Monday, May 16, 2016

ULINZI WA MALAIKA!


Kama wana wa Mungu tuna ahadi ya kulindwa na malaika kokote tuwapo..sawa na Neno la Mungu linavyotuambia hapo chini;


Zab91

9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe,Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zakeWakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.


Malaika ni viumbe dhahiri kabisa na ukijua kuwatumia utaona wakitenda kazi kwenye shughuli zako za kila siku.

Iweje leo hii watu huweka mawazo na msisitizo sana kwenye nguvu za Giza au wachawi kuwafuata usiku,na kusahau kuwa wapo malaika wanawalinda?

Shetani amepumbaza fikra za watu waone mashetan yana nguvu zaidi ya malaika,
Tangu hapo shetani hana nguvu kwa sababu yalishamshinda tangu zamani akatimuliwa mbinguni!
Anachoweza kukifanya ni kukujaza hofu tu!

Akihakikisha umejaa hofu vya kutosha sasa anapata mwaya wa kukulingilia na kuvuruga mambo yako.

Usipompa nafasi hawezi kuingia kwako.

Leo ijue nafasi ya malaika ambao Mungu ametupa kutuhudumia kila wakati.

Ukiwasemesha wanasikia na kutii kile Mwana wa Mungu anachowaambia.

Watumie leo!

Uwe na siku yenye Baraka tele!
~Minna
©2016.

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...