Wengine, ni Hatia.
Mtu anaishi chini ya hatia kwa sababu ya mambo aliyofanya nyuma au aliwahi kufanyiwa!
Anaishi akiwa na majuto na aibu ya Yale yaliyotokea zamani!
Anaruhusu jana yake kuitawala Leo yake na kumfanya asione mwanga wa kesho!
Anajiadhibu mwenyewe na kuteka mafanikio yake mwenyewe,
Ni kweli tu matokeo ya jana zetu,lakini sio ticket ya kuwa mfungwa wa jana yako!
Kusudi la Mungu kwako halifungwi na jana yako,
#Alimgeuza muuaji Musa kuwa kiongozi mzuri wa Waisraeli,
#Alimgeuza Gideoni mnyonge,kuwa mtu hodari na mkuu.
Mungu amebobea kwenye kuwapa watu mianzo mipya(mwanzo mpya)
Yeye ni mtaalamu kwenye hilo eneo!
Unamkumbuka Sauli kwenye agano jipya,
Kama kuna mtu asingefaa kabisa alikua ni yeye,, Ila Mungu alimgeuza kuwa mtumishi wake mkubwa sana,,na Leo hii tunasoma kitabu cha Agano Jipya ambacho sehemu kubwa ya zile barua aliziandika yeye!
Unadhani kesi ya imeshindikana??? Hapana!
Mruhusu Mungu akuoneshe sababu ya yeye kukuweka hapa duniani,usiishi tena chini ya hatia bali uishi maisha yanayoongozwa na kusudi la Mungu.
@minna_book_club_tz
@minna_blessed
# TunaendeleaKusoma
#ReadingMarathon
#JoinTheClub
#YouAreNotLateForSeptemberReading
@minna_blessed
# TunaendeleaKusoma
#ReadingMarathon
#JoinTheClub
#YouAreNotLateForSeptemberReading