Leo tuongee kidogo kuhusu msamaha!
Msamaha una faida zaidi kwake anayesamehe, kuliko anayesamehewa!
Usiposamehe wewe ndio una HASARA, na sio yule ambae hujamsamehe!
Yeye anaendelea na maisha, huenda hajui hata kama amekuumiza hivyooo...wewe ndio unabaki na mzigo ndani!
So, the best way, ni kumsamehe!
Hakuna KOSA lisilosameheka! hata liwe kubwa namna gani!
Mungu anasamehe wauwaji sembuse wewe?
Kama unahisi umekosewa kosa kubwa sana la kutokusamehe, Muulize Yesu, aliyekufa kifo cha aibu akiwa hana kosa, na bado akasamehe!
Muulize Stephano, aliyepigwa mawe mpaka kufa, na bado akasamehe!
Kama umetendewa zaidi ya hawa,,basi unaweza kujitetea,,lakini bado haitasaidia...kwa sababu msamaha unakusaidia wewe zaidi hata kuliko unayemsamehe.
Maisha yana mengi ya kuwaza, zaidi ya kuwaza watu waliokukosea!
Usiruhusu akili yako ianze kumtafakari mtu aliyekukosea, onyesha ukomavu wa akili kwa kumsamehe na uendelee mbele!
Unajizuilia baraka zako mwenyewe, kwa kutokusamehe!
Samehe leo na utaanza kuona baraka zinakufuata!!!
#NguvuYaMsamaha##FunguoYaBaraka#
~Mwl Minna