Thursday, May 2, 2013

PRESS CONFERENCE ILIYOFANYIKA LEO TAR 02 MAY 2013 IKIWA NI MAANDALIZI YA AFLEWO TAR 03 MAY 2013

Tukiwa katika countdown ya kuelekea AFLEWO, yakiwa yamebaki masaa machache kuelekea tukio ambalo limesubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa jiji la Dar na mikoa ya jirani, baadhi ya wanakamati wa AFLEWO walikua na Press conference na waandishi wa habari kuelezea nini hasa kitajiri katika AFLEWO siku ya Ijumaa tar 3 May 2013, pale BCIC Mbezi Beach kwanzia saa tatu usiku mpaka baadae.

 Mwaka huu 2013 kutakua na wageni toka Mwanza, Moshi na Zanzibar wanaokuja pia kujifunza Aflewo Ilivyo Kisha wanakwenda kuandaa AFLEWO kwenye mikoa yao.

Maono ya mwaka huu ya AFLEWO yakiwa ni kujenga madhabahu ya Mungu katika taifa letu.

Walio Pichani Kushoto ni Samuel Sasali, Mkurugenzi wa Habari Aflewo, Bishop Freddie Japhet Kyara Mlezi Wa Aflewo Tanzania, Pastor Paul Safari Mlezi wa Aflewo Tanzania, na Samuel Rodin Mwangati Music Director wa AFLEWO.

 
 

 

 
 

 
 
USIKUBALI KUKOSA!
 

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...