Habari ya Asubui msomaji wangu,
Asubui ya leo nimeona ni share nawe jambo hili kwa ufupi, naamini litakutoa mahali na kukupeleka mahali.
Kwanza kabisa KILA mwanadamu anakitu ambacho Mungu ameweka ndani yake.yaani kila mwanadamu ana talent ambayo Mungu alipomuumba aliiweka ndani yake.
Na kila kitu ambacho Mungu ameweka ndani ya mwanadamu ni kwa kusudi maalumu, na kazi maalumu.
Kitu hiki ni kama mbegu.Wote tunajua mbegu ndogo yaweza kuzaa msitu mkubwa.na kwa mbegu moja tu iliyopandwa mahali leo hii tunaona misitu mikubwa sana.
Ndivyo ilivyo kwa vile vitu Mungu alivyoweka ndani yetu. Ni mbegu tu.
Wengi wetu huvidharau na kuona kama sio kitu kwa sababu tunataka kuuona msitu mkubwa,badala ya kuitunza ile mbegu na kuimwagilia na kuipalilia ikawa msitu mkubwa.
Mbegu hizi kwa wengine kugundulika kwa haraka sana, na mapema sana katika maisha yao, lakini kwa wengine huwa zimejificha na huenda kugundulika baadae sana maishani.
Hii ni kutokana na makuzi, mazingira tunayoishi na watu wanaotuzunguka.
Kama ambavyo ili mbegu istawi inahitaji mazingira sahihi, kumwagiliwa na kupaliliwa,hali kadhalika na kile kilicho ndani yako kinahitaji mazingira sahihi, watu sahihi na ufahamu sahihi ili kikue.
Ni jukumu la kila mtu alyeokoka kuchochea kile kilicho ndani yake kwani ni Agizo katika NENO LA MUNGU.
Mwanzo1:28,
Mungu akawabariki na Mungu akawaambia: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia na kuitiisha, na mtawale samaki wa baharini na viumbe vinavyoruka vya mbinguni na kila kiumbe hai kinachotambaa juu ya dunia.
Zaeni, maana yake iko mbegu ndani yako,ambayo yapasa kuzaa na kuongezeka, si tu kuongezeka bali kujaa katika mazingira ilipowekwa.
Tumewekwa Duniani kuzaa na kuongezeka katika vile vitu Mungu alivyoweka ndani yetu. Huwa tunautumia huu mstari kwa habari ya kuzaa watoto, na kuongeza familia, ila tukiutazama kwa mapana zaidi, ni kuzaa na kuongezeka kwa vile vitu Mungu alivyoweka ndani yetu.
Jua tu kwamba ndani yako kuna kitu ambacho hakuna mwanadamu aliyenacho, na hatatokea mtu mwenye nacho.
Uliwahi kujiuliza kama William Gilbert na wenzake wasingepalilia mbegu iliyokua ndani yao leo hii huenda tusingekua na umeme huenda tungekua bado na vibatari, na chemli!
Au umewahi kujiuliza kama Arl-benz,Gottlieb Daimler na Whilliam Maybach wangenyamaza kimya bila kuikuza mbegu iliyokua ndani yao na kugundua ingine ya magari, leo hii tusingekua na magari huenda tungekua tunatumia punda na farasi hadi leo!
Amazingly, umewahi kujiuliza kama Mark Elliot Zuckerberg asingepalilia mbegu yake leo hii tusingekua na Facebook.Achilia mbali akina colgate,Heitz, Toyota na wengine wengi walioamua kpalilia mbegu zilizokua ndani yao na hatimae kuwa msitu mkubwa!
Mwenzetu Azam, kauteka uchumi wa jiji la Dar kwa asilimia kubwa kwa vile tu alijua kuna mbegu ndani yake na akiimwagilia tu itakua msitu mkubwa!Na leo tunaona msitu wake ulivyo mkubwa!
Si zaidi sana kwa Wana wa Mungu!!!!!!!!!!!!!!
There is greatness in each one of us! ni kitendo cha kuamua tu!AMUA LEO KUPALILIA MBEGU ILIYO NDANI YAKO, NA UTAZAA MSITU MKUBWA, UTAKAO WASAIDIA WENGI!
Kwa leo niishie hapo..
Ubarikiwe sana Mtu wa Mungu.
Uwe na jumamosi yenye baraka.
Nakupenda!
Firmina!