Wengine hudhani akipata degree atatosheka,
Anapata degree na bado anajikuta hajatosheka, anaiendea Masters,akimaliza anakuta badooo hajatosheka,anasoma PhD anajikuta bado hajatosheka..
Wengine hudhani wakioa au kuolewa watafika Kiwango cha kutosheka,
Wanaoa au kuolewa na baadae hujikuta ile kiu ya ndani badoo haijatoshelezwa.
Wengine hudhani wakiwa na pesa,Nyumba na magari huenda
watatosheka,lakini wanajikuta wana kila kitu na bado kuna KITU
wanapungukiwa.
Wengine hudhani wakienda kuishi nje ya nchi watapata kitu cha kuwatosheleza,lakini wanajikuta badoo ndani kuna kiu inadai kutoshelezwa!
Wengine anadhani akibadili kazi akapata na mshahara mkubwa basiii hapo atakua amefikia satisfaction..kweli anapandishwa cheo au anahama kazi,anapata alichotaka, ila kuja kugundua kuwa badoo kuna kitu hakijakaa sawa!
KIU hii itatoshelezwa tu kwa kugundua kile ulichoumbiwa kufanya na kukifanya.
Ukijua kwa nini upo Duniani na ukanza kufanya yaliyokufanya uwepo kwenye sayari Dunia hapo utapata UTOSHELEVU WA KWELI.
#Utajuaje unachopaswa kufanya?
Muulize Muumba wako#
Alipokuumba alijua fika unachopaswa kuja kufanya.
Kaa nae Vizuri atakupa A-Z ya unachopaswa kufanya na namna ya kukifanya.
#Ishi Maisha Yenye Kusudi#
~Mwl Minna.

No comments:
Post a Comment