Friday, September 7, 2012

If you don't know your tittle, you do not know the authority you have! Usipojua nafasi yako au cheo chako, hutaweza kujua mamlaka uliyonayo.



If you don't know your tittle, you do not know the authority you have!
Usipojua nafasi yako au cheo chako, hutaweza kujua mamlaka uliyonayo.


Mamlaka hutokana na cheo chako au nafasi yako uliyonayo. Rais kwa mfano, bila cheo alichonancho ni mtu wa kawaida tu kama mtu mwingine yeyote. Nafasi yake ndio inamfanya awe na mamlaka aliyo nayo.Askari bila cheo alichonancho hana mamlaka yeyote ya kufanya kazi ya uaskari. Kadhalika mama au baba kwenye familia asipojua nafasi yake au cheo chake kama mama au baba,hawezi kujua mamlaka aliyonayo katika familia.

Mpaka utakapojua nafasi au cheo chako ndipo utakapojua mamlaka uliyonayo katika eneo fulani.Iwe ni nyumbani, au kanisani, au katika eneo lako la kazi.Sio lazima uwe na cheo kikubwa, kama mkurugenzi au mwenyekiti wa sehemu fulani au meneja fulani ndio utumie mamlaka uliyonayo, kila mtu ana nafasi fulani katika eneo alilopo.Hata muuza machungwa ana nafasi yake katika eneo alilonalo, kuhakikisha anapanga machungwa yake vizuri  na kwa usafi yakaweza kununuliwa! Asipotambua nafasi yake hapo, hawezi kutumia mamlaka aliyonayo.

Kadhalika mkristu yeyote asipojua nafasi yake hawezi kujua mamlaka aliyonayo. Mamlaka katika eneo husika hutokana na nafasi mtu aliyonayo katika hilo eneo. Iwe ni kikundi cha watu au ni tasnia fulani au taaluma fulani au huduma fulani.Huhitaji kuwa mchungaji au kiongozi mkubwa sana kanisani ndio utumie mamlaka uliyonayo, hapo hapo ulipo una nafasi kubwa ya kutumia mamlaka uliyonayo ikiwa utagundua nafasi yako au cheo chako.

                                King of the jungle!

Mnyama Simba ambae wote tunamfahamu anaitwa 'King of the jungle' au mfalme wa mwitu, lakini tumwangalie huyu simba ana nini hadi kuitwa hivyo?
Simba sio mnyama mkubwa kuliko wote,wala sio mnyama mrefu kuliko wote, wala sio mnyama mjanja kuliko wote, wala sio mwenye mbio kuliko wote, wala sio mnyama mwenye nguvu kuliko wote.
Simba ni mnyama ambaye aliijua nafasi yake toka mwanzo na akaitumia vizuri,anatumia mamlaka aliyonayo katika nafasi aliyonayo kule mwituni.
Kila mnyama akimwona simba anakuja, anakimbia. Kwa maana nyingine, ana mpa heshima yake, 'mzee wa kaya' anapita.
Simba anajua nafasi yake au cheo chake kama king of the jungle, na hivyo hutumia mamlaka aliyonayo vizuri.

Kujua nafasi yako au cheo chako inakupa uwezo wa kufanyia kazi mamlaka uliyonayo.
Kama Rais asingejua kama yeye ni Rais ina maana asingeweza kutumia mamlaka aliyonayo kama Rais.
Mwalimu asingejua nafasi alioyonayo kwa wanafunzi wake asingejua mamlaka aliyonayo.
Kutambua nafasi au cheo ulichonacho katika eneo ulilopo itakusaidia kujua mamlaka uliyonayo. Wakristu wengi sana hawajui nafasi walizonazo kwenye ufalme wa Mungu na ndio maana maisha yao hayana tofauti na watu wengine ambao hawamjui Mungu.

Hata mtoto asipojua kama yeye ndiye mrithi wa baba yake hawezi kutumia mamlaka aliyonayo kama mrithi, na Biblia inasema, mtoto huyo atabaki kama mtumwa na sio mrithi kwa sababu hajui kama yeye ni mrithi..

Mrithi anakua mrithi pale ambapo yule anayemrithisha hayupo.Na kama anayemrithisha hayupo na bado mrithishwaji yule hajui kama yeye ni mrithi ataendelea kuishi kama hali ile ya kwanza ili hali anao urithi mkubwa ambao ameachiwa na baba yake.
Huo ni mfano halisi wa maisha ya kila siku..lakini usishangae kuona kwamba hayo ndio maisha ya wakristu wengi sana, ambao wanajiita ni wakristu lakini hawajui nafasi zao au 'vyeo' vyao katika ufalme wa Mungu.

Tayari tunao urithi ambao Mungu ametupa kama watoto wake, lakini kutokana na kutokujua, mtu anaendelea kuishi maisha ya matatizo yasiyoisha, na shida zisizokoma kwa sababu tu ameshindwa kujua mamlaka aliyonayo katika nafasi yake.

Rais anapotoka madarakani, hawezi tena kutumia mamlaka aliyokuwa nayo kama Rais hapo awali,kwa sababu sio yeye aliyekua ana amuru, bali ni ile nafasi yake ndio ilikua ina amuru.Na ndio maana akiondoka adarakani, yule anayeingia madarakani, ndie anakua na mamlaka ya kuamuru vitu vifanyike.
Sio kwa sababu ni yeye kama yeye, ila kwa sababu ya nafasi aliyonayo, na ameitambua hiyo nafasi hivyo akatumia mamlaka aliyonayo.
                                Martin Luther king jr

Wote tuliomkiri Yesu Kristu, tumefanyika watoto wa Mungu,lakini sio watoto wote wa Mungu ni watumishi wa Mungu.Ila watumishi wote wa Mungu ni watoto wa Mungu.-Not all Children of God are servants of God, but all Servants of God are children of God-hii inatokana na kujua nafasi uliyonayo.
Kujua nafasi yako katika ufalme wa Mungu, ndio kutakufanya uwe mtumishi wa Mungu kutokana na kile ambacho Mungu amekuita kukifanya kwenye ufalme wake.

Kujua nafasi yako kutakuwezesha kuwa na mamlaka juu ya vitu ambavyo kitaingilia utaratibu wako wa maisha. Kwa mfano, Ukijua kwamba una mamlaka juu ya magonjwa yote ambayo unaweza kutaja, utakua na uwezo wa kuamuru yatoweke kwako. Ukijua kuwa una mamlaka juu ya umaskini na ujinga, utakuwa na uwezo wa kuamuru viondoke kwako kwa kutumia ufahamu ulionao kufanya vitu ambavyo vitaondoa umaskini na ujinga kwako.

Tambua nafasi yako uweze kutumia mamlaka uliyo nayo!





No comments:

Post a Comment

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...