RUTH 1:
Tunaona kulikua na njaa katika Israel hivyo bwana mmoja aitwae Elimeleki na familia yake wakawa wanakimbia njaa..




Wakaenda katika nchi ya Moab.umbali wa kama mile 30 au mwendo wa siku 7-10 kwa kutembea..


akiamini kupata chakula huko

Walikaa huko na Elimeleki akafa.
Wale wanae wawili wakaoa wanawake wa Moab..Opra na Ruthu.
; wakaishi miaka 10 ya ndoa.
Baadae wale wana wa Naomi nao wakafa.
Akabaki Naomi na wakweze.
Naomi akaamua kurudi KWAO Bethlehem maana alisikia Bwana ameutembelea mji kwa chakula(njaa imeisha)


.
Nacho kilikua kipindi cha mavuno.
FUNZO:
Elimeleki alikimbia mbali na Mungu(nchi ambapo Mungu aliwapa) kwa sababu ya njaa na badala ya kufanikiwa alikoenda aliishia kukutwa na mauti yeye na wanae..
Tunaona pia Abraham alikimbia njaa kufika Misri mkewe nusu wamuoe,Mungu akaingilia kati
Mwana mpotevu nae alikimbia nyumbani akidhan ataenda kufanikiwa zaidi huko mwishowe alirudi hom mikono mitupu
Uweponi mwa Mungu ni mahali salama hata kama tunaona mambo ni magumu,,tuchikilie tu Bwana atakukumbuka tuuu..huko Moab hakuna jema
KWA UPANDE WA MAMA MJANE-NAOMI.
Wakweze Naomi walikubali Kwenda nae Bethlehem,ila Naomi aliwasihi sana wabaki maana walikua bado wadogo hivyo walipaswa waolewe nao wawe na familia zao.
Mkwewe mmoja(Opra) akakubalkubaki
Lakini mkwewe wa Pili(Ruthu) akakataa..akataka Kwenda na Naomi.
NAOMI
Alikua mwanamke aliyemjua Mungu wake,aliyeishi kwa Upendo na wakweze na kuwajali na kuwatendea mema.
Alikua mwanamke aliyemjua Mungu wake,aliyeishi kwa Upendo na wakweze na kuwajali na kuwatendea mema.
maana waliishi nae zaidi ya miaka kumi,na bado walitaka kuendelea kuishi nae
Hata ulipofika wakati wa kuachana nae ikawa ngumu.
FUNZO:
Mwanamke anayemcha Mungu hutachoka kuishi nae.
Kwa kuwa Moyo wake wakati wote umejaa upendo na ukarimu.
Mwanamke anayemcha Mungu hutachoka kuishi nae.
Kwa kuwa Moyo wake wakati wote umejaa upendo na ukarimu.