Friday, September 14, 2018

Nini kinaendesha maisha yako?


Wengine, ni Hatia.

Mtu anaishi chini ya hatia kwa sababu ya mambo aliyofanya nyuma au aliwahi kufanyiwa!


Anaishi akiwa na majuto na aibu ya Yale yaliyotokea zamani!
Anaruhusu jana yake kuitawala Leo yake na kumfanya asione mwanga wa kesho!

Anajiadhibu mwenyewe na kuteka mafanikio yake mwenyewe,

Ni kweli tu matokeo ya jana zetu,lakini sio ticket ya kuwa mfungwa wa jana yako!
Kusudi la Mungu kwako halifungwi na jana yako,




#Alimgeuza muuaji Musa kuwa kiongozi mzuri wa Waisraeli,

#Alimgeuza Gideoni mnyonge,kuwa mtu hodari na mkuu.

Mungu amebobea kwenye kuwapa watu mianzo mipya(mwanzo mpya)

Yeye ni mtaalamu kwenye hilo eneo!

Unamkumbuka Sauli kwenye agano jipya,
Kama kuna mtu asingefaa kabisa alikua ni yeye,, Ila Mungu alimgeuza kuwa mtumishi wake mkubwa sana,,na Leo hii tunasoma kitabu cha Agano Jipya ambacho sehemu kubwa ya zile barua aliziandika yeye! 

Unadhani kesi ya imeshindikana??? Hapana!

Mruhusu Mungu akuoneshe sababu ya yeye kukuweka hapa duniani,usiishi tena chini ya hatia bali uishi maisha yanayoongozwa na kusudi la Mungu.

@minna_book_club_tz
@minna_blessed
# TunaendeleaKusoma
#ReadingMarathon
#JoinTheClub
#YouAreNotLateForSeptemberReading

MINNA BOOK CLUB BRINGS YOU....

Tayari Mungu alishapanga uzaliwe lini,uzaliwe wapi,na hata wazazi gani uzaliwe kwao.

Inawezekana kwa wazazi wao waliona umezaliwa nje ya ratiba yao,ila kwa Mungu huo ndio ulikua muda sahihi kabisa wa wewe kuzaliwa!

#UmeumbwaKwaKusudi
#Karibu tusome pamoja

NI HATARI SANA!

Ni hatari sana huo mwavuli wa juu kabisa unapokua haupo,,pale husband anapokua wa mwisho anakua kwenye hatari kubwa sana,

Ni hatari sana kama hiyo miamvuli miwili ya juu haipo,,wife anakua danger zone,, Na ni hatari zaidi kama hiyo miavuli mitatu ya juu haipo,child anakua kwenye hatari isiyoelezeka!

Familia yoyote isiyo na Mwavuli wa Kristo ipo hatarini kupatwa na lolote maana haijafunikwa na haiko salama.


Unaweza kudhania pesa zitakulinda,

Unaweza kudhania ukiwa na nyumba,magari na dhahabu nyingi zitakulinda,

Unaweza kudhania jina kubwa na kujulikana kila mahali ni ulinzi kwako,

Ila waulize,
Waliokuwa na pesa na shida ilipokuja ikazishinda-kuna vitu pesa haina majiibu yake

Waulize waliokuwa na majumba,magari na dhahabu,,kuna shida ziliwavamia hata hizi asset hazikua na msaada kwao,

Waulize watu maarufu,,watakwambia kuna saa hata majina yao hayana msaada kwao,walotafuat nani anawajua,na hakukua hata na mmoja wao aliyejitokeza!

Funikwa na mwavuli wa Yesu Kristo utakua salama muda wote!
#Ije mvua lije jua,huna mashaka kwa sababu uko salama!
#Zaburi91:1

@minna_blessed

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...