Wednesday, July 19, 2017

#Majira kwenye maisha: (kwa ufupi tu)


Kuna majira makuu manne kwenye maisha.
1.Asubuhi ya maisha yako
2. Mchana ya maisha yako
3.Jion ya maisha yako.
4. Usiku wa maisha yako.

1. Asubuhi.
Asubui ni kipindi toka kuzaliwa mpaka kumaliza elimu yako na kuanza kujitegemea au kujisimamia mwenyewe.
unaweza ukawa na asubuhi nzuri sana au mbaya sana. lakini hiyo haizuii wewe kuwa na mchana mzuri.
Hapa wengine husahau kuwa asubuhi huwa inapita haraka sana na kuzembea au kupuuzia maelekezo wanayopewa na walioko mchana na jioni!

2. Mchana
Ni kipindi cha kufanyia kazi maarifa yote uliyoyapata asubui, ie kutoka kwa wazazi, kutoka shuleni, kutoka kwenye maeneo mbalimbali uliyojifunza.
Ni kipindi cha kujenga maisha yako huku ukijua siku moja jua litachwea, na itakua jioni.
Hapa vijana wengi hujisahau na kudhani siku zote itabaki kuwa mchana, hivyo jioni huwajia kwa kushtukiza.
Wapo wanaoitumia mchana yao vizuri na kuwa na uhakika na jioni njema sana.

3.Jioni
Hiki huwa ni kipindi cha kufaidi matunda ya kazi uliyoifanya mchana.
Huwa sio kipindi cha kufanya kazi, ila kama ulizembea na kuzubaa mchana, unaikuta inakulazimu kufanya shughuli ambazo ulipaswa uwe umezifanya ilipokua mchana wako
Hiki ni kipindi cha kujiandaa na usiku. maana usku huwa hauchelewi sana ikishafika jioni.
Chochote ulichokipanda mchana, hapa jioni ndio unakivuna sasa! na kinakua dhahiri kiasi kwamba hata walioko mchana wanaona.

4. Usiku
Hiki ni kipindi cha kujiandaa kupumzika. maana sasa ni usiku. huwezi tena kufanya kazi. giza limeingia.
hapa sasa kama ulitumia mchana na jioni yako vizuri, usiku wako utakua na mwanga, hivyo hutakaa gizani.
ila kama uliutumia vibaya, usiku wako utaishia kuwa gizani na hakuna atakayejua kama upo maana hutaonekana, ni usikuu!

Nimeeleza kwa ufupi sana.Nadhani utakua umeelewa na kujua wewe uko majira gani.

na kama unatumia majira yako vizuri huku ukijua kuwa hayo majira kuna siku yatapita utaingia majira mengine na hutaweza kufanya tena yale ya majira ya nyuma!

Usipoteze muda! Tumia muda wako vizuri. Majira hayagandi.
Ubarikiwe sana!
~Minna Matee

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...