Zab 117:1-2
"Halleluya
Enyi mataifa yote,msifuni Bwana,
Enyi watu wote mhimidini,
Maana fafhili zake kwetu sisi ni kuu,Na uaminifu wa Bwana ni wa milele."
Watu wote wa kabila zote na aina zote wanaitwa KUMSIFU na KUMHIMIDI Bwana.
Watu wote bila kujali kabila,dini,itikadi,uraia,tabia wala rangi!
Yaan ile kwamba ni MTU unaitwa na kuwajibika kumsifu na kumhimidi Mungu.
Kwanini?
Kwa sababu FADHILI na UAMINIFU wake ni wa milele.. Mwanadamu anaweza akakufadhili kwa muda tu,kwa wakati Fulani tu,lakini Mungu haangalii mvua wala jua,haangalii umeamkaje au utamlipa nini yeye FADHILI zake ni za siku zote(milele)
Mwanadamu anaweza kuwa mwaminifu kwa wakati tu,au kwa muda tu,,lakini Mungu UAMINIFU wake ni wa milele.. Hata unapokua sio mwaminifu yeye badooo anabaki kuwa mwaminifu!
Ndio maana mtunga zaburi anamwita KILA MTU kutoka kila mahali ili TUMSIFU HUYU MUNGU AMBAE FADHILI ZAKE NA UAMINIFU WAKE NI WA MILELE YOTE.