Tuesday, July 17, 2012

FAMILY BUSINESS SUCCESSION/KURITHISHA BIASHARA YA FAMILIA



Hii ni aina ya biashara ambayo inakua inamilikiwa na familia na nyingine huwa na baadhi ya watu wachache ambao sio wana familia.

Inawezekana wewe ni kijana unayesoma makala hii, pengine hata huna familia, na hata malengo ya kuwa na biashara pia huna, lakini ipo siku kwenye safari yako ya maisha utakuwa na familia, ana utakua na biashara na itakua faraja ya ajabu kuona biashara yako ikiendelea hata kama wewe hutakuwepo (going concern),hivyo utahitaji kurithisha familia yako, makala hii itakua akiba kwako. AKIBA HAIOZI!

Famiily business zipo sehemu nyingi sana Duniani,kuanzia MAREKANI, ULAYA, ASIA NA AFRICA, na kampuni nyingi sana Kubwa duniani ni za familia, zinamilikiwa na familia pamoja na kwamba zinakuwa na watu wengine nje ya FAMILIA.

HAPA CHINI NI BAADHI YA KAMPUNI KUBWA DUNIANI ZINAZO MILIKIWA NA FAMILIA, INGAWA ZINA WANAHISA(SHAREHOLDERS) WENGINE AMBAO SI WANAFAMILIA.
Company
Rank
Wal-Mart Stores
1
Ford Motor Co.
2
Samsung
3
LG Group
4
Carrefour Group
5
Fiat Group
6
Ifi Istituto Finanziario Industriale S.p.A.
7
PSA Peugeot Citroën S.A
8
Cargill Inc.
9
BMW (Bayerische Motoren Werke AG)
10
Hyundai Motor
11
Koch Industries
12
Robert Bosch GmbH
13
SCH (Banco Santander Central Hispano S.A.)
14
ALDI Group
15
Auchan Group
16
Pinault-Printemps Redoute
17
Ito-Yokado
18
Tengelmann Group
19
J Sainsbury
20
Motorola
21
Viacom
22
Novartis Group
23
Tyson Foods
24
Bouygues
25
Roche Group
26
Bertelsmann
27
Weyerhaeuser
28
Loew’s
29
News Corp.
30


KWA NINI FAMILY BUSINESS NYINGI SANA KWA TANZANIA HUFILISIKA  NA KUFA MARA TU, MMILIKI ANAPO UGUA, KUFARIKI AU KUZEKA?

Zipo sababu nyingi zinazofanya biashara nyingi zinazomilikiwa na familia kufilisika au kufa mara baada ya mwanzilishi kuugua,kuzeeka au kufa.Biblia intuagiza kuwaachia watoto urithi (mithali13:22   Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; bali mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.) 

1.KUKOSEKANA KWA MAANDALIZI


Wafanya biashara wengi huwa hawana Utamaduni wa kuwaandaa watoto wao kwa ajili ya kurithi biashara, na matokeo yake ni wao wenyewe kuendelea kuendesha biashara hadi uzeeni, KUKOSEKANA KWA MAANDALIZI HUPELEKEA KUFA KWA BIASHARA NYINGI ZA FAMILIA.
Lakini pia watu wengi huangamia kwa kukosa maarifa.Yapasa kujua(Maarifa) kuwa uko umuhimu wa kuwaachia watoto urithi, ikiwa ni pamoja na kuwaandaa tangu mapema.
Si vizuri maandalizi kufanyika kwa haraka(Zima Moto) hiyo hufanya mrithishwaji kushindwa kuwa na ujuzi na uzoefu wa kutosha kuendesha biashara.
Biashara hufa pia kwa sababu mtu anaye chaguliwa kurithi biashara au kusimamia anakuwa hana Elimu wala uelewa kuhusu biashara za baba yake na matokeo yake ni kuongoza anavyo jua yeye na mwisho kufa kwa biashara yenyewe.kwa mfano baba ana kampuni ya uzalishaji bidhaa, mtoto kasomea udaktari,hapo moja kwa moja huyo mtoto hawezi kurithishwa biashara na akaiendeleza kwa sababu hana ujuzi wa elimu kuhusu biashara hiyo.


Tunaona kwenye biblia hata wakati Mussa anaongoza safari ya wana wa Israel, Joshua alikua mmoja kati ya watu wa karibu sana na Mussa.
Alikua akijua kila Mussa alichokua anafanya.Hata ilipofika wakati wa yeye kuendelea na safari ya kuwaongoza Waisrael, haikua shida kwa sababu tayari Mussa alishamuandaa, na tunaona jinsi Joshua alivyo waongoza Waisraeli na wakafika kwa ushindi.(Joshua1-).

2. UENDESHAJI WA BIASHARA KIUCHAWI/KWA KUTUMIA NGUVU ZA GIZA/WAGANGA

Ni ukweli kabisa kwamba baadhi ya matajiri wa Tanzania ukifuatilia historia za biashara zao na jinsi wanavyo ziendesha utagundua kwamba, zinaendeshwa kwa NGUVU ZA GIZA, unakuta kuna mashariti kibao,LIKIWEMO LA TAJIRI KUTOA KAFARA, TAJIRI KUTORUHUSIWA KUTUMIA VITU VYA ANASA N.K.

Kutokana na hilo biashara nyingi sana hufa mara tu mmiliki anapofariki.Hata biblia inasema Mungu anasema hilo ni chukizo kwake hivyo atawaangamiza watu wa jinsi hiyo (kumb10:12). Si ajabu, kuona kuwa biashara nyingi hufa, ni kwa sababu hazifuati misingi ya kiMungu katika kuziendesha.


