Katika Kuelekea Event ya Aflewo Tanzania 2013,Siku ya alhamisi ilikuwa Bishops Breakfast Forum katika Hotel ya Regency Park Mikocheni,ikiwa ni katika kuwashirikisha Maaskofu na Mtume wa huduma mbalimbali maono na maana ya kuwepo kwa Aflewo Tanzania mwaka 2013.
AFLEWO ni neno linalosimama badala ya "Africa Lets Worship", huduma ya kusifu na kuabudu, ambapo kunakua na mikesha ya kusifu na kuabudu kila mwaka katka nchi mbalimbali barani Africa. Ilianzia Nairobi nchini Kenya mwaka 2004,na ina maono ya kuwa na usiku mmoja wa Kuomba,Kusifu na Kuabudu katika Africa ifikapo mwaka 2017. Na maono haya yanaonekana yatafikiwa maana nchi nyingi sana zimeshaanza AFLEWO na nyingine zinaendelea kujiunga2017"
Vison ya AFLEWO: " To stir up hope in Jesus across Africa throuhg annual events of Worship in Music and prayer by 2017"
Kwa Tanzania AFLEWO ilianza 2011, Dar Es Salaam na ina walezi watatu (3) ambao ni Bishop Deo Lubala,Pastor Abel Orgenes na Pastor Paul Safari.
Wanategemea kuanzisha katika miji mingine kama Zanzibar,Moshi,Mwanza na kwingine kama mambo yataenda kama walivyopanga.
Mnamo terehe 3-5-2013 BCIC Mbezi Beach itakuwa ni usiku wa aina yake katika Kumsifu na Kumwabudu Mungu ambapo Aflewo Mass Choir yenye waimbaji zaidi ya 90 watapaza sauti zao wakiimba sifa kwa Mungu.
Katika Bishops Breakfast hiyo iliyoudhuriwa na baadhi ya Maaskofu kama Apostle Ntepa,Bishop Fredie Kyara, Bishop Elly Mwende,Bishop Simtovu,Bishop Mwasota, Bishop Shegga, Pastor Fredie (UpperRoom Minisry )Bishop Gamanywa ambaye aliwakilishwa na Pastor Amoni Kilahiro na wengine wengi na kuisifu Aflewo kwa kuweza kuwakutanisha na wao kama Maaskofu katika Jiji la Dar es salaam na kuwashirikisha Maono ya Aflewo Tanzania na kusifu juhudi zinazofanywa maana ni katika Kuujenga mwili wa Kristo na kulileta pamoja Kanisa la Tanzania na Afrika Kwa Ujumla.
Pastor Paul Safari na Abel Orgenes Kama walezi wa huduma ya Aflewo Tanzania,wakieleza umuhimu wa huduma hiyo kwa waimbaji ni pamoja na kukua kwa maisha ya kiroho kati ya waimbaji na Mungu maana tofauti na uimbaji pia kuna mafundisho kuhusu Maisha ya wokovu na Maana ya Kufisu na Kuabudu kwa ujumla
Pastor Fredie Kyara aliweza kutoa ushuhuda wa jinsi Mkesha huo ulivyo wa baraka sana kwa kusema jinsi ilivyoweza kukutana na uwepo wa Mungu kwa Mkesha uliopita mwaka 2012,na kusihi Maaskofu wengine kukubali na kuunga mkono huduma hii ya Aflewo kwa kuwa ruhusu waumini wao makanisani kuhusika kikamilifu.
Kwa kumalizia Maaskofu hao walipata nafasi ya kuchangia na kusema kuwa wanakubaliana kwa nia moja na kusema wako tayari kushiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha mkesha wa Aflewo Tanzania 2013 unafanikiwa.
picha na maelezo kwa hisani ya gospelvisiontz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment