbusha pale uliposahau kwa ajili ya ustawi wa kazi ya Mungu:

1. Kuwa Sehemu ya Huduma.

Kuwa sehemu ya Huduma kwa kuhusika moja kwa moja na shughuli zote zinazohusika na huduma ikiwa ni pamoja na kuhudhuria ibada kwa uaminifu na onyesha kuwa upo tayari kufuata uongozi wake. Hii kwanza itabariki maisha yako na itamtia moyo mchungaji wako pia. Onyesha mchango wako katika meneo mbalimbali kanisani kwa kutumia karama zako na vipawa. Uwe tayari kutumika bila kutarajia kupata chochote kutoka kwa mchungaji. Uwe mwepesi kuwashuhudia wenye dhambi neno la Mungu na kuwatia moyo wale waliovunjika moyo na kukata tamaa.


2. Wahi kwenye Ibada na Onyesha Uhai Wakati wa Ibada

Huwa inamtia moyo sana mhubiri, pale anapokuwa akihubiri na watu kuonyesha kuwa wapo pamoja naye na wanamsikiliza kwa makini.Onyesha uhai kwa kuitikia, kwa kupiga makofi, kwa kupunga mikono na hata kusimama pale wanapoguswa na ujumbe fulani. Kwanza atajua kuwa kuna watu wanamsikiliza na sio kusikiliza tu bali wanapokea kile wanachohubiriwa. Waweza kushiriki katika kuandaa ibada kwa kushiriki katika kufanya usafi, kupamba kanisa.

3. Muombee Mchungaji Wako

Mchungaji wako anakutana na changamoto nyingi katika utendaji wa kazi ya Mungu na anahitaji sana maombi yako maana kwa kibinadamu ni vigumu kuzikabili. Muombee ili Mungu amtie nguvu, ampe hekima, na kuzidi kumfunulia siri zake kwa ajili yenu ambao mpo chini ya uchungaji wake. Ombea familia yake, mke au mume wake na watoto wake pia.
2 Thesalonike 3:1-2 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.


4. Onyesha Utii Kwa Uongozi Wake

Biblia inaonyesha wazi kuwa ni lazima kuwaheshimu viongozi wetu wa kiroho. Ebrania 13:17 inasema “Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi”
Haipendezi wala haibariki kuwa kinyume na uongozi uliopo chini ya mchungaji wako na kwa yale ambayo anakuagiza kutenda maana yeye ndiye anayekesha kwa ajili ya roho yako.

 
5. Mheshimu
Mheshimu mchungaji wako hata zaidi ya unavyomheshimu mtu mwingine anayekuongoza. Ndio, unaweza ukawa unamazoea ya karibu na mchungaji wako lakini hii haikufanyi ukose heshima, muonyeshe heshima kwa maneno na kwa vitendo iwe ni kanisani au mahali pengine popote hata kama umemzidi kipato, elimu, umri n.k
1 Thesalonike 5:12-13Lakini, Ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.

6. Simama Pamoja Naye Katika Nyakati Ngumu

Rafiki wa kweli ni yule anayesimama nawe katika hali zote za maisha, sio yule anayekuacha pale mambo yanapokuwa magumu. Simama na mchungaji wako katika hali zote, usiwe mshirika wa matukio na mafanikio bali simama naye katika nyakati zote. Mtie moyo pale anapopitia magumu iwe ni katika huduma au kifamilia na kumsapoti kwa hali na mali pia, na sio kusimama pembeni na kumsengenya au kumlaumu.

 
...fuatilia sehemu ya pili wiki ijayo.

Monday, October 15, 2012

WHAT KIND OF HUSBAND ARE YOU?



 How can your wife describe you? Below are few categories of husbands:

(1). Autocratic Husband- He is a self-knowledge, self-involved, unbending, unyielding husband. Nobody can correct him, nobody can counsel him. To him, he knows everything. He is very arrogant and stubborn. He has no mentor. He does not fear, honour or respect anybody. He doesn't want anybody to advise him and he can not be influenced by anybody especially his wife, who hardly knows his plan or what he may do next. He is a difficult man to live with.

