MAFANIKIO NI HATUA ni kipengele katika Blog hii kinachokujia kila wiki chenye lengo la kukujuza na kukufikirisha wewe msomaji wetu kuhusu mafanikio katika nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku kwa sababu mafanikio hayatokei kwa siku moja bali MAFANIKIO NI HATUA.
Leo katika MAFANIKIO NI HATUA tutajifunza jambo moja kubwa ambalo linaweza kukupelekea wewe kufanikiwa au kubaki katika hali ile ile uliyonayo.
Unajua kuna watu wengi sana na huenda nawe ukawa mmoja wao, wanazuia baraka na mafanikiko yao kwa sababu ya maneno wanayojinenea?
Unajua kwa maneno yako unaweza kuwa kile unachotaka kuwa katika maisha?
Je, unajua kuwa maneno yako yanaonesha una mtazamo gani kuhusu maisha?
Na unajua kuwa maneno yako yanaonyesha kiwango cha ufahamu wako kuhusu maisha?
Basi kama hukujua hilo ni vema leo ukaelewa kuwa maneno unayosema kila siku kwenye maisha yako ndio yanatengeneza aina ya mtu tunayemuona leo.
Biblia inasema,mtu atashiba kwa matunda ya kinywa chake, lakini pia inasema, aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo na inasema pia mtu hunena yaujazayo moyo wake. Kwa hiyo huwezi kuongea kitu ambacho hakiko ndani yako.
Na kile unachoongea ndicho kitakua katika maisha yako.
Katika jamii tunayoishi wazazi wengi huzoea kuwaita watoto wao, majina ya wanyama, au vitu visivyo na thamani, mara utasikia we mbwa, we paka, we mjinga, mtoto kichaa wewe.. na maneno ya jinsi hiyo, na baadae katika kukua kwao watoto wakianza kuwa na tabia mbaya mzazi anaanza kujiuliza huyu mtoto ametoa wapi hii tabia wakati yeye mwenyewe ndie aliyeiumba kwa mwanae.
Watu huwa wanajisemea maneno katika maisha yao, oh, mimi siwezi, oh, kwetu huwa hatufanikiwi, oh, mi ni kilaza, ohh sie kwetu ni masikini, hatujawai kufika hata kidato cha nne, kwetu huwa tukiolewa lazima tuachike, kwetu huwa hichi kwetu huwa kile, huishi kujisemea maneno ya kushindwa na kutokufanikiwa.
Na kabla hujagundua unajikuta unaishi katika aina hiyo ya maisha, na chochote utakachoshika hakitafanikiwa,na kila utakae oa au kuolewa nae anakuacha, unajikuta umezalishwa watoto kila mmoja na baba yake, kwa sababu ulishajisemea kwetu huwa kila mtoto anakua na baba yake.
Mwanadamu amepewa mamlaka katika maneno yake, na ndio maana mambo mengi unayoyasema katika maisha yako hutokea na kuwa kweli.
Amua leo na anza leo kujisemea maneno ya baraka, maneno ya mafanikio na utaona mtazamo wako unaanza kubadilika, anza leo kuwatamkia watoto wako, maneno mazuri, waambie mwanangu una akili sana, wewe ni mtoto mwenye hekima, utafanikiwa katika maisha, wewe sio wa kushindwa n.k na utaona jinsi mtoto wako anakavyoanza kubadikia.
Anza leo kutamka maneno mazuri kuhusu uchumi wako, kuhusu ndoa yako, kuhusu, masomo yako.
Na ,maneno hayo yatakupa nguvu ya kufanya juhudi kufikia kile unachojinenena..
Tuonane tena wiki ijayo katika segment nyingine ya MAFANIKIO NI HATUA.
Firmina
+255 753 008 212
Thursday, June 20, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)
MWAPOTEA KWA SABABU HAMJUI...
Mara nyingi usichokijua huwezi kukifanya wala kukisema! kwa sababu hukijui. Yesu anawaambia wanafunzi wake, baada ya wao kushindwa kujua hat...

-
The Pencil Maker took the pencil aside, just before putting him into the box. "There are 5 things you need to know," he to...
-
Many people assume that listening and hearing are one and the same. However, there is a big difference between the two. Unless they were ...
-
Some people would say that God is against prosperity, but these ten famous Christian businessmen would disagree. In fact, they would likel...