Webrania 5:13-14
13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.
14 Lakini CHAKULA KIGUMU ni cha WATU WAZIMA, ambao akili zao, kwa KUTUMIWA, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

Mara nyingi huchukuliwa kuwa mtu akiwa na umri mkubwa amakua pia amekomaa na amekua kiasi cha kuweza kuchukua na kukabiliana na majukumu mbalimbali.
#kiuhalisia kumbe sivyo.
Mtu anaweza akawa na miaka mingi lakini akili yake ni kama anamiaka miwili!
#Hivyo hivyo na maisha ya kiroho!
Kuwa na miaka mingi katika wokovu sio kigezo cha kuwa mtu huyo amekua na amekomaa kiroho!
Kuwa na miaka mingi katika wokovu sio kigezo cha kuwa mtu huyo amekua na amekomaa kiroho!
#Unaweza ukawa na miaka 10 ya wokovu na ukawa na tabia na mwenendo wa mtu aliyeokoka jana ambae anajifunza kutembea!
#Unaweza ukawa na miezi sita tu kwenye wokovu, na ukawa kama mtu mwenye miaka 5 kwenye wokovu!
#NINI HUSABABISHA HIZI TOFAUTI?
#ziko sababu nyingi,
mojawapi ni aina ya chakula unachokula na kukifanyia mazoezi.
mojawapi ni aina ya chakula unachokula na kukifanyia mazoezi.
Ukimpa mtoto chakula tu bila kumcheulisha au kumfanya acheze kile chakula hakitafanya kazi na kukua kwake kutakua na hitilafu!
#Ukila chakula kila siku na kubaki umekaa tu, chakula kile hakiwezi kufanya kazi! Lazima utoke, ufanye kazi au mazoezi ili chakula kile kifanye kazi vizuri katika mwili wako, nawe uweze kukua vizuri na kuwa na afya njema!
#Ndivyo ilivyo na maisha ya wokovu!
Aina ya chakula unachokula kinamchango mkubwa sana katika ukuaji wako.
Aina ya chakula unachokula kinamchango mkubwa sana katika ukuaji wako.
#Anapaswa kupewa vyakula vigumu, atafune mwenyewe mifupa!
#Mkristu wa miaka mitano kwenye wokovu bado anakunywa maziwa tuuuu ana hatari na afya yake.
# Unakuta bado anategemea kulishwa, hawezi kula mwenyewe, hiyo ni dalili mbaya.
#Hawezi kusoma Neno mwenyewe na kumsikia Mungu akisema nae, mpaka mchungaji wake amtafsirie kila kitu, huyo anashida kubwa.
#Hawezi kusoma Neno mwenyewe na kumsikia Mungu akisema nae, mpaka mchungaji wake amtafsirie kila kitu, huyo anashida kubwa.
#Akiumwa mafua tu anaenda kutafuta penye maombi akaombewe, huyo anashida kubwa!
#Lazima ufike umri uweze kujihudumia baadhi ya vitu, na ndio uanafunzi ambao Yesu anawafundisha wanafunzi wake.
#Aliwafundisha na baaday ya hapo akawatuma waende wakafanya kazi.
#Hawakukaa tuu wakiendelea kula bali walitoka wakaenda kufanyia kazi kile Yesu alichowafundisha na ndipo walipo kuwa na kuwa mitume wakubwa hata leo tunasoma habari zao.
#Jipime mwenyewe ujue uko wapi, ili uweze kuamka usingizini na kuishi maisha sawa na umri wako!
~ Minna Matee
@2017
@2017