(2). Corrosive Husband- He is abusive; hot tempered and a wife beater. He is not in charge of his temper. He is a no-joke, no-play, no-laughter and no-nonsense man. He shouts and barks at home. The house is a military camp; his room is a defence headquarters, while he is the garrison commander, lion of the family and commander in chief of family forces.

(3). Solo Husband- He stays in separate room away from his wife. He is a “single” married man. He prefers sharing his secret with friends; the only time he talks to his wife is when he needs food and sex.

He is self-centered; his common words are “I”, “me”, “mine” and “myself”. He is full of self-glorification, self-justification and stinginess.

(4). Semi-Husbands- They are not real husbands, they are men under their trouser but lesser than that in their duties at home. They are real men in bed and on the dining table; but when it gets to paying school fees they are nothing. It is their wives that pay the house rent, electricity bills, buy food and provide generally for the family. It is not that he is not working; it's just that he is a useless man that will not provide for his own family. While some are too lazy to work, others that have money spend their money outside to the detriment of peace in their homes. A semi-husband is a disgrace, Proverbs 24:27, I Tim 5:8.

(6). Supermarket Husbands- These are the kind of husbands that are unfaithful to their wives. They are everybody's husband. They spend lavishly on their girl friends, woman friends, prostitutes and concubines outside; while giving little or nothing to their household.

To men like this, anything in skirt is good for a bedmate. They pay huge amount of money on hotel bills. They are shameless to the extent that they visit brothels for prostitute or park their cars in the bush path to perform their ungodly act with immoral ladies. Some even go to the extent of impregnating their house-maids and sleeping with their wives' younger sisters, Proverbs 7:1-27

(7). Executive Husbands- These are the kind of men that live their lives in an executive way. They do not allow their wives to have any close relationship with them. They operate their rooms as if it is the general manager's office; no love, no romance and no intimacy.

If their wives want to enter their rooms, they have to knock and obtain permission before coming in. They do issue orders to their family members as if to the workers under them and inform their families about their plans as if addressing a press conference; where no journalist is allowed to ask any question.

Their wives can not easily talk to them, in fact; they have to send their children to them before they can get anything from them.

One thing that is common to most of them is that most of them are business executives hence, they use their office experience to the maximum at home expecting everybody at home to follow suit. They have little or no respect for their wives, if their business is not going on fine, then the whole family is in trouble. Many of them always want their wives to be full-time house wives so that they can have full control over them.

(8). Traditional Husbands- They see their wives as properties. They believe women are third class citizens, useful only in the kitchen and bedroom. To them, a woman is just a cook, a tool of pleasure (sex) and baby making machine.

They give no attention to their wives who they see as somebody that is a little bit above their house-maid. They believe that their younger ones living with them are to be served by their wives, while they are expected not to do anything at home.

Most of them are still using the style of their grand fathers for their marriages. They believe a woman must not enjoy sex; love must not be shown to them, they must be beaten if they misbehave, if she fails to give birth to a baby boy then she is a failure. If they give birth to children who behave poorly they belong to the wife, the one that behave excellently belong to the father.

(9). Baby Husbands- They are not under-aged men physically, but they are infant mentally. They know how to build a house but not how to make a home.

If you want to know baby husbands look for the following:

• He keeps malice with his wife

• He rejects food because he is angry

• He beats his wife

• He reports his wife to friends and family members

• He keeps a separate room from his wife.

• He embarrasses his wife publicly

• He calls his wife goat, animal, fool, etc.

• He loves his mother more than his wife

• May refuse to give house-keeping allowance because of a little misunderstanding

• Can never be influenced by his wife

• He is a contentious husband, he nags.

• Will never pray with his wife

• Always find it difficult to say “I am sorry”.

• Will never help his wife with the baby.

• He threatens his wives with polygamy or divorce

• He criticizes, condemns and compares his wife with other women

• He does not love his wife, if he does; he will never say it, or demonstrate it.