3. UGOMVI WA KIFAMILIA (FAMILY CRISIS)

Hii ni moja ya sababu kuu ya family business nyingi sana kufa, Mara tu baada ya Baba/Mama kufariki, huanza ugomvi mkubwa sana wa kugawana mali za baba/mama, Na huu ugomvi ni matokeo yakutokuwepo maandalizi mapema ya nani ataongoza biashara za famailia,na mali zilizopo.
Wenzetu wazungu wameendelea, kwao ni jambo la kawaida kwa mtu kuandika wosia hata kama hajazeeka. 
Waafrika bado hatujafunguka, mtu anaona akiandika wosia ni kama anajiuombea kufa mapema. Wosia ni muhimu sana kwa familia,vinginevyo wazazi huwa wanawaacha watoto katika hali ngumu pale wanapoondoka ghafla.
Mungu ameamuru Baraka mahali watu wanapoishi kwa pamoja kwa umoja
(zaburi 133:1-3) 


4. UKUBWA WA FAMILIA(POLYGAMY FAMILIES)

Hii hutokea hasa kwa familia zenye wake zaidi ya mmoja (poligamy families).Ukubwa wa Familia nao ni sababu kuu ya Biashara nyingi za familia kufa, Mara baada ya Mwanzilishi kuchoka au kuugua,Watoto wa mmiliki na wake zake huanza michakato ya kugawana mali na kwa kuwa familia ni kubwa sana hujikuta wana ua kampuni na kugawana kila mtu cha kwake.

5. UTENGANO KATIKA FAMILIA(FAMILY SEPARATION).

Hili ni tatizo pale ambapo Baba/Mama anaendesha biashara katika eneo lingine na watoto wanakaa mbali, hivyo watoto kushindwa kuwa karibu na biashara na kujifunza kile baba/mama anachofanya, hii hutokea hasa pale ambapo wanandoa wametengana hivyo kufanya watoto kukaa mabali na wazazi.

7. KUFANYA BIASHARA ISIYO HALALI(ILLEGAL BUSINESS)

Ni wazi kuwa kama familia inafanya biashara ambayo si halali si rahisi kwa wazazi kuwarithisha watoto,kwani mzazi anajua wazi kuwa anachokifanya ni halali kwa sheria za nchi na hivyo hufanya kimaficho.Hivyo basi kuplekea watoto kutokiujua hasa baba/mama anafanya biashara gani.
Mwishowe mtu hyo akizeeka/kufa na kile alichokua anafanya hufa pia.

JE NI ZIPI NJIA SAHIHI AU NJIA NZURI ZA KURITHISHA BIASHARA?


1. ANZA KUANDAA FAMILIA YAKO MAPEMA



Anza kwa kuiweka familia yako katika mkao wa kuja kurithi BIASHARA ZAKO MARA TU UTAKAPO KUWA HUNA NGUVU, UMEZEEKA AU UMEFARIKI. hii ninzuri ili kuwepo na muda wa kutosha wa watoto kujifunza na kupata uzoefu wa namna ya kuendesha biashara.
Familia ni lazima waafikiane nani atakua mrithi wa kuongoza biashara yao, haihitaji siri yoyote hapa.Kila mwana familia lazima ajue fulani ndiye atakae kuwa msimamiaji wa biashara na kukubaliana na hilo.hiyo itaondoa mgogoro pale ambapo muda wake ukifika wa kusimamia.

2. ANZA KUMUANDAA MURITHI KISAIKOLOJIA



Warithi wa BIASHARA huandaliwa MAPEMA sana na sio swala la ZIMA MOTO, namara nyingi kwa watanzania warithi wa biashara hupatikana kwenye kikao cha familia mara tu baada ya msiba, na hapa ujuzi huwa hauzingatiwi.

Mpe mazoezi ya vitendo ikiwa ni pamoja na kumwachia afanye baadhi ya shughuli mwenyewe.mrithi anatakiwa aandaliwa.


- KIELIMU- apewe elimu inayo husika na biashara za Baba, na Mtoto asishauriwe kusoma medicine wakati anatakiwa kurithi Biashara hapo moja kwa moja anatakiwa kusomea kuhusu usimamizi wa biashara.


- KISAIKOLOJIA- Ni lazima aadaliwe kisaikolojiaili ajue jinsi ya kusimamia hiyo kazi,

3. ANZA KUANDAA DOKOMENTI ZA KURISISHA MAPEMA



Ni vizuri Dokoment za kurisisha zikaanza kuandaliwa MAPEMA SANA ikiwemo na kuwatumia wanasheria kuziandaa na kuanza kubadili Majina ya Umiliki wa Biashara kutoka wew kwenda kwa uliye muandaa au familia yako.

4. PANGA KABISA NA LINI UTAMUACHIA MRITHI MAJUKUMU

Hapa watu huzani ni Mpaka Mmilikia Afe/augue/azeeke ndo arisishe, Hapana,unatakiwa kabisa kupanga Tarehe na wakati wa kukabidhi majukumu na wewe kupumzika Nyumbani na kula matunda ya kazi yako.

5. MTAMBULISHE MRITHI WAKO KWA MARAFIKI WAKO WABIASHARA/WAFANYAKAZI

Ni vizuri marafiki wako wa biashara wakajua MRITHI wako mapema. Ili kurahisisha kuendelea kwa biashara na sio yeye kuja kuanza tena moja.


Tujifunze kwa wenzetu WAHINDI. Hao ni moja kati ya watu wenye mafanikio kwenye FAMILIY BUSINESS SUCCESSION ndIo maana ni vigumu kukuta Mtoto wa Kihindi akitafuta kazi, wengi wao wanasoma kusaidia Biashara za BABA ZAO, na wengi wao wanasomea Kozi ambazo zinaendana na Biashara za WAZAZI WAO.

NB:  Mithali 22:6 ...mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.




Email:firmina.matee@gmail.com

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...