Habari ya Asubui msomaji wangu,
Asubui ya leo nimeona ni share nawe jambo hili kwa ufupi, naamini litakutoa mahali na kukupeleka mahali.
Kwanza kabisa KILA mwanadamu anakitu ambacho Mungu ameweka ndani
yake.yaani kila mwanadamu ana talent ambayo Mungu alipomuumba aliiweka
ndani yake.
Na kila kitu ambacho Mungu ameweka ndani ya mwanadamu ni kwa kusudi maalumu, na kazi maalumu.
Kitu hiki ni kama mbegu.Wote tunajua mbegu ndogo yaweza kuzaa msitu
mkubwa.na kwa mbegu moja tu iliyopandwa mahali leo hii tunaona misitu
mikubwa sana.
Ndivyo ilivyo kwa vile vitu Mungu alivyoweka ndani yetu. Ni mbegu tu.
Wengi wetu huvidharau na kuona kama sio kitu kwa sababu tunataka kuuona
msitu mkubwa,badala ya kuitunza ile mbegu na kuimwagilia na kuipalilia
ikawa msitu mkubwa.
Mbegu hizi kwa wengine kugundulika kwa haraka
sana, na mapema sana katika maisha yao, lakini kwa wengine huwa
zimejificha na huenda kugundulika baadae sana maishani.
Hii ni kutokana na makuzi, mazingira tunayoishi na watu wanaotuzunguka.
Kama ambavyo ili mbegu istawi inahitaji mazingira sahihi, kumwagiliwa
na kupaliliwa,hali kadhalika na kile kilicho ndani yako kinahitaji
mazingira sahihi, watu sahihi na ufahamu sahihi ili kikue.
Ni jukumu la kila mtu alyeokoka kuchochea kile kilicho ndani yake kwani ni Agizo katika NENO LA MUNGU.
Mwanzo1:28,
Mungu akawabariki na Mungu akawaambia: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia
na kuitiisha, na mtawale samaki wa baharini na viumbe vinavyoruka vya
mbinguni na kila kiumbe hai kinachotambaa juu ya dunia.
Zaeni,
maana yake iko mbegu ndani yako,ambayo yapasa kuzaa na kuongezeka, si tu
kuongezeka bali kujaa katika mazingira ilipowekwa.
Tumewekwa
Duniani kuzaa na kuongezeka katika vile vitu Mungu alivyoweka ndani
yetu. Huwa tunautumia huu mstari kwa habari ya kuzaa watoto, na kuongeza
familia, ila tukiutazama kwa mapana zaidi, ni kuzaa na kuongezeka kwa
vile vitu Mungu alivyoweka ndani yetu.
Jua tu kwamba ndani yako kuna kitu ambacho hakuna mwanadamu aliyenacho, na hatatokea mtu mwenye nacho.
Uliwahi kujiuliza kama William Gilbert na wenzake wasingepalilia mbegu
iliyokua ndani yao leo hii huenda tusingekua na umeme huenda tungekua
bado na vibatari, na chemli!
Au umewahi kujiuliza kama
Arl-benz,Gottlieb Daimler na Whilliam Maybach wangenyamaza kimya bila
kuikuza mbegu iliyokua ndani yao na kugundua ingine ya magari, leo hii
tusingekua na magari huenda tungekua tunatumia punda na farasi hadi leo!
Amazingly, umewahi kujiuliza kama Mark Elliot Zuckerberg asingepalilia
mbegu yake leo hii tusingekua na Facebook.Achilia mbali akina
colgate,Heitz, Toyota na wengine wengi walioamua kpalilia mbegu
zilizokua ndani yao na hatimae kuwa msitu mkubwa!
Mwenzetu Azam,
kauteka uchumi wa jiji la Dar kwa asilimia kubwa kwa vile tu alijua kuna
mbegu ndani yake na akiimwagilia tu itakua msitu mkubwa!Na leo tunaona
msitu wake ulivyo mkubwa!
Si zaidi sana kwa Wana wa Mungu!!!!!!!!!!!!!!
There is greatness in each one of us! ni kitendo cha kuamua tu!AMUA LEO
KUPALILIA MBEGU ILIYO NDANI YAKO, NA UTAZAA MSITU MKUBWA, UTAKAO
WASAIDIA WENGI!
Kwa leo niishie hapo..
Ubarikiwe sana Mtu wa Mungu.
Uwe na jumamosi yenye baraka.
Nakupenda!
Firmina!