• He leaves the house without anybody knowing where he has gone to.

• He gives no room for romance and intimacy. All he wants is sex.

• Gives no room for foreplay before sex. He is just like a carpenter who has no emotion for the nail.

• He retaliates instead of rewarding

• Never does anything to improve his marriage. He will never read marriage books, attend seminar or go for counseling.

(10). Kingdom Husbands- They are extra-ordinary husbands; they are what God want them to be as husband. They know that their God is to be feared and worshipped, their wives are to be loved and their children are to be catered for. They are “real men”, men indeed; they are the SUNSHINE in the life of their wives and children.

- They are man of integrity: - They mean what they say; and say what they mean

- They do pray with and for their wives.

- They are faithful, loving and caring.

- They cherish and nourish their wives.

- They have hostering i.e. they do listen to the suggestion of their wives.

- They are good communicator.

- Apologize easily, forgive quickly.

- They lead their homes with wisdom

- They never retaliate, they rather reconcile.

- They do speak the truth in love.

- They provide for their family (1 Tim. 5:8)

- They stay in the same room with their wives.

- They “leave” their parent and leave to their wives.

- Their wives know how much they are earning.

- They are actively involved in child bearing, rearing, discipline and parenting.

- They have ultimate respect for their wives.

- They do support their wives in the kitchen.

- They are close to their wives, full of honour and they do play with their wives.

- They are skillful in the bedroom; meeting their wives bedroom need.

Kingdom husbands are not common but God can make you one of them, turning your home to a place to be.

Kingdom Husbands – Traits of an Uncommon Hubby

Kingdom husbands are common men with uncommon sense.
Are you a great husband?
Do you want to be one?
Do you want to be a husband your wife will adore, honor and hero-worship? Then all you just need to do is to develop the following traits of uncommon husbands:

1. God Fearing: The first trait of a great husband is the fear of the Lord. He fears the Lord enough to obey His words. He fears the God enough to care and provide for his wife. No husband can be a wonderful husband expects he is God fearing man.

2. Godly Character: A great husband is of a man with godly character. He is meek, gentle, caring, loving, forgiving, supportive, wise and cautious. He is not stingy but honest. He does not attend night clubs, smoke or practice adultery.

3. Love: He loves his wife with all his heart and is not ashamed to let anybody know. He expresses love to his wife at any given opportunity.

4. Respects and Honors: When you see a man that embarrasses his wife in the public, he is a total failure as a man of valor. A great husband respects and honors his wife and gives all glory to God.

5. Good Communication: A woman loves it when her husband is talking and listening passionately to her. A good husband is open to his wife. He speaks the truth is love and is always positive in his reactions to his wife.

6. Great Leader: He is never a boss but is a tender lover. He knows how to make people follow him without forcing them. He has vision, which he shares with his family. He influences the family and offers them good examples.

7. Diligent: A great husband is a worker; he is not lazy. He puts his hands to work and makes bread available to his family.

8. Romantic: He satisfies his Wife’s Bedroom Desires. A great husband is romantic. He knows how to make his wife enjoy him. He is tender, patient and careful with the wife in the bedroom. He knows that foreplay is a must if a woman must enjoy sex. Hence, he never rush the wife but brings her up before any sexual act.

9. He gives His Wife Peace: The wife of a great husband is always sad to see him travel because he is a man of peace with no space for fighting, bitter arguments, abuse, curse, shouting, malice, bitterness, resentment, bickering and hatred. A great husband has no time for all these. He is a source of joy to his darling wife.

10. He is Committed to Marriage: He never threatens his wife with beating, separation or divorce but is ready to give his marriage anything it takes to make it work. His wife is number one in his life after God. His wife is his thinking partner, friend, prayer partner, bed mate, and confidant!
--------------------------------

This is not meant to abuse anybody, but for you to check yourself and try to be a better husband and father, may God help you in Jesus name.

 


Source: Pastor Bimbo Odukoya

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...