Friday, September 9, 2016

JINSI YA KUONA CHANGAMOTO UNAZOPITIA KAMA FURSA NA SIO KIKWAZO-Sehemu ya 1

Yapo majira mbalimbali katika mzunguko wa dunia ,hali kadhalika maisha yana majira na nyakati mbalimbali.



Si kila siku itakua kiangazi, au kila siku itakua masika, au kila siku itakua vuli au kipupwe!
Majira ni lazima yawepo na yapo ili kutupa mazuri zaidi na mema zaidi kila siku.

Kinapokua kipindi cha masika huwa ni kipindi cha mvua nyingi, na hata mfumo wa maisha hubadilika.

Huwezi kukuta mtu amevaa fulana nyepesi wakati wa mvua kwa sababu anahitaji nguo nzito inayousitiri mwili wake dhidi ya hali ya hewa ya wakati huo.

Lakini pia huwezi kukuta mtu amevaa koti kubwa wakati wa kiangazi, vinginevyo atakua na matatizo ya kiafya. Lazima atavaa nguo nyepesi inayopitisha hewa kwa sababu kipindi cha kiangazi ni kipindi cha jua kali na joto jingi.

Kwa mmoja majira fulani yanaweza kuwa changamoto ila kwa mwingine yakawa fursa.

Kwa mfano, kipindi cha kiangazi ni fursa kubwa sana kwa mfanya biashara anayeuza barafu kwa sababu ni wakati ambao barafu huhitajika sana.

Lakini kipindi hiki ni changamoto kwa muuza myavuli, kwa sababu kwake hatauza sana kwa sababu sio msimu wake.
Kadhalika majira yanapobadilika na kuwa masika, muuza barafu kwake ni changamoto kupata wateja, lakini kwa muuza myavuli ni fursa kwake kwa sababu yeye ndio atakua anahitajika zaidi kwa kipindi hiki.

Vivyo hivyo katika maisha ya kila siku kuna majira mbalimbali(Mhubiri 3:1).
Kuna wakati wa kuwa na vingi na kuwa na vichache. Kuna wakati wa kupita kwenye hali ngumu na wakati wa kupita kwenye utele.

Sasa basi, unawezaje kufanya majira yote yakawa fursa kwako na sio tatizo, na ukayafurhia yote yanapokuja kwako?

...Ungana nami kesho hapa hapa tuendelee

~Minna
*Furahia maisha kila siku*

MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...

Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...