Friday, January 22, 2021

JE,UTAKUBALI SHAMBA LAKO LIKAPANDWA MAGUGU KWA SABABU YA USINGIZI?

 


..lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

MT. 13:25 SUV



Usikubali shamba lako lipandwe magugu na adui kwa sababu ya usingizi.

Usingizi upo wa aina mbili

Wa kiroho na wa kimwili.


Wa kiroho ni pale ambapo unaacha kuwa rohoni yaan unaacha kuomba,kusoma neno,kutenda matendo mema,na kuliishi Neno la Mungu.


Hapo adui shetani kupitia mawakala wake anapata mlango wa kuingia kwenye himaya yako na kupanda magugu(uharibifu).

Yaan anapanda mbegu(wazo) ambalo huenda usijue kama ni gugu ukadhani ni ngano.


Na kwa vile umelala huwezi gundua.


Vyote vinakua na siku moja inagundulika haikuwa ngano lilikua gugu😱


Kila mtu anashangaa kulikoni huyu ndugu kafanya hivi au vile,

Kumbe ni gugu la muda mrefu lilipandwa bila mtu kujua kwa sababu alikua amelala.


Amka mpendaa tuwe macho rohoni kupitia maombi,kusoma neno kila siku,na kulitafakari ili kujilinda na adui anayesubiri tu tusinzie kidogo apandikize mbegu ya gugu ndani yetu.



Umebarikiwa!

Friday, January 15, 2021

OMBI LA LEO:MUNGU AMSHA ROHO ZA WATU WALIOKUSUDIWA KUSABABISHA KUTIMIA KWA NENO LAKO MAISHANI MWANGU MWAKA HUU 2021


 1.Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 


 5. Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu.

EZR. 1:1‭, ‬5 SUV


✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻

Omba Mungu aamshe roho za watu ambao wamekusudiwa kutumiwa nae kutimiza Neno lake maishani mwako



Ili kupenya maishani inahitajika watu Mungu aamshe roho zao watumike kukubariki,

Watumike kukuvusha mahali,

Watumike kukusemea mahali upate kibali,

Watu waamshwe roho zao watoe pesa zao,muda wao, mawazo yao kwako ili uvuke kwenda hatua nyingine ya maisha.


Ili kusudi la Mungu kwako 2021 litimie unahitaji watu.


*Na hao watu ni mpaka Mungu awe ameamsha roho zao kutenda kwako,* hawawezi kutenda tu hivi hivi.


Ombi letu leo,

Ee Mungu wangu amsha roho za watu waliokusudiwa kutenda kwangu ili Neno lako kwa mwaka huu 2021 litimie kwangu.


Hii ni kanuni mojawapo ya kiroho ya kusababisha mambo kutokea katika eneo/jambo lako lolote.

Omba Mungu aamshe roho za waliokusudiwa kukusaidia uvuke hapo ulipo.


Umebarikiwa!

UMESHAANDIKA MALENGO YAKO YA 2021?

Shalom Msomaji wangu.

Pokea salamu za mwaka mpya 2021!



Naamini kila mmoja wetu ameshaandika malengo yake ya 2021.

-kiroho

-kiuchumi

-kimaendeleo/uwekezaji

-kitaaluma/career

-kibiashara

-kiafya

-kihuduma


Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

Mithali 16:1 NEN


Wengi wanaishia kuwaza tu.

Ni vizuri *kuandika*


Na kuyaweka mahali ambapo utakua unayaona mara kwa mara.


_Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi: *“Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma.*_

Habakuki 2:2 BHN


Unaweza kuandika na kuyabandika mahali ambapo utakua unayaona kila siku.

Ili ukumbuke kutafanya isifike june ukawa umeshasahau na umeendelea na mambo mengine ambayo hayakuwa kwenye malengo yako.


Au kwenye diary ambayo unaitumia kila wakati ili ufunguapo uwe *unayaona*



*Kwa nini uandike?*

1.Itakua kufocus kwenye kile ulichopanga na hutatoka nje ya mstari.

2.utakumbuka na hutakua na kisingizio kwamba ulisahau.

3.ili uwe unajipongeza kila unapotimiza lengo mojawapo ya uliloandika.


Kuna watu hapa wanaandika malengo ya makampuni wanayofanyia kazi na mpango mkakati wa kuyatimiza lakini hajiandikii ye mwenyewe malengo yake ya mwaka na hana mpango mkakati binafsi.

Kama kampuni ingekua genius ingeandika kichwani isingeweka kwenye maandishi.😜

Ndio maana mwaka ukiisha ukimuuliza mtu ulifanya nini mwaka huu anakwambia hata sioni..zaidi ya kula tu asubui mchana jioni😃


Au akienda sana atakutajia kitu kimoja au viwili tu.

Kweli miez 12 umepewa na Mungu kufanya kitu kimoja au viwili tu! Si ni utumiaji mbaya wa muda huo?

Hayo yanatokea kwa sababu malengo hayaandikwi.

Na yakiandikwa notebook inawekwa kabatini kujaa vumbi.


Hayatengenezewi mkakati wa namna ya kufanyika,hivyo hayawez kutokea tu..lazima yasababishwe kutokea.


Mwaka 2021 TUAZIMIE KUWA NA MALENGO YA KUELEWEKA NA TUWE NA MPANGO MKAKATI WA KUYATIMIZA.


 Unaweza kutumia mchanganuo kama nlioweka mwanzo au ukaongezea vingine kulingana na wewe mwenyewe.


Hii ndio siri mojawapo ya waliofanikiwa!


Uwe na siku njema!

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...