MAFANIKIO NI HATUA ni segment mpya katika blog ambayo ina lengo la kukuhabarisha, kukufikirisha na kukuchangamotisha wewe msomaji kuhusu nini maana ya mafanikio, juhudi mbalimbali ambazo hufanywa na watu waliofanikiwa, njia ambazo yapasa kuzifuata kuyafikia mafanikio yako,kwa nini watu wengi hutamani kuafanikiwa lakini hawafikii yale mafanikio..fuatana nami hapa hapa blogini! Na leo nataka nikufikirishe zaidi..
Kama wanadamu kila dakika inayopita huwa tunafanya maamuzi ya kile tunachotaka kuwa, maamuzi ya kufungua biashara mpya, kuanzisha kampuni, kuwa mjasiliamali, kuwa mkulima ,kutafuta kazi nyingine, kuoa/ kuolewa, kujenga nyumba nyingine, na kadhalika na kadhalika.
Kaa ukijua kuwa, njia yoyote utakayoichagua, kumbuka kuwa hutakua peke yako, ushindani sio kitu cha kuchagua ni lazima utakutana nao. Namna mbalimbali za kufanya vitu zilishavumbuliwa miaka mingi iliyopita, na hata hicho unachofikiri kufanya hakitakua kipya chini ya jua.Tayari kuna mtu alishawahi kufikiri kufanya hivyo pia!
Hebu tufikiri pamoja, kwa mfano unataka kufungua biashara ndogo ya kuuza matunda, na una kila malighafi inyohitajika.Matunda unayo na una namna ya kuyapata huko baadae, vifungashio unavyo,na unafikiri itakua ni biashara nzuri sana.
Kabla hujachukua hatua ya kuanza biashara yako,unatafuta eneo ambalo ndio utakua unafanyia biashara zako. Eneo ambalo unapata, tayari unakuta kuna mtu anafanya biashara kama ile ile ya kwako unayowaza kuja kuifanya hapo!Je, utabadilisha mawazo na kufanya biashara nyingine?
Kama uko focused, hutaacha, kwa sababu hiyo ndio njia unayotaka kuiendea.
Kuna wakati katika maisha tuna pita na kukanyaga kule ambapo wengine wamepita na kukanyaga,tunaishi yale maisha ambayo wengine wameishi, lakini ukweli ni kwamba,haijalishi ni watu wangapi wanaonekana kufanya kile ambacho wewe unataka kufanya, haijaishi ni hatua ngapi unaziona zimeshakanyaga pale unapotaka kukanyaga,hakuna anayeweza kukanyaga kama wewe. Hakuna anayeweza kufanya vitu kama ambavyo wewe utafanya.Kwa sababu tumeumbwa tofauti, na kila mtu ana kitu cha tofauti ndani yake. Haijalishi wanaouza matunda ni wangapi, lakini hawafanani, huduma zao hazifanani, haijalishi mafundi vyerehani wako wangapi, lakini hawafanani, kila mmoja ana kitu chake unique.
Njia utakayoichagua ni njia yako, haijalishi ushindani utakao kuwepo, as long as you are sure that it is your path, follow it!
Katika kufanya uamuzi wa kuifuata njia ulioichagua, kuna changamoto ambazo utakutana nazo.. ungana nami wiki ijayo hapa hapa kwenye blog ntakapoongelea changamoto hizo.