Friday, April 1, 2016

SUMMARY YA KITABU CHA RUTHU.

 

 UTANGULIZI:


 

 
Kitabu cha Ruth kinasadikiwa kuandikwa na Suleiman au Daudi kutokana na kuwepo kwa baada ya maneno ya watu hawa.
 
WAKATI: Kiliandikwa wakati wa Waamuzi katika Israel.
 
UKUBWA:Kitabu cha Ruthu kina Sura 4!
 
 
SURA YA KWANZA:
Tunamwona kulikua na njaa katika Israel hivyo bwana mmoja aitwae Elimeleki na familia yake wakawa wanakimbia njaa..😩🏃🏃🏃👨👩👦👦
 
Wakaenda katika nchi ya Moab.umbali wa kama mile 30 au mwendo wa siku 7-10 kwa kutembea..🚶🚶🚶🚶 akiamini kupata chakula huko🍹🍞
 
Walikaa huko na Elimeleki akafa.
Wale wanae wawili wakao wanawake wa Moab..Opra na Ruthu.💃💃; wakaishi miaka 10 ya ndoa.
 
Baadae wale wanawa Naomi nao wakafa.💀
 
Akabaki  Naomi na wakweze.
 
Naomi akaamua kurudi KWAO Bethlehem maana alisikia Bwana ameutembelea mji kwa chakula(njaa imeisha)😋🌽🍇🍎.
Nacho kilikua kipindi cha mavuno.
 
 
FUNZO:
Elimeleki alikimbia mbali na Mungu(nchi ambapo Mungu aliwapa) kwa sababu ya njaa na badala ya kufanikiwa alikoenda aliishia kukutwa na mauti yeye na wanae..
Tunaona pia Abraham alikimbia njaa kufika Misri mkewe nusu wamuoe,Mungu akaingilia kati😳
Mwana mpotevu nae alikimbia nyumbani akidhan ataenda kufanikiwa zaidi huko mwishowe alirudi hom mikono mitupu🤔

 Uweponi mwa Mungu ni mahali salama hata kama tunaona mambo ni magumu,,tuchikilie tu Bwana atakukumbuka tuuu..huko Moab hakuna jema😟

KWA UPANDE WA MAMA MJANE-NAOMI.
 
Wakweze Naomi walikubali Kwenda nae Bethlehem,ila Naomi aliwasihi sana wabaki maana walikua bado wadogo hivyo walipaswa waolewe nao wawe na familia zao.
Mkwewe mmoja(Opra) akakubalkubaki🙋
Lakini mkwewe wa Pili(Ruthu) akakataa..akataka Kwenda na Naomi.
 
NAOMI
Alikua mwanamke aliyemjua Mungu wake,aliyeishi kwa Upendo na wakweze na kuwajali na kuwatendea mema.
maana waliishi nae zaidi ya miaka kumi,na bado walitaka kuendelea kuishi nae👍
Hata ulipofika wakati wa kuachana nae ikawa ngumu.
 
 
FUNZO:
Mwanamke anayemcha Mungu hutachoka kuishi nae.
Kwa kuwa Moyo wake wakati wote umejaa upendo na ukarimu.
 

 SURA YA PILI:

 Naomi na Ruthu wamefika Bethlehem ni kipindi chmavuno🌽🍇🍎
Lakini wao hawakuwepo nchini kwa miaka mingi hivyo hawakua wanacha kuvuna🤔
 
Ikabidi waende kuokota masazo kwenye mashamba ya watu(ILIKUA DESTURI kwa Waisreal kuwa kipindi cha mavuno walipaswa kuacha mabaki ili wahitaji na wasiojiweza waweze kupita kuokota mabaki lau wajipatie chakula)🍠🌽
 
Hivyo Naomi akamwambia mkwewe Ruthu akafanye hivyo.
Ruthu akatii..
akaenda..kweli akapata masazo🍒
 
Na akaenda akiokota hadi akafika shamba la Boaz(ndugu wa Mume wa Naomi)👴
 
Ndipo Boaz katika kufanya Partol akamwona Ruthu..akauliza huyu nani!? Akaambiwa kuwa ni nkwewe Naomi Mke wa Nduguyo!
Ndipo akamruhusu kukusanya masazo katika shamba lake.
 
KESHO yake Ruthu akaruhusiwa kukusanya tena zaidi na akaambiwa asiende shamba lingine awe anakuja kukusanya shambani kwa Boaz tu😉😉😉☺ ☺
Na akakusanya masazo yapatayo EFA moja(sawa na ujazo wa njoo ya Lita 22)🌽🌽🌽🌽🌽🌽🌽🍠🍠
 
lakini pia tunaona Boaz alikua tayari na CV ya Ruthu(2:11) 📝 na habari ya Yale Ruthu aliyomtendea Naomi.
 
 
FUNZO:
 Tusichoke kutenda MEMA kwa watu Mungu alioweka maishani mwetu..kwa sabbu hujui ni yupi Mungu atamtumia kama mlango wa Baraka kwako.
Watu wanaambiana!
Unapotenda mema au mabaya kwa MTU,huwa anasema.
Naomi aliwaambia watu wa kwake Yale Ruthu aliyomfanyia japokua Ruthu hakujua lolote😊

 
SURA YA TATU:
😀Hapa tunaona WEMA unajibu!
Naomi anamrudishia Ruthu 'fadhila'💃
Naomi anampa Ruthu 'mchongo' wa kutoka kimaisha😀😀😀
Ruthu anafuata maelekezo yooote bila kuongeza chumvi😉 😉
Ila tunaona pia baada ya Boaz kuelewa ndipo anamwambia Ruthu kuwa atafanya kama ilivyodesturi.
WAKATI ULE  mwanamke akifiwa na mumewe ndugu qa karib hununua like shamba pamoja na Mke na kuwamiliki.
Hivyo Ruthu Kwenda kwa Boaz usiku ilikua ni kutengeneza mazingira ya ile desturi kufanyika sawa na maelekezo ya mkwewe!
 
FUNZO:
 Wema hauozi!
Naomi aliamua kumrudishia Ruthu wema.
Maandalizi yanapokutana na Fursa huzaa bahati🤓

Ruthu alijiandaa kwanzia kwenye kutenda mema Mpaka kujiandaa kabla ya kuingia kwa Boaz====ndipo fursa ilipojitokeza,Ruthu akapokea sehemu yake💃😊
 

SURA YA NNE:
 
Ndipo Boaz akaitisha kikao cha kununua ardhi ya Naomi pamoja na yeye na mkwewe.👭🙇
Ndugu aliyekua wa karibu zaidi kwa Elimeleki akakataa kununua,,ndipo Boaz aliyekua anafuatia kwa ukaribu,akakubali kulinunua!
🤑🤑 akanunua shamba pamoja na Mali zake zote(Naomi na Ruthu) 😆😆
Boaz akamchukua Ruth kama mkewe,
Tangu siku ile maisha ya Ruth na Naomi yakabadilika😀😀😀 😀
Boaz na Ruth wakajaliwa mtoto mmoja wa Kiume wkaamwita Obedi(amabe alikuja kuwa babu yake Daudi)
Na Naomi akawa mlezi wa Obedi mjukuu wake😊😀😆
 
 
BOAZ:
 
Alikua mtu tajiri sana,
 
Alikua na hekima, ( tunaona hakumwingilia tu Ruthu Bali alifuata desturi,pia alipoitisha kikao hakusema kama alimtaka Ruth Bali aliwaambia ni habari za kuuza shamba)
 
Alikua mkarimu ( alimruhusu Ruthu kuendelea kukusabya masazo shambani mwake)

 ========
MWISHO
========
~Na Mwl Minna.
 
Facebook: minna matee wa victor.
Watsap: +255 753 008 212
 
 
(Karibu katika program ya kujisomea Biblia, kama unataka kuwa sehemu ya kundi hili unaweza kuwasiliana nami kupitia email, Watsap au facebook address hapo juu)

Friday, January 15, 2016

NEW YEAR,NEW PAGE!



Happy new year my precious reader,

It has been a while since I wrote here in my blog, and God has been God to me as He has granted me another opportunity to speak to you through my fingers and your eyes as we ponder together the secrets of the Kingdom of God!

Today I want to wish you a very very prosperous year that we have just started, and to encourage you to be expectant of blessings that are prepared your way for this year.

Every new year is like a blank new page waiting for someone to write in it.



What you decide to do in this new year will write into the new page and make it a chapter.

The page may remain blank for months until you take a  pen and write.

One simple secret of writing on this page is by setting GOALS.



Goals are roadmap towards success.

Without goals success will remain a dream never come true.

Set goals and set them "SMART-ly""

SMART goals are Specific, Measurable, Attainable, Relevant and has a Time frame.

Every day make sure you do something towards achieving your goals.

Every month do an evaluation of how far you have reached towards accomplishing those goals.

By doing that, you will find yourself achieving your yearly goals!

See you then, in the process of writing in the page of 2016...

again,
HAVE A VERY PROSPEROUS YEAR 2016!

~Minna


Monday, November 2, 2015

Unapoanza kuona Majitu,,jua unakarikibia kuingia Kanani!!






Kama bado hujaanza kuona majitu, bado una safari ndefu..kwa sababu majitu yako Kanani sio jangwani!!

Unapoyaona sasa, usijione kama panzi mbele yao, kwa sababu ndivyo watakavyokuona pia!!!

Majitu yasikutishe,,kwa sababu uliye naye ana nguvu kuliko hayo majitu!!

Usisahau kuwa Kanani kuna Maziwa na Asali,,sio majitu tuuu!!!

Hayo majitu ni ya muda tu, na unapaswa kuyaangamiza, na umepewa uwezo wa kuyaangamiza, ili upate hayo Maziwa na Asali ya Kaanani!!!

‪#‎NenoLaMunguTamuuu‬#

~Mwl Minna

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...