Mara nyingi tunapofanikisha kufanya jambo, huwa tunakuwa na kutoshelezwa katika lile eneo, na wengi huwa huridhika na hapo walipo na kuona sasa nimefika, na hapa panatosha!
Wanasahau kuwa yale mafanikio yanaweza kuwa ndio kikwazo cha kuzuia kuzidi na kuongezeka kwao zaidi katika hilo eneo, kwa maana ya kwamba, mtu hujikuta akiganda hapo na kuacha kufikiri zaidi namna ya kufanya zaidi ili kupata zaidi!
WATU WENGI HUJIKUTA WAKIONGELEA MAFANIKIO YALIYOPITA TU NA HAWANA JIPYA!
Unakuta mtu anasema;
Mimi nilipokuwa kijana nilikua na pesa sana,
Mimi nilipokua shule nilikua naongoza,
Mimi nilipokua nafanya kazi sehemu fulani nilifanya hiki na kile,
Mimi nilikuwa naomba sana,
Mimi nilikuwa nahubiri hadi watu wanaokoka,
n.k
ndio ulifanikisha hayo lakini je sasa umefanya nini?
Vipi kuhusu sasa?
Kama kila unachoogea ni cha wakati uliopita(past) tu na sio wakati uliopo unaoendelea(present continuous) jua kuna shida mahali.
Yaliyopita ni historia tayari, na yanapaswa tu kukupa hamasa na kufanya zaidi sasa.
USIBWETEKE KWA SABABU YA MAFANIKIO YALIYOSHAKUA HISTORIA!
FANYA SASA, ONGEA YA SASA!
Kuridhika na yaliyokwisha pita hutengeneza kiburi cha kuridhika, na kujikuta unadumaa mahali pamoja.
Ndipo unapoona wengine wakiendelea katika hilo eneo na kuanza kuwasema kuwaonea wivu na kuwasema vibaya ili kuharibu kile wanachokifanya.
Na wewe ukiamua kutokutosheka na hapo ulipofika unaweza kuwa zaidi ya hivyo pia.
Wazungu wanasema the sky is the limit, ila mimi naamini the sky is not the limit, you can go beyond the sky as well!
Uwezo wa kufanya zaidi uko ndani yako, wala hauko kwa mtu, hivyo usimlaumu wala kumtarajia mtu wa nje kuja na kuleta mabadiliko ndani yako.
Amua,Amka,Anza!
#ThePowerOfNow#
~Minna
@2016