Wednesday, February 27, 2013

10 YEARS MAZNAT ANNIVERSARY! ( An interview with the Founder of Maznat Bridal)


 
Kwa wakazi wa Dar es salaam na hata nje ya Dar, jina la Maznat halitakua geni masikioni mwao.
Ni safari iliyoanza mwaka 2003 kwa mwanzo mdogo, ambao kwa macho ya kawaida usingejua kama ingefikia leo.
MAZNAT BRIDAL inachukua nafasi hii kukualika wewe mdau wa tasnia ya urembo au beauty industry, wewe uliyewahi kuwa bibi harusi, ukapambwa na Maznat, wewe bibi harusi mtarajiwa na kila mwanamke mjasiliamali kwenye anniversary au sherehe ya kufikisha miaka kumi (2003- 2013)
 
MAHALI: JIAMOND JUBILEE
SIKU: 5 MAY 2013
MTUPIO: KITENGE CHA KANTE( kinapatikana Mazant Bridal Mikocheni)
WAIMBAJI WATAKAOKUWEPO: Bahati Bukuku, The Voice na wengine.
Kwa mawasiliano: 0752 666670, 0783 444470, 0718 818999
 
Zawadi itatolewa kwa bibi harusi aliye na watoto watatu na bado akaweza kuvaa gauni lake la harusi.
Gauni 3 za harusi zitatolewa kwa bibi harusi watarajiwa kama zawadi.
Christian Bloggers tulipata nafasi ya kupata breakfast pamoja nae naye alikua na haya ya kusema:
 
Bloggers: Ulianzaje Maznat hadi imefika hapa ilipo?
Maznat: Tulianza nyumbani na wakati mwingine nlikua nafanya bure, baadae tukaahamia kwenye chumba kimoja, na nlikua nawapamba na kuwatengeneza marafiki zangu na waumini wenzangu kanisani. 
Bloggers:Nini siri ya mafanikio yako?
Mazant: Kwa kweli nakiri kuwa ni Yesu tu ndie aliyeniwezesha kufika hapa nilipo leo. Lakini pia consistance and courage. Sikuwai kuacha kufanya kazi hata kama sikupata faida siku hiyo, niliendelea tu. my motto always is; "if you can dream it you can have it".
Bloggers: Mafanikio gani ambayo umeyapata?
Maznat: Mafanikio yako mengi sana, namshukuru Mungu kwa hilo. Kwanza nimeweza kujenga mahusiano na watu, nimefahamiana na watu wengi, nimetengeneza ajira kwa watu wengi, nimebadilisha pia mtazamo uliokuwepo juu ya beauty industry.
Bloggers: Kila penye mafanikio kuna changamoto. Ni changamoto gani umekutana nazo katika safari hii ya miaka 10 na Maznat?
Maznat:Bidhaa feki, ni changamoto kubwa sana ambayo tunakutana nayo, na ili kupata bidhaa original nna lazimika kusafiri mwenyewe kwenda kuzileta. Pili, wateja wanakua hawapo tayari kulipia huduma nzuri na bidhaa original. Utamhudumia mtu vizuri, alafu ikifika saa ya kulipa inakua usumbufu, na umetumia product original.
Bloggers: Saluni nyingi wana kawaida ya kubadilisha wafanyakazi, vipi wewe?
Maznat: Mimi kwa kweli nakaa sana na wafanyakazi wangu, siri kubwa ni kuwajali. Mimi nimewafungulia saccos, nawalipa vizuri kwa hiyo mtu hawezi kuondoa mahali ambapo anauhakika na maisha yake.
Bloggers: Umewahi kusomea au kwenda shule ya beauty?
Maznat:Ndio. nimesomea, nna diploma ya beauty, lakini pia mimi ni Mwanasheria by Proffession, nna Masters ya Sheria, na pia nimesoma Certificate ya Human Resource ambayo pia imenisaidia kujua namna ya kuongoza wafanyakazi wangu.
Napenda tu kusema, Biashara ukiwa umesoma ni rahisi zaidi ukilinganisha na mtu anayefanya biashara akiwa hajasoma.
Bloggers: Tuambie kuhusu hii miaka 10 ya Mazanta Bridal.
Maznat: Kwanza ni siku ya kumshukuru Mungu kwa Maznat Bridal kufikisha miaka 10, tangu mwaka 2003 hadi leo sio safari ndogo. Siku hito tunatarajia takribani wanawake 800, wakiwepo ma bibi harusi waliowahi kupambwa na Maznat, ma bibi harusi watarajiwa, wateja wooote wa Maznat, wajasiliamali wanawake na wanawake woote wa jiji la Dar.
Wajasiliamali watasikia jinsi Maznat ilivyoanza hadi hapa ilipofikia.
Bloggers:Je, kuna kiingilio?
Maznat:Kiingilio ni elf 50,000/= tu, pamoja na kitenge cha sare aina ya kante.
Bloggers: Itaanza saa ngapi?
Maznat: Itaanza saa tisa mchana hadi saa tatu usiku.
Bloggers:  Unawezaje kubalance familia na kazi?
Maznat: Kwa kweli namshukuru Mungu familia yangu inanipa full support, nina mume very inteligent and very supportive. Napata full support kutoka kwenye familia yangu.
Bloggers: Una neno gani la mwisho la kuwaambia wasomaji?
Maznat: Nawaambia waje hiyo tarehe 5 May 2013,pale Diamond Jubilee, kutakua na mambo mengi sana mazuri. Wajasiliamali wanawake waje wasikie ushuhuda wa Maznat ilipotoka hadi hapa ilipo.Nawakaribisha wote. 
Bloggers: Asante sana.
Maznat: Asante sana.
 
Maznat mwenyewe akifafanua jambo

Bloogers wakisikiliza kwa makini.

Kikao kikiendelea

 

kulikua na chaiiii


Christian Bloggers katika picha ya pamoja baada ya kikao.
 
 

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...