Tuesday, November 6, 2012

UKIPUNGUZIWA MITIHANI NA MAKSI NAZO ZINAPUNGUA!

Habari za Jumanne hii wapendwa wangu, natumaini mko vyema na Mungu ametupa tena siku nyingine ya kufanya kusudi lake!
Ndio, kufanya kusudi lake, na sio kuhesabu siku kama ambavyo wengine husema.Kuna watu wengi sana walitamani kuona siku ya leo lakini walishindwa, ila wewe Mungu amekupa neema hii, chukua dakika chache na umshukuru Mungu.
Leo nataka tuangalie kitu kimoja ambacho tangu utoto watu wengi wamekua hawakipendi: MITIHANI!

Wote tumefanya mitihani tukiwa shule na wengine bado tunaendelea kufanya mitihani. Na kila inapofika siku ya mitihani huwa wanafunzi wengi hawaipendi, na wengine huiita moja kati ya siku mbaya katika maisha yao ya shule.Tuangalie kwa undani kidogo ni akina nani huwa wanafanya mitihani na ni kwa nini huwa wanafanya mitihani?
Ili ufanye mtihani, lazima uwe umepitia mafunzo fulani, au kozi fulani, kwa lugha nyingine lazima uwe mwanafunzi. Utahitajika kufanya mtihani na ufaulu ili uweze kwenda kwenye hatua nyingine.Mitihani inakuwezesha kwenda hatua nyingine. Bila kufanya mtihani na kufaulu, hutajua kama umefuzu kwenda hatua nyigine.Na maksi ndio huwa kipimo cha kujua kama umefaulu au utarudia tena mtihani.Mitihani ikiwa michache maksi nazo zinakua chache!Kama kufaulu form 4 unahitaji mitihani saba ukafanya mitano, hata kama ukifaulu yote, lakini maksi hazijafikia bado hutakua umefaulu!
Ndio maana wanafunzi wanapofanya mitihani huwa wanapimwa uwezo wao katika level waliyopo kama wanastahili kuendelea na level nyingine ya juu.


Katika maisha ya kawaida huwa kuna mitihani pia ambayo kila mtu anaipitia, na anapofuzu anaenda level nyingine.
Pale ambapo utaogopa mitihani ina maana kwa lugha nyingine unaogopa kwenda level nyingine ya maisha.Na usipopiga hatua katika level nyingine ina maana hutakua na maisha yenye mabadiliko.
Usiogope mitihani, wala usichukie mitihani kwa sababu ndio itakayokuruhusu kuingia hatua nyingine.
Wakati mwingine unajiuliza mbona kitu hiki kinajirudia kile kile katika maisha?mbona jaribu ni lile lile kila siku?
Ujue bado katika hile eneo hujafaulu huo mtihani, ndio maana inabidi uendelee kulifanyia mtihani hadi utakapofaulu ndipo utavuka kwenda level nyingine.
Hata shule mwanafunzi asipofaulu mtihani, si hua anarudia hadi atakapo faulu ndipo anaenda hatua nyingne? Kama hajafikisha maksi anarudia hadi zitakapo fika?Sembuse katika maisha!
Ili usirudie rudie mtihani, lazima ujue ni wapi ulipokosea ili upajifunze zaidi na mtihani utakapokuja usikosee tena, na uweze kufaulu kwenda hatua nyingine!
Usipojifunza pale ulipokosea, utaendelea kukosea na kuendelea kurudia mtihani hadi utakapofaulu.
Na utakaposhinda unavuka daraja na kwenda hatua nyingine.Ndipo utasikia mtu anasema hapo nlikuaga sipawezi kila siku nlikua nakosea, ila siku alipoweza alienda hatua nyingine na kukutana na mitihani mingine!
Penda mitihani, kwa sababu inakupa kujijua umefikia wapi katika hatua zako za maisha, na pia mitihani inakupa ruhusa ya kwenda kiwango kingine au hatua nyingine!
kumbuka: UKIPUNGUZIWA MITIHANI UTAPUNGUZIWA NA MAKSI!

No